Mama Kijo Bisimba alaani kauli za Magufuli juu ya Mwanamke. Asema kauli zake hazimfai mtu aliyekalia kiti cha Ofisi ya Rais

Mama Kijo Bisimba alaani kauli za Magufuli juu ya Mwanamke. Asema kauli zake hazimfai mtu aliyekalia kiti cha Ofisi ya Rais

Natamani hizi kelele wangepiga pia kwa video za connections. Wanawake wengi wanadhalilishwa mitandaoni,uchi nje nje kijo kakaa kimya.
Ninashangaa watu wengi wameshikilia kumlaani ama kumpinga Magufuli kuhusu kauli zake za kudhalilishaji wanawake weusi! Kwa kauli zake za hadharani kuhusu rangi ya ngozi au maumbo ya mwanamke iwe ni nyeusi au nyeupe ni UDHALILISHAJI wa mwanamke kwa jumla. Katika akili zake ambazo haziendani na hiyo PhD tunayoambiwa anayo, mwanamke ni 'object' tu ya kufanyia utani!! Ajabu ya jamii ya kitanzania utasikia wanawake wenyewe wanaokaangwa kama objects (including waliosoma sana) wanashangilia, wanapiga vigelegele, wako mitandaoni kutetea kwa nguvu zote upumbavu huu eti ni utani, eti hiyo ndio mitazamo ya Wasukuma, nk!!!! Please, give me a break - huyu jamaa ni katili na anachofanya ni ukatili wa kijinsia. Wanawake wenye welewa kama mama Bisimba amkeni na mmnyime kura kwa udhalilishaji wa kijinsia. Mama Janeth Magufuri nenda ukapige kura ya "uhuru, haki, na maendeleo ya watu".
 
Kuniuliza nafanya nini hapa its a lack of tolerance. Ni kuishiwa hoja na kuanza kutoa povu
No!Wewe ulisema kuwa huwa huna haja na social media bali ni mpenzi wa movies ndiyo nikashangaa mbona uko hapa wakati hii nayo ni social media!Sasa hapo kukosa tolerance iko wapi?Siruhusiwi kushangaa pale ninapokutana na yanayoshangaza?au una maana yako ya "kukosa tolerance"?
 
Wapi nimesema sipendi social media?Pitia upya post zako uone.
Tatizo mkuu huwa 'unajifanya' unanifahamu sana wakati wala huna ulijualo. Umeandika na ukajijibu.
No!Wewe ulisema kuwa huwa huna haja na social media bali ni mpenzi wa movies ndiyo nikashangaa mbona uko hapa wakati hii nayo ni social media!Sasa hapo kukosa tolerance iko wapi?Siruhusiwi kushangaa pale ninapokutana na yanayoshangaza?au una maana yako ya "kukosa tolerance"?
 
Wapi nimesema sipendi social media?Pitia upya post zako uone.
Tatizo mkuu huwa 'unajifanya' unanifahamu sana wakati wala huna ulijualo. Umeandika na ukajijibu.
Najifanya nakufahamu sana wewe apo?Nikufahamu sana ili uongeze nini katika maisha yangu?Mimi sikufahamu sana wala sihitaji kukufahamu sana kwa sababu kukufahamu sana haina tija katika maisha yangu.
 
That's good mkuu. Well have a nice holiday.
Najifanya nakufahamu sana wewe apo?Nikufahamu sana ili uongeze nini katika maisha yangu?Mimi sikufahamu sana wala sihitaji kukufahamu sana kwa sababu kukufahamu sana haina tija katika maisha yangu.
 
Mataga atabaki kuwa mataga tu
No!Wewe ulisema kuwa huwa huna haja na social media bali ni mpenzi wa movies ndiyo nikashangaa mbona uko hapa wakati hii nayo ni social media!Sasa hapo kukosa tolerance iko wapi?Siruhusiwi kushangaa pale ninapokutana na yanayoshangaza?au una maana yako ya "kukosa tolerance"?
 
Ukimsikiliza Jiwe sana

1. Haheshimu wanawake kabisa anawaona ni watu duni kwake

2. Likely yuko very obsessed sana na mambo yale

3. Hajali kuumiza hisia za mkewe hadharani

4. Anadhani kwa kuwa ni mtu mkubwa basi anaweza kuzungumza chochote with impunity

Msikilize JPM hapa akitoa kauli za ajabuajabu juu ya mwanamke:


View attachment 1599467

Aka msukuma
 
Huyu jamaa hajitambui kabisa,nadhani hata mataifa mengi yanatushangaa inakuaje tunakuwa na rais asiyejitambua namna hii.
 
Mwanamama mtetezi wa siku nyingi wa haki za binadamu hususan za wanawake mama Kijo Bisimba, amelaani vikali kauli za Rais Magufuli anazozitoa mara kwa mara juu ya wanawake.

Akihojiwa na redio moja ya nje, Mama Bisimba amesema, kauli hizo za Magufuli zisichukuliwe kimizaha mizaha kwa sababu hizo kauli zinaweza kupelekea unyanyasaji mkubwa na ubaguzi.

Mama Bisimba amesema, haifai mtu aliyekalia ofisi nyeti kama ya raisi kutoa kauli za udhalilishaji kama huo. Ameshangaa kuona Magufuli mara kwa mara akimgeuza Mwanamke kama chombo cha mizaha.

Akieleza kwa umakini mkubwa, Mama Bisimba anasema watu wengi wanashangazwa na tabia hii ya Magufuli hadi wanajiuliza, huyu mzee ana shida gani na wanawake?.

Mama Bisimba akatolea mfano, namna Magufuli alivyokuwa akielezea uamuzi wake wa kumchagua Mama Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wake alipotoa kauli kuwa kwanza huyo mama ni mweupe mweupe.

Maelezo haya ya mama Kijo yanafuatia kauli ya juzi ya Rais Magufuli aliposema kuwataka wananchi wamchague mgombea ubunge mwanamama mmoja wa Dar ambapo alisema yeye hutoa ushirikiano mzuri wa kikazi kwa wanawake weupe na siyo wanawake weusi.

Kabla ya hapo alipokuwa huko mkoani Magufuli alisikika kwenye mkutano wa kampeni akisema kuwa atafutiwe kasichana kadogokadogo!

Huko nyuma amewahi kutoa kauli kuwa kama watu wa mikoa ya kusini wangeanzisha sintofahamu juu ya suala la Korosho, basi ambacho angeanza nacho ni kupiga shangazi zao ( yaani wanawake)

Wakati huohuo, mpinzani mkubwa wa Magufuli katika uchaguzi mkuu huu ndugu Tundu Lissu, ameendelea kuhoji kauli hizi za Magufuli, Lissu anahoji kauli ya Magufuli siku chache kabla ya kampeni pale Magufuli alipopewa jogoo akiwa njiani kutokea Lupaso, na kwa mizaha akamwambia yule mzee aliyempa jogoo kuwa laiti angekuwa nyumbani kwao huko Chato angemuozesha mama yake. Kauli hii imeleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi wameonyesha kutoifurahia kauli hiyo. Iweje mtoto awe mshenga au kuwadi wa mama yake?

MY TAKE:
Rais Magufuli aache kutoa kauli za mizaha na utaniutani juu ya wanawake. Hawa ni mama zetu, ni dada zetu, ni bibi zetu, ni wake zetu, ni dada zetu), wanastahili kuheshimiwa. Si sahihi kila wakati akishika mike basi anaanza kutoa kauli tata kuhusu mwanamke.

Kuwa kwake msukuma, au kutokea kwenye background ya jamii ya mfumo dume hakumpi uhalali kumgeuza mwanamke kama mwanasesere wa kufanyia mizahamizaha.

Yeye ni mtu mkubwa sana katika nchi, na ofisi yake ni kubwa sana. Kauli zake si tu zinaweza kuathiri wanawake humu nchini, bali zinaweza kuathiri mtu mweusi yeyote duniani kwa kuendelea kubaguliwa sababu ya rangi ya ngozi yake.

Pia kuwa raisi haimaanishi anamiliki kila mtu na kwamba anaweza kusema lolote na chochote mahali popote na eti ikawa chereko tu, hapana tunataka mtu anayekalia kiti cha rais apime kauli zake, aangalie athari yake kwa jamii kuanzia watoto wadogo hadi wazima, atazame muktadha mzima wa mahusiano ya kijamii nchini na hadi kimataifa ndo aamue kuzungumza au kuacha!. Siyo kila kitu chafaa kwa utani!

Tumewahi kuwa na maraisi wanne kabla yake, na walikuwa wakifanya utani wa hapa na pale katika mazingira muafaka, lakini hawakwenda mbali huko anakokwenda Magufuli kwenye utani juu ya utu wa mtu na rangi za ngozi.

Magufuli anaonyesha "obsession" iliyopitiliza kwenye issue za wanawake, na hili kusema kweli halifai kwa mtu mwenye hadhi ya nafasi ya ofisi aliyoikalia!.

Hapa chini ni kauli za mama Kijo Bisimba:

View attachment 1599407
Sio mizaha bali ndivyo alivyo. HANA HEKIMA na si mara ya kwanza kutoa kauli za hovyo, kuudhi, kuvunja moyo na kukanganya. Huwa hafanyi bahati mbaya na ndio maana hata zile kauli za kibaguzi kazirudia zaidi ya mara moja kipindi hiki cha kampeni.
 
Back
Top Bottom