Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Hahahaaa! Hawa wazinzi bwana, bora uzinzi wao wangeufanyia mbali na watoto wao(maana vikojoleo vilishindwa kuwasiliana na akili), sasa watoto ndio wanaumia, kesho hao watoto watakuwa wazazi wa aina gani!!

Bado mnahangaika na hili jambo wakuu?
Hili lilishamalizika, hivi navyozungumza leo nimeamkia mahala pengine, ndio nimehama rasmi na kufunga ukurasa wa hilo suala, in fact ndoa ilifariki tangu 2012, kwa kua alikatalia nyumbani kwangu ikaonekana kama bado ipo kumbe ilikufa, sasa leo nimefunga zoezi
Mwisho wa wiki nachukua watoto kutoka nilipowahifadhi, biashara imeisha

Kama mnashauriana kwa ajili ya manufaa ya wengi humu hiyo sahihi, ila kama mnanishauri mm, ni sawa na kumuamsha maiti aamke
 
We ulishalileta humu acha watu walijadili, huna tena mamlaka ya kutupangia cha kuongelea labda ufute uzi.
Ila safi km umeamua kuhama maana [emoji134] [emoji134]

muangalie tu namna nzuri ya kuwalea hao watoto wenu vyema na kujaribu kupunguza damage mlioifanya kwao(maana haiwezi isha yote).
Good luck
 
Busara ya wazazi wako ni kubwa sana na unacho fanya ni utoto mtupu.siku moja utakuja kugundua hata huyo uliye nae ana mtu wake na wewe unamtunza tu . ushauri wang ni kwamba msamehe mkeo, anza maisha upya na uwarudishe watoto muwalee wewe na mke wako.
 
Mawazo yako yamepokelewa kwa moyo mmoja, watoto sasa ndio priority kubwa katika sakata hili, tunajaribu sasa kufanya damage control

Mwisho ningependa nikuulize kitu
Huyu mwanamke kukatalia kwangu kwa kipindi chote hicho, nini kimemsukuma? Lengo ni mali? Lakini kama ni mali mbona huko nyuma nilishamwambia basi tugawane mali nusu kwa nusu lakini bado akakataa, hakutoka, ww kwa mawazo yako unadhani ni nn hasa lengo lake?
 
Busara ya wazazi wako ni kubwa sana na unacho fanya ni utoto mtupu.siku moja utakuja kugundua hata huyo uliye nae ana mtu wake na wewe unamtunza tu . ushauri wang ni kwamba msamehe mkeo, anza maisha upya na uwarudishe watoto muwalee wewe na mke wako.

Chief, am sure you are not updated, hii thread ilishavuka hatua hiyo kitambo, nakusihi sasa hivi ujaribu kupitia tu mjadala kati yangu na wachangiaji wengine ili uwe current
 
Busara ya wazazi wako ni kubwa sana na unacho fanya ni utoto mtupu.siku moja utakuja kugundua hata huyo uliye nae ana mtu wake na wewe unamtunza tu . ushauri wang ni kwamba msamehe mkeo, anza maisha upya na uwarudishe watoto muwalee wewe na mke wako.

Chief, am sure you are not updated, hii thread ilishavuka hatua hiyo kitambo, nakusihi sasa hivi ujaribu kupitia tu mjadala kati yangu na wachangiaji wengine ili uwe current
 
Mungu usinipe mwanaume kama huyu naomba sana
Mimi nafikiri ombi lako ulifanyie mabadiliko kidogo, lisomeke hivi

Ee mungu niumbie moyo safi, niweze kuwa mke mwema, mwaminifu kwa mme wangu, mvumilivu katika hali zote, nisishawishike na aina yoyote ile ya tamaa kiasi cha kumsaliti mme wangu
Nidumu katika imani siku zote
In jesus name amen

Hili ndilo ombi unalostahili kuomba na sio hilo lingine, ombi hili litakuwezesha kuishi na any man in this world
 
Mmmmh! Lengo lake yeye ndio anajua, ila i can say anajutia kosa na hakutaka kuachana na wewe, au yawezekana anaogopa macho na maneno ya jamii,au anaogopa watoto watawaonaje, au........ ila majibu sahihi anayo yeye.
 
Wanaume sijui mna akili gani(na mliambiwa mzitumie kuishi nasi) kwahiyo nawe kuingiza wanawake ndani kwako huku watoto wakishuhudia"eti kisa unamkomoa mkeo" unajiona booonge la genous eti?
personally siungi mkono hilo la kuingiza mwanamke but two wrongs doesnt make right
usiniambie ngoma draw hapo
huyu mwnaamke hana akili
 
personally siungi mkono hilo la kuingiza mwanamke but two wrongs doesnt make right
usiniambie ngoma draw hapo
huyu mwnaamke hana akili
Ila mwanaume ana akili? Hapo walikutana wanaofanana, au hujui "ndege wafananao...."
 
Reactions: nao
Mwanaume kuishi na mwanamke aliyepigwa na mpigaji unamjua ni vigumu sana kusahau.wanawake wanafikir cc tupo sawa nao.ndio maana dini ya ukristo na uislam zinaruhusu kuacha mzizi.na hazikuandia mume mzinz bali ni mke mzinzi bcs mungu anajua shughuli yake bcs yy pia ni Mwanaume. Sababu nyingine zote haziruhusu kuacha mke kasoro hyo tu.inafikiri kwann mungu aliruhusu.
Kuishi na mke mzinz ni mateso makali kuvumilia ni ushujaa
 
Mmh, Aisee haya mambo sikia kwa mtu!
Lkn Kaka ulikosea kumleta mwanamke ndani very bad! Msamehe tu, japo kusamehe sio karudiana.
 
Nawaza baba kaleta mwanamke ndani, mama nae alilala na huyo mwanaume hapo ndani!???
 
Mmh, Aisee haya mambo sikia kwa mtu!
Lkn Kaka ulikosea kumleta mwanamke ndani very bad! Msamehe tu, japo kusamehe sio karudiana.
Lengo la kuleta mwanamke mwingine ndani ni kwa kuwa alikataa kuondoka, ndipo nikaona labda nimletee mwanamke ndani ataondoka na si vinginevyo
 
Narudia tena haya mambo yasikie kwa mtu usiombe yakukute! Mi nitasamehe kwa sbb ni agizo kutoka kwa Mungu ili usije nikosesha Baraka zangu! Lkn kusamehe sio lzm karudiana nisije lipiza bure!!
 

kaka; pole sana kwa mkasa uliokukuta; lakini naomba nianze na kukulaumu; pamoja na kuwa ulitendwa vibaya na mke wako wa ndoa but ulifanya kosa kubwa sana kuleta ndani kidemu chako wakati mke wako wa ndoa yupo ndani hata kama mmegombana. kosa la pili, umewakosea watoto wako kwa kuwaingizia mwanamke amabae sio mama yao, na kwa bahati mbaya tayari wamekuwa na uelewa kuwa baba na mama wana ugomvi. kosa la tatu ni wewe kuendekeza kulipiza kisasi tena kwa kubadilisha wanawake na kunywa pombe jirani na nyumbani kwako ukizani kuwa utasolve tatizo.

jambo jingine kaka yangu; kama ulifunga ndoa ya kikristu huwa haivunjwi mpaka mpaka ithibitike mahakamani kuwa kuna makosa ya kimasilahi mmeshindwana; but unatakiwa kujua kuwa; hakuna kosa lisilowezwa kusameheka hapa duniani; ndugu kuna kitu kinaitwa Temperament & Behaviour (Hulka na tabia), kaka; binadamu tumeumbwa na sifa hizo kuu mbili; kamwe huwezi kuibadili hulka ya binadamu lakini waweza kuibadili tabia; na utambue kuwa hulka sio dhambi bali tabia mbaya ndo dhambi; najua kabisa hiyo haikuwa hulka ya mke wako bali ilikuwa ni tabia tu iliojianzisha wakati wewe haupo na kwa maana hiyo unaweza kuibadili tabia mbaya ya mke wako ya kutoka nje ya ndoa kwa kuanza kumsamehe kama alivyokili na kutubu.

mrudie mkeo, leeni watoto wenu ili mjenge future nzuri ya familia yako kaka; ugonvi huwa hautatuliwi katikati ya mapigano; na kamwe tambua kwenye ndoa kuna mafarakano (conflict) but kamwe dont change the conflict into fighting; ukifanya hivyo jamii tutakuona ulikuwa bado haujakomaa kuwa na familia.

nakutakia msamaha mwema; nakuomba tafuta wimbo unaitwa "Nguvu ya Msamaha" umeimbwa na Ambwene Mwasongwe. utakukumbusha kitu huo wimbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…