Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aisee

Enhee
Wamachame wapoje?
Kuna mmoja alisababisha mjomba wangu akajiua...daaaa wale watu ni nomaaa

Wapalesitina achana nao kabisa hahahaha
 
Mkuu.. nikushauri kabisa.. huwezi shindana na mama mkwe. Hutokaa ushinde. Sisi sote ni mama wakwe watarajiwa. Haya madhaifu kwakua tunayapitia basi itapendeza endapo tukajirekebosha pindi tunapokua mama wakwe tusinyanyase mabinti wataokuwa wanaolewa na vijana wetu ili kufuta hii zana ya mama wakwe ni wabaya. Tujifunze kuwa na huruma.

Pia... asilani abadani usibebe mimba. Siyo kigezo cha kumkeep mwanaume. Kuwa single mother si dhambi ila uko tayari?

Endelea kumshawishi mpenzi wako na watu wazima wanaowazunguka wakiwamo viongozi wa dini ili kuweka mambo sawa.

Pia jitahidi kuwa karibu na mama mkwe nafsi yako ikiwa imeridhia. Ukimtembelea usiende bila kapu la vyakula shoo.. mambo yako usimwambie ila jenga urafiki tu.

Zaidi hameni mkaishi mbali zaidi na familia ya mume ili kupata amani or else watawasumbua sana.

Zaidi ya yote... jipe muda na wewe. Usiogope kisa aibu. Hapana. Haya mambo hutokea. Ni sehemu ya maisha. Kama siyo riziki haitakua salama sana. Na maybe siye.

Mungu anakupenda sana. Wewe ni wa thamani sana.
 
Mkuu umetisha sana.. Kiufupi wewe ni wife material

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Kuna mmoja alisababisha mjomba wangu akajiua...daaaa wale watu ni nomaaa

Wapalesitina achana nao kabisa hahahaha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wapoje??

Ilikuwaje?
 
Mimi ninaamini ndoa ni ya kati ya watu wawili wanaopendana. Hao wa pembeni ni Ziada tu. Imeandikwa Mwanaume ataachaje na baba yake na ataambatana na mkewe na watakuwa mwili mmoja. Nimefurahi kuwa huyo kijana anakupenda sana na ninakuhakikishia hatokuangusha huyo. Shikaneni na pendaneni mpaka kieleweke. Fungeni ndoa yenu hiyo August 2021 kwa FURAHA zote. Asiyekutaka anywe sumu.
 
Kumbe huwa una ushauri mzuri. Kule kwenye SIASA unaongea mambo ya ajabu sana
 
Yaani mama mkwe ambaye ni mama mzazi wa mume wake mtarajiwa anywe sumu?
Una utani wewe!
Mama ana nguvu Sana nyie.

Tumuombee tu kwa Mungu,kama ipo ipo tu!
 
Mimi mama mkubwa wangu Mnayakyusa aligoma kwenda kwneye sherehe ya mwanae kisa kaoa Mchagaa jamaa hata hakujali yanii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hadi leo wanadundaa alafu bro kafanikiwa kichiziii yani. Mama ake hajawahi kwenda kwa mwanae hata siku moja yani hataki hata kusikia!! Hapo bro alishazaa na wanawake watatu tofauti ambapo mama yake aliwakataa wawili huyu wa nne bro akasema liwalo na liwee yani

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Tatizo linaweza lisiwe tatizo ila kulifanya tatizo lisionekana linaweza kuwa zaidi ya tatizo
Mwaga mchele kwenu ...waambie kila kitu
Huondoe mzigo wakutaka kulisolve tatizo peke yako
 
Yaani mama mkwe ambaye ni mama mzazi wa mume wake mtarajiwa anywe sumu?
Una utani wewe!
Mama ana nguvu Sana nyie.

Tumuombee tu kwa Mungu,kama ipo ipo tu!
Nguvu gani? Mtu unaongilia mpaka mahusiano ya watoto kisa ukabila? Ingekuwa ni tabia fulani mbaya ningeunga mkono ila siyo ukabila.
Mama hao hao kuna ambao wameingilia ndoa za watoto wao mpaka zinasambaratika. Mama asiyejua kujenga familia SIYO MAMA HUYO ILANI MVUNJA NYUMBA.
 
