Mama mkwe anamhimiza mke wangu anichune; naomba ushauri

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
 
Umeandika upande mmoja wa Mama mkwe akimu-induce Binti yake akuchune, Lakini hujaonesha response ya Binti alijibu Nini au alifanya Nini kinachoonesha kukubaliana na mawazo ya Mama.

Ni kama kukuta msg katumiwa Mkeo ya kutongozwa Lakini yeye hajajibu chochote, hiyo itakufanya umtimue?

Ila kama kuna mpango wa pamoja wa aina hiyo, chukua tahadhari. Mojawapo ita Wazee Wenye hekima wa pande zote mbili, kisha liweke hadharani.
 
Daah pole ndugu upo kwenye janga kubwa mno ila wachache wanaweza kuona kama nimaigizo tuu haya.

Natamani kukupa ushauli ila muda unanibana sana.

Lakini tafakari sana huenda ushalishwa hadi limbwata.

Kwaushauli zaidi chukua namba hapo profile yangu.
 
happens. tulisema usioe kwa huruma, usioe kwa kuprove mtu, usioe kwa sifa. honestly utashtuka hata kukupenda hakupendi sema ulikuwa na pesa tu. you invest too much to walk away.
act huna pesa mapema. ujue panapo vuja.

note : hizo screenshot asizione utalogwa ndugu mwandishi,
 
Umeandika upande mmoja wa Mama mkwe akimu-induce Binti yake akuchune, Lakini hujaonesha response ya Binti alijibu Nini au alifanya Nini kinachoonesha kukubaliana na mawazo ya Mama.

Ni kama kukuta msg katumiwa Mkeo ya kutongozwa Lakini yeye hajajibu chochote, hiyo itakufanya umtimue?

Ila kama kuna mpango wa pamoja wa aina hiyo, chukua tahadhari. Mojawapo ita Wazee Wenye hekima wa pande zote mbili, kisha liweke hadharani.
Nashukuru kwa ushauri mkuu. Mke wangu alijibu: "NDIO MAMA NIMEKUELEWA". Jibu hili linaashiria kuwa lengo lao ni moja. Najuta kumfahamu huyu mama mkwe. Kumbe wakwe wa mjini wana matatizo makubwa kiasi hiki?
 
Naungia kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zangu naomba ushauri! Mimi ni mwanaume wa miaka 35 nimeoa mwaka huu mwezi wa pili na mwanamke niliyemuoa nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mitatu, ningeshamuoa tangu zamani ila kuna vikwazo vilikuwa vinazuia tusioane ikiwemo masomo na kupangilia maisha yaende sawa.

Kabla sijamuoa huyu mwanamke tulikuwa tunapanga mambo mengi mazuri, kama kujenga, kuzaa watoto, kufungua biashara, kutengeneza family ya kiMungu, jinsi tutakavyowalea watoto wetu, tuliongea mambo mengi sana. Nilimfungulia biashara ya milioni saba mwaka jana mwezi wa pili, nyumbani kwao nilikarabati nyumba yao, nikaweka masofa ya gharama, TV. king'amuzi na radio.

Nilimjengea mama yake jiko na choo cha kisasa nikawabadilisha kabisa. Sijui nilirogwa ama vipi nilijikuta nasukumwa kufanya tu na nilijikuta nampenda sana mpenzi wangu. Tumeenda hivyo hadi mwezi wa pili mwaka huu ndipo tulifunga ndoa, tukafanya harusi kubwa tu na mimi ndio nilikuwa nagharamikia nikisaidiana na familia yangu. Sasa siku kadhaa zilizopita kupitia simu ya mke wangu nimekuja kugundua kuwa mama yake anamfundisha asiwe mzembe kunichuna.

Tena sio kumfundisha, inaonekana alishamfundisha zamani sasa anamhimiza asikae kizembe ahakikishe anavuna vitu vya kutosha, imagine!! Ni kama Mungu tu kwasababu mimi sina mazoea kushika simu ya mke wangu kwahiyo alikuwa hafuti meseji japo hizo nilizofuma zimeanzia mwezi wa tatu. Anamwambia asikae kizembe hii bahati aliyoipata kwenye familia yake hakuna binti hata mmoja aliyebahatika kupata mume mwenye unafuu kama mimi.

Sasa hivi ndio akili inanirudi naanza kuunganisha matukio ya nyuma, nimemwaga sana pesa kwao yani alikuwa akiniitisha tu natuma! nimejikuta naumia mnooo najuta hata kufunga hii ndoa, nilijibana nikamfungulia duka ambalo hata mama yangu sijamfanyia hivyo. Lakini mimi nilifanya kwasababu ya kumfanya achangamke na nikikwama kulea familia tukipata watoto anisaidie.

Nimewaza mengi! Nawaza huenda hata hakuwa na nia ya kunizalia maana unawezaje kuiba mali za baba watoto wako? akiishiwa watoto watakula nini sasa? Sijamwambia kitu natafakari kwanza maana nilitaka kummaliza kabisa, niliondoka nyumbani nalala hotelini na hajui kama nimesoma meseji zake, nimezipiga picha tu niko nazo. Nahisi kichwa kinawaka moto. Naomba ushauri wa haraka nisiteketezwe zaidi🙏
Kausha nazo usimuoneshe umesoma hizo meseji, fanya kwa vitendo focus kwenye maisha ya familia hii ya kwako, kwao basi tena umeshafanya ya kutosha, labda itokee dharura ya msiba au ugonjwa.
NB: ukimuonesha umejua atakuloga ndio utoe zote.
 
happens. tulisema usioe kwa huruma, usioe kwa kuprove mtu, usioe kwa sifa. honestly utashtuka hata kukupenda hakupendi sema ulikuwa na pesa tu. you invest too much to walk away.
act huna pesa mapema. ujue panapo vuja.

note : hizo screenshot asizione utalogwa ndugu mwandishi,
Nashukuru kwa ushauri mkuu; nitachukua tahadhali.
 
Umeandika upande mmoja wa Mama mkwe akimu-induce Binti yake akuchune, Lakini hujaonesha response ya Binti alijibu Nini au alifanya Nini kinachoonesha kukubaliana na mawazo ya Mama.

Ni kama kukuta msg katumiwa Mkeo ya kutongozwa Lakini yeye hajajibu chochote, hiyo itakufanya umtimue?

Ila kama kuna mpango wa pamoja wa aina hiyo, chukua tahadhari. Mojawapo ita Wazee Wenye hekima wa pande zote mbili, kisha liweke hadharani.
Unamtetea mwanamke? Kwa hizo service zote alizotoa jamaa inaonesha dhahiri alipigwa na kitu kizito
 
Uliyoandika yote hayo nimeona ni ya kawaida sana, ila kipengele ulichosema kuwa mama yako haujamfanyia jambo la maana kwa mfano huo!! nimejikuta naumia sana.

Pole sana brother, napenda kukushauri lakini tueleze kwanza msimamo/majibu ya mkeo yalikuwaje kwa mama yake?
 
Umeandika upande mmoja wa Mama mkwe akimu-induce Binti yake akuchune, Lakini hujaonesha response ya Binti alijibu Nini au alifanya Nini kinachoonesha kukubaliana na mawazo ya Mama.

Ni kama kukuta msg katumiwa Mkeo ya kutongozwa Lakini yeye hajajibu chochote, hiyo itakufanya umtimue?

Ila kama kuna mpango wa pamoja wa aina hiyo, chukua tahadhari. Mojawapo ita Wazee Wenye hekima wa pande zote mbili, kisha liweke hadharani.
Wazee hawana uwezo wa kusuluhisha migogoro ya ndoa za kileo
 
Back
Top Bottom