Mama Anauza Sufuria 5 Kubwa za Chakula Kwa Siku: Halipi 100 Serikalini!



😁😁😁 Anataka Kodi anashindwa kutafuta Kodi katika madini, bandari n.k
 
Hivi vyakula huwa sili kwa sababu kuna wengine wanatumia mambo ya kishirikina sana ili kuvuta watu. Unaweza kutapika utumbo ukiambiwa wengine huwa wanaweka nini kwenye hiyo michuzi!
Unaweza kuta huo mwiko wa kupakua ni mkono wa mtu
 
Ndugu Jaji Mfawidhi acha kuumia kwa huyo mama kujitafutia riziki zake kwa kuvuja jasho na kukaa kwenye moto kupika. Huo ushauri wako wa kutaka serikali ichukue kodi kwa hiyo mama ntilie ungeachana nao na kujikita kuishauri serikali iongeze hata 1% tu kwenye mirabaha inayopata kwenye madini. Hiyo hela ni mara elfu ya hivyo vijisenti vya mama ntilie.
 
Mtoa mada kama ni demu namuonea huruma atakaye kuoa maana anaishi na mchawi ndani
 
Watu wa namna hii hawapaswi kulipa hata mia (100). Wanafanya ukarimu tu kwa watu. Ni kazi za mateso na kero kubwa! Pengine serikali ilipaswa kuwalipa hawa watu.
 
Kwenye hii nchi ukipata mwanya wa kukwepa kulipa kodi usijiulize mara mbili. Hizo kodi zenyewe si ndiyo hizo wanazonunulia ndege za kwenda kutalii nje kila siku!
 
Ana urafiki na mtu wa mochwari...sio wateja hao mpaka anawakemea.
 
Kwa siku hapo lazima anachukua kati ya laki 5 mpaka 7.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…