Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Hahahaha hii ingekuwa ni kweli hii familia ingelisema toka mwanzo.
Ukimuangalia Mzee Nasibu alivyo fanana na Diamond na Tifa........ kuamini kuwa huyu mzee sio mzazi wa Diamond ni ngumu sana....
Mimi naona hapa shida ni matunzo ya huyu baba ndio yameleta maneno na njia pekee ya kumzima huyu mzee ni kumkana kabisa hahahaha.
Sitokuja kushangaa kuja kusikia kuwa Tiffa au Nilan sio mtoto wa Diamond kwakuwa karma ndio ilivyo.....
Aiseeee ni vituko tuuu maana huyu mzee asingelikuwa anadai matunzo asingelidhalilishwa kabisa......................
 
Huyu Mzee Aliikosea Nin Hii Familia[emoji849]
Kwanini anang'ang'aniza asipotakiwa??

Watu hawakutaki yeye anajikomba. Halafu ni mwanaume miaka 50+ nadhani. Mbona aliishi bila wao miaka yote hiyo kwann asipambane aendelee na maisha yake halafu Amuachie Mungu tu. Na tena uzuri wenyewe ana watoto wengine wanaomkubali kwanini anamfanya Abdul kuwa spesho?? Hicho kinachomfanya amuone spesho Abdul ndo hicho wanakitumia na wao kumrudi. Aachane nao tu
 
Huyu ndio mzee Nyange mwenyewe 😇😇😇😇 duh.
Screenshot_20210115-152955.png
 
Shangaa hadi ule mbonyeo wa mashavu jamani..!!
Wametafuta njia ya kumtoa mzee kwenye familia wameipata. Ili wasiulizwe tena kuhusu mzee Abdul. Eti baba ake Diamond alikufa mama Diamond akiwa na mimba ya Diamond kwahiyo jiulize sasa mzee Abdul alikutana na huyu mama lini, je wakati huyo baba ake Ricardo momo anakufa alikua na mahusiano na mama Naseeb au walishaachana. Sema mama Naseeb aseme tu hajui kama mzee Abdul au mzee Nyange ndio baba halisi wa Diamond maana alikua anakitembeza mpaka kwa wahindi koko (baba yake Esma). Maana hata Esma hamjui baba yake amebaki kujiita Esma Dangote.
 
Wanasema.baba tafuta hel.tuu maan ukiondoka nyuma mam anabak anapandikiz roho mbay kwa mtot kuwa baba ako alininyanyas Sana na baada ya mtoto kukua anakua na kisilani na baba Koo kiukwel hao wanaongea wako sahihi kabisa mama yao ndoo chanzo nini kifanyike mama diamond avunje ukimya asem ninan mhusika
 
Habar wanajf,


Aliyesema kuwa wanawake na mama zetu tusiwaamini hakukosea leo kwani huenda wazazi wetu wa kiume walio tulea sio baba zetu.

Leo Rikardo Momo amesema kuwa mzee Abdul sio baba yake Diamond na kusema kuwa yeye na Diamond wanachangia baba na baba yao anaitwa Mzee Salim Nyange.

Haya yote yanaweza kuwa sawa lakini kwanini Diamond anaitwa Naseeb Abdul na siyo Salim Naseeb Nyange? Hivi inawezekana baba mlezi kupewa hadhi ya ubin wa mtoto au ndio mama Diamond anataka amalize mchezo?

Na kama ni kweli Mzee Abdul sio baba yake Diamond huenda mama Diamond alikataliwa hii mimba na mzee Salim Nyange akaamua kumtupia zigo mzee Abdul na bila shaka mzee alikubali kiroho safi ila huenda alikuwa anaambiwa mengi na ndugu pamoja na rafiki.

Apa hii story sioni kama ina utofauti na story iliyopo kwenye mziki wa Stamina na Profesa Jay maana namuona Diamond anamlaumu Mzee Abdul kwa kutokumlea ilihali Mzee Abdul alijua Diamond siyo mwanae na bado akaendelea kuwa baba kwa uwezo wake.

Ila sijaamini kama Mzee Abdul sio baba yake mzazi Diamond sababu sio rahisi mtoto alelewe na baba wa kambo mpaka abadilishe jina la ubin wake pia na kuwapa mpaka watoto zake jina la babu yao feki walitumia kama babu yao.

Hizi ni faulo zinataka kuchezeka hapa Mama Diamond anataka kumaliza mechi.

Picha ya uyo nyange please
 
Sasa sisi walimwengu tunaona picha utoto za Diamond akiwa na Mzee Abdul.

Huyo Naseeb Nyange yeye picha ziko wapi ??

Unajua nchi hii sasa hivi maisha yamekuwa magumu sana na kumekuwa na tatizo kubwa sana la ajira. Hali hiyo imejenga hali ya Kuabudiana sana.

Mtu akiwa na pesa kidogo au madaraka anaabudiwa kama mungu. Mpaka umetokea msamiati mpya wa chawa.

Yaani mtu akiwa na visenti au madaraka HAKOSEI.
Ukimkosoa chawa wake wanakushambulia hatari.

This is too much.
Hii nakazia kabisa
 
Mnahamishwa tu na ile interview ya esma
Muanze kujadili hili sasa

Ova
 
Back
Top Bottom