Mama ana uchungu wa kuzaa mwaka huu. (2025-1964=61)!

Mama ana uchungu wa kuzaa mwaka huu. (2025-1964=61)!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam, Shalom!

Naongea lugha ya kiroho.

Wanaume wote wana tumbo la uzazi kama ilivyo kwa wanawake na ndani yao kuna watoto wa kiume na kike, mfumo wa uzazi wa Mwanaume umetunzwa ndani ya mwanamke, amekaimishwa kutunza na kuzaa kiumbe. Anyway tuendelee...

Tanzania ni kiumbe, kina macho mikono, miguu, kina tabia zake binafsi na kinareflect MAISHA na tabia zilizo ndani ya dude Hilo linaloitwa Tanzania, Tanzania kama kiumbe, kina Mkuu wa Anga la Tanzania aliyepewa mamlaka na walio ndani kuhakikisha yaliyokusudiwa yanatimia juu ya nchi.

Tanzania ana tabia zake tofauti na jirani yake Kenya au Uganda, mtoto huyu amelelewa upande mmoja pekee wa mama Katika makuzi yake, ndio maana hana ujasiri, uoga umemjaa.
Utakubaliana na Mimi kuwa Tanzania, tabia zake ni tofauti na Kenya Katika nyanja mbalimbali

Tanzania ni chotara, HALFCACT, Tanganyika alipata uhuru 1961, Akaoa mke aitwaye Zanzibar, Kisha wakazaa mtoto mwaka 1964, mtoto huyo ni Tanzania.


Tofauti na ndoa nyingi, baba anapofunga ndoa na mama, wanakuwa kitu kimoja Katika ulimwengu wa Roho, lakini hubaki akionekana huyu ni Baba, na huyu ni mama na huyu ni mtoto, jambo hili ni tofauti kwa Tanzania, Mtoto yupo aitwa Tanzania, mama mdogo yupo aitwa Zanzibar, baba hayupo, alichukuliwa Katika vifungo vya Giza, wale wa gizani wajua mambo haya vizuri, baba alitangazwa amekufa lakini yupo mahali, anapumua illa yupo, anaona watoto wakiteseka ila hawezi fanya chochote sababu amefungwa, ni mateka.

2025-1964=61.

Usishangae kwanini mwaka huu ni ngumu Katika majira haya ya nchi yetu,ni majira ya mimba na uchungu wa kuzaa.

Ugumu upo Sababu huu ni mwaka wa uchungu wa uzazi, ni mwaka ambao 1961,mama alikosa utulivu, alihangaika huku na kule, alikimbia peku, alivua nguo Ili kujaribu kupunguza uchungu wa mimba aliyobeba, asiweze, mwaka huu ndio siku Ile kuu ilitimia, akaingia labor na kuzaa mtoto chotara HALFCACT aitwaye Tanzania.

Mtoto huyu Tanzania HALFCACT hakuwahi kupata uhuru.

Ni Katika majira na mwaka ule ule babaye alipopata uhuru 1961, miaka Ile Ile 61mtoto anafikisha miaka 61,mwaka huu 2025.

ALIYE GEREZANI(TUMBONI )NDIYE MTOTO ANAYEHITAJI KUZALIWA.

Gereza ni TUMBO la uzazi lililomficha Mtoto anayerusha mateke tumboni kumuumiza mama mdogo Zanzibar Ili mtoto huyo aweze kuzaliwa.

Hujiulizi kwanini majira haya ambapo mama mdogo Zanzibar amekalia kiti Cha ndoa,ndio muda ambao mtoto anang'angania atoke tumboni Ili azaliwe?

Kinachopiganiwa kizaliwe SI REFORMS KATIKA ELECTION AU KATIBA MPYA PEKEE, Kinachotaka kutoka tumboni majira Yale yale Katika birthday ya 61 years ni kumtoa usukuleni Tanganyika. Narudia Tena, anatoka utumwani Tanganyika(BABA), yuaja yuaja. Kunjueni mikono kumpokea enyi wakunga. Anakuja kumtoa babaye usukuleni.

Ili uchungu wa mama mjamzuto uishe, ni shart azae mtoto, mtoto atoke tumboni, aje duniani, aje nuruni, uraiani, Ili wote tushangilie kuzaliwa mtoto.

NB: Aliye tumboni, gerezani, yupo kwa special mission ya ukombozi . abarikiwe .

Nawasilisha 🙏
 
Mtoto anarusha mateke mpaka wanataka kumnywesha sumu tumboni humo humo.

Wakifanya hivyo watadhuru mama na mtoto tumboni.
Na aina ya mimba ya aina hii ni zile mimba ambazo hauwezi KUitoa hata kwa miti shamba,

Mtoto ni lazima azaliwe ,haijalishi mama atatoka labour mzima au ...
 
Kwani mchungaji Rabbon huwa habugii hata kidogo kwa afya "damu ya Yesu" pale madhabahuni?
Nimekwambia hapo Katika mada🙄

Mtoto chotara aliyelelewa ndani ya ndoa akimwona baba Mzazi kwa miaka 3 pekee ana tatizo kubwa kimalezi.

1.Hana ujasiri wa kiume., uoga umemtawala.

2. Ulevi wa pombe, uchawa,ushabiki wa mpira, betting na mambo ya kijinga ndio ameendekeza.

In short ameroggwa, sasa mwaka huu ndio mwaka ambao uchawi umeexpire,

Nadhani umesikia huko kuna mgombea karudishiwa rushwa na pesa alizohonga wananchi.

Mambo yamebadilika.
 
Nimekwambia hapo Katika mada🙄

Mtoto chotara aliyelelewa ndani ya ndoa akimwona baba Mzazi kwa miaka 3 pekee ana tatizo kubwa kimalezi.

1.Hana ujasiri wa kiume., uoga umemtawala.

2. Ulevi wa pombe, ushabiki wa mpira, betting na mambo ya kijinga ndio ameendekeza.

In short ameroggwa, sasa mwaka huu ndio mwaka ambao uchawi umeexpire,

Nadhani umesikia huko kuna mgombea karudishiwa rushwa na pesa alizohonga wananchi.

Mambo yamebadilika.
Isije ikawa joka lipo jirani linavizia mtoto atoke limmeze!Umakini upo?
 
Back
Top Bottom