Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Alivyonipa hizi taarifa nilimbembeleza sana wakae waonge awashawishi mpaka wakubali akanijibu mpaka mimi nimeamua tufunge ndoa bila wao siyo mjinga familia yangu naijua, sikukata tamaa nikaendelea kumbembeleza aweke mambo sawa akaniambia yameongelewa mengi sana mengine sitaki uyajue coz utaumia msimamo wangu tutafunga ndoa. Mimi mwenyewe sipendi kufunga ndoa ndugu wa mume hawapo najua madhara yake itakuja kutokea shida badae ambayo wao ndowangekuwa msaada Ila watashindwa kunisaidia
 
Duu, pole. Usijali Kama ni mipango ya Mungu mtaoana tu.
 
Kusema kweli mikoa ya Mbeya na Iringa kwenu ukisema unaoa uchagani hakuna anayekuelewa.....sijui wachaga waliwafanya nini wazee wetu, nimeishi mikoa yote, wazee wengi wamewasusia watoto wao Proposal za kuoa uchagani
NI KWELI NAMI NATOKEA MIKOA HIYO,

IKO HIVI:

WANAWAKE WENGI/WOTE WA KICHAGA WANAMALEZI KAMA WANAUME FLANI HIVI, TENA BORA UKAISHI NA MWANAUME KULIKO MWANAMKE WA KICHAGA.

HAWANA ZILE SIFA ZA UKIKE KIKE KAMA WANAWAKE WENGINE, NA UKIOA MCHAGA LAZIMA UWE NA MWANAMKE WA PEMBENI (NI LAZIMA, CHUNGUZA). MWANAMKE HUYU WA PEMBENI ATAKUFANYA UONEKANE MWANAUME NA ATAKUKAMILISHA KWENYE MAHITAJI YA SEX.

NA NDOA ZENYE KUDUMU ZA WACHAGA NI ZILE ZA WAO