Serikali na wakuu wa nchi hawawezi kuingilia swala hili. Hili swala ni Personal au family issue. Kinachotakiwa hapa ni mambo mawili ya kufanya; jambo la kwanza ni Mzee Abdul na Nasib (Diamond Platinumz) wakae pamoja na wakubaliane kufanya utafiti wa kisayansi kuhusu vinasaba vyao na majibu yawekwe hadharani ili kila mmoja wetu katika jamaii na ulimwengu tutambue.
Jigine la kufanya kama hilo haliwezekani, ni sisi wana jamii kumchangia baba Nasib hela ili amtafute mwanasheria ambaye atamsaidia kupeleka hii issue mahakamani ili mahakama imtake au kumlazimisha Nasibu kutoa vinasaba vyake na vile vya Mzee Abdul kwenda kupimwa ili ijulikane kama Mzee Abdul kweli ni baba wa Nasibu au la sio au Mama Dangote atuthibitishie kitaalam matokeo ya kauli yake inayodai kuwa Nasib Mzee Abdul sio baba yake mzazi, vinginevyo sisi hatuna mamlaka ya kuchukua maamuzi yoyote yatakayo saidia kuleta ufumbuzi wa sibzofahamu hii.
Kama matokeo ya uchunguzi wa vinasaba wa Nasib na Mzee Abdul yataonyesha kuwa Nasib sio mtoto wa Mzee Abdul, basi mahakama itatoa hukumu ya kuthibitisha kuwa Nasib Mzee Abdul sio mtoto wake. Na hapo vitatafutwa vinasaba vya Nasib kisayansi.
Physical appearances za Nasib na Mzee Abdul inaokena kama vile Mzee Abdul ameji Clon mwenyewe, lakini kwa vile sisi binadam hatuna uwezo wa kujua nguvu za Mungu au Nature basi sayansi ya vinasaba (DNA) ndiyo mkombozi wetu wa utatatuzi wa mambo kama haya.
Ila naomba niwaambie kitu kimoja watanzania wenzangu, kama itafahamika kuwa Nasib na Mzee Abdul ni mtoto na baba na Nasib, kwa jina la kisanii Diamond Platinums, akaendelea kumkana Mzee Abdul kuwa sio baba yake na hivyo kutomtolea mchango wa maisha, basi ieleweke kuwa umaarufu wa Diamond Platinumms ni wa kimashetani, kutakuwa kuna majini yana mbeba Diamond Platinumz na masharti aliyopewa ni kuto mtambua Mzee Abdul kama baba yake na ndiyo sabau inayomfanya yeye kutokumtolea mchango wowote ule wa kimaisha, kwani Diamond Ülatnamms na Mama yake wanahofia akifanya hivyo, umaarufu alio nao na utajiri alioupata utapotea.
Nakumbuka kule kwetu Kinondoni kulikuwa na watu wenye utajiri kama huu wa kishetani, mmoja wao ambaye alikuwa maarufu sana enzi hizo ni Mwanamboka. Sasa hivi Mwanamboka imebakia historia.
Hivi ndivyo itakavyo mtokea Diamond Platinumz kama ata kiuka masharti aliyo pewa. Sioni sababu yoyote ile ya yeye kuwasaidia watu wengine na ambao hawana hata shida kubwa ya kimaisha na kumwacha baba yake akiteseka, sio tu kimaisha bali hata kimoyo na roho. Inaonekana dhahiri kuwa Mzee Adul hana amani na mambo haya anayotendewa. Anasononeka sana.