Tutalaumu sana watanzania kutojituma.
Binafsi nimetembea mikoa yote ya Tanzania, nilichojifunza juu ya watu fulani eti wavivu watu fulani wachapa kazi NI UONGO MTUPU.
Tanzania kila mahala watu wanajituma sana ili kuishi maisha mazuri, kimsingi kila mtu hapendi dhiki na anahitaji kupata mkate WA kila siku.
TATIZO KUBWA LA TANZANIA NI MIFUMO NA UMASIKINI WA KURITHI WA JAMII NYINGI.
mfano mdogo ni Pwani ambako tunawaita wavivu, kiuhalisia sio wavivu Bali mfumo wa maisha waliorithi, mfumo wa nchi na umasikini wa vizazi vilivyotangulia.
Mfumo wa maisha ya watu wa Pwani NI ukarimu na kutojali Sana baadala yake wanafocus sana akhera na sio dunia.
Hali imewafanya kutojali kuuza ardhi, kutojali kupata kikubwa kwa njia ya dhuluma, kutofanya biashara ambazo dini inakataza.
Mfumo wa nchi pia umechangia miji mingi ya Pwani kudumaa maana hakuna setup ya viwanda wala shughuku kuu za uzarishaji mali kama migodi, nk.
Umasikini wakurithi, Familia ikiwa masikini kuna uwezekano mkubwa sana vizazi vinavyofuatia navyo kuwa masikini, watu wengi wa Pwani kutoka na utamaduni na historia vizazi huko nyuma vilikuwa masikini na havikuona sana umuhimu wa kuiishi dunia matokeo yake ni umasikini wakurithishana.
Umasikini wa fikra au kuchelewa kupata fikra kuliwafanya watu wa Pwani kutoona umuhimu wa Elimu dunia matokeo yake watu walijikita zaidi kwenye Elimu akhera bila kuzingatia Elimu dunia.
Wachaga sio wachapakazi maana hata miongoni mwao ziko familia masikini.
Wachaga kilichowabeba na kinachowabeba ni suala la kihistoria, uwepo wa wamissionary wengi ukanda wa Kilimanjaro kulipelekea wachaga wengi kwenda shule na kufanikiwa kuingia kwenye mifumo, uwepo kwenye mifumo kujisaidia kunyanyua Kaya zao na kufika hapo walipo, lingine Kwa wachaga ni ubinafsi na roho mbaya (hivi watu wa Pwani wakikosa wakagawa ardhi na kukalibisha wageni), ubinafsi wa kupeana deals na kazi wachaga wenyewe kwa wenyewe bila kuangalia watu wa makabila wengine kinawabeba sana.
Hapo mengi sana ya kuandika, tufungue bongo zetu, wavivu wapo kila jamii na wachapa kazi wapo kila jamii.
Leo tunasifiana na kukandiana huku Africa lakini Wazungu wanatusema WaAfrica wote na kutuita wavivu, JE TUKUBALI WAAFRICA WOOTE NI WAVIVU?