Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Chukua huu ushauri aisee
 
Duh mwanaume mfanyie yote ila uzinzi noma hata akikusamehe IPO siku tu mi nalielewa hilo na wanawake mlio kwenye ndoa jitahidi sana kama huwez kuishi bila yeye usidhubutu.......kaka Fanya kinachokupa Amani,ila kwenye maamzi yako kumbuka watoto
Wazo la kuwapeleka watoto boarding liko poa na kuhusu kuoa mwanamke mwingine MTU asikutishe unaweza pata mwanamke safi tu kuliko kuishi bila Amani.
 
Ulikosea approach tangu mwanzo. Alivyoletwa na wazazi, kesho yake tu ungebeba watoto na kuwapeleka kwenye usalama then ungeondoka ukawaachia nyumba na usionekane tena. Hizo za kumletea mwanamke umemshajiweka kwenye kundi lake maana kama kuzini ameshamuonyesha kuwa nawe umezini. Either ondoka umuachie nyumba au baki usamehe maisha yaendelee.
 
Urafiki na mahusiano yangu hapana. Kuja kwangu bila ridhaa yangu ni kosa kubwa ambalo halisameheki popote pale.
Urafiki mwisho kanisani, kazini kwangu marufuku
 
Kwanza ninakupa pole sana kwa yaliyokukuta. Ninajua maumivu yake. Ninashauri umsamehe na kumpa masharti maana unakoelekea siyo kuzuri. Looks like you are totally confused. For the sake of the children and yourself msamehe tu brother maana ukifikria kuoa tena utaweza kumpata ambaye ni mbaya kuliko huyo uliyenaye. Kama ninyi ni wakristo nendeni mkamwone mchungaji wenu f kwa ajili ya kupewa ushauri. Ninashauri tena ninaomba umsamehe na anaweza kuwa mke mzuri sana hapo baadaye.
 
waonee huruma hao watoto wa shule ya msingi..,.kama wasingekua watoto ungemwachia nyumba then unafanya yako
 
Ondoka wewe tafuta nyumba hamisha watoto mkaishi kwingine huyo mwache abaki mwenyewe hapo!! akiwafuata mpaka makazi mapya kamshitaki
 


!
!
Yes mkuu. Yeye ndio wa kuondoka hapo aisee
 
Msalala Kwetu:

Kama Hukuwahi kucheat huko masomoni ni vizuri sana.

Kama tangu uoe hujawahi kucheat ni vizuri zaidi.

Lakini kama ulishawahi kulala na mwanamke mwingine kwenye ndoa ( ambapo tayari) ahh kaka msamehe. Kpimo hicho hicho unachompimia na wewe jipimie.

Unawapa watoto tabu bure, unampa dada yako tabu bure kukaa na wanao.

Tulizana. yaache maisha yaendelee. Wewe sio malaika.
 
kama ametubu na kujutia kosa lake, huna budi kumsamehe for the sake of your children. Akija mama mwingine anaweza akakuvuruga kuliko huyo.
hii isikie kwa mwingne lakn ikiwa yako ni ngumu kumesa.

Si jambo rahisi kumsamehe mzinzi
 
Namshangaa tu huyo mke..tangu 2012 hujamgusa na bado yupo? Kweli ana moyo wa ajabu..ningetamani aniazime huo moyo wake. Usiponigusa mwezi tena kitanda kimoja..bila sababu yoyote ya ugonjwa, kutakuwa hakuna ndoa kwasababu maana ya ndoa kwangu ni tendo la ndoa.
Kama alivyokushauri Miss chagga...ondoka wewe mwachie watoto hapo lakini hakikisha unawahudumia watoto wako kwa kila kitu ili wasiteseke. Siku moyo wako ukipenda kumsamehe rudi kwa mkeo. Maisha mnayoishi hapo ni maigizo, mnawaumiza sana watoto na pia mnajiumiza na nyie vile vile.
 
Kama vp mpishe uanzishe maisha mapya kimya kimya.
We uko kama mimi yani ukinisaliti nikiondoka huwa sigeuki nyuma, big up sana
 
Chief nashukuru kwa mawazo yako

Nilipona maumivu siku nyingi, usaliti ulifanyika 2012, hivyo nilisha move on, tatizo ni mwanamke kukatalia kwangu, mengine nilishayasahau
Na suala la msamaha halipo, msamaha kama binadam nilishasamehe, ila mapenzi ndio haiwezekani, sina upendo nae tena

Siwezi kuishi bila furaha kwa maisha yangu yaliyobaki duniani kisa watoto, ndio fate hiyo, cha msingi ni wapate elimu na wakae sehemu salama wakipata huduma zote
Watabaki kwa dada yangu wakilelewa hapo na kupata huduma zote
 
Kweli nakuunga mkono ni kitu kakutia aibu huyo mwanamke.
Move on
 
Ondoka wewe tafuta nyumba hamisha watoto mkaishi kwingine huyo mwache abaki mwenyewe hapo!! akiwafuata mpaka makazi mapya kamshitaki
Mama, nimeupokea ushauri wako kwa mikono miwili, umeongeza kitu kikubwa sana,
Nipo tayari kumuachia nyymba ss tutaanza upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…