Pole miss chuga . Lakini hata mimi kidogo nina shida na mabinti wa mlimani !!. Unajua ni kwanini ?. Ni kwa sababu ukimuoa tu atakulazimishe (ki mapenzi) mkajenge Kilimanjaro . Na ki kwetu kujenga kwao na mwanamke, kabla ya kufanya hivyo kwetu ni haramu. Na hapo ndipo ninapo shida.

Mambo mengine mko sawa tu.
 
Unaona sasa. Yaani mtoto unamkatalia mabinti tena amezaa nao halafu eti utegemee mabinti zako au wajukuu zako wa kike watafanikiwa. Kuna familia mabinti na wajukuu wanazalia tu nyumbani kumbe ukichimbua utakuta ni manunguniko ya mabinti waliozalishwa huko nyuma na kuacha. Akitamka laana inafuata kizazi cha kike mpaka cha nne unashangaa wanazalishwa na hawaolewi.

Mimi wanaopendana makabila tofauti huwa naulizia wazi mbele yao wote kuwa makabila yenu haya mnafahamiana vyema dos and donts? Mnakubali kuyaishi? Wakijibu ndiyo sina pingamizi. Muhimu wapendane na wawe na life vision ya kuwapeleka mbele kimaisha. Full stop.
 
Kweli wakati mwingine maovu tunayoyapanda kwa watu, yanarudi kwa watoto wetu wemyewe wasio na hatia
 
Huyo mama usidhani hana akili hadi akurupuke tu na kuingilia
 
na nyie wachaga mbadilike tabia zenu ona sasa Yanayowakuta... Ukiwa kule kanda ya ziwa.. Story za wachaga utazisikia sana ukiwa kusini mpaka magharibi ni nyie tu na tabia zenu... Badilikeni bhana mnachowafanyiwa atu wanakiweka kama reference
 
Kuna kaukweli fulani hapa. Kuna binti wa kichagga niliwahi kudate nae. Alikuwa soft siku za kwanza but jinsi tulivyozoeana nikaona anaanza kutaka nipanda kichwani.

Mimi ni mtu wa kupenda sana mahusiano ya kudekezana na kujaliana yaani mwenzangu anapokwazika nitambembeleza hadi basi ili alainike arudi sawa pia nategemea na yeye awe hivyo hivyo kwangu.

Loh, kwa huyu binti nilinoa, alikuwa ananitengenezea swaga zile za kisela ambazo mimi huwa sizielewi kabisa. Yaani mtu ukimind jambo anakukaushia utajua mwenyewe na hata hajali....

Ikafika muda akawa akiamua lake basi hataki kubadilishwa na anakuwa mbogo.

Nikaona huyu hanijui huyu....... Anataka kujua upande wangu wa giza unafananaje.....

Nilichofanya nikakata mawasiliano ghafla tu nikakausha kama wiki nione atarespond vipi, eti nalo likakausha kimya..... Nikamblock kila sehemu nikafutilia mbali namba..... Hadi leo nimeshalisahau.....

Ni mabinti wazuri kwa muonekano na wanafaa kwaajiri ya mgegedo tu, ila ndoa adabu ya mke ni sifuri. Wanataka mwanaume uwe mkorofi. Mimi ukorofi binafsi sipendi, kuongea na mwanamke wangu kama naongea na kuruta wa jeshi sina huo utamaduni....

So kwa sisi ambao tumeshawashtukia tunawatafuna tu ila ndoa wakazitafute huko kishumundu siwezi ishi na mtu kiburi, jeuri na mkosa adabu kwa mume wake.

Maana ipo siku haina jina mtu unaweza amka vibaya ukachapa mtu makofi ukaonekana manyanyasaji wanawake.

Jamii zingine wamejaa kibao..... Ya nini kuhangaika na wachache wasio na adabu kwa mume....
 
Huwajui Wachaga wala hujawahi kuishi nao acha kuleta taharuki.
Mods wanatakiwa kufuta hii comment maana inaleta taharuki
Mimi shuhuda nimeishi moshi na Arusha nimeona. Ndio maana wanaume wa kichagga wanaongea fulani utadhani wanafoka ndio wanaelewana na hao wake zao.....

Mimi siwezi ishi na mwanamke kishari shari. Ni aidha romantic au tusiwe pamoja kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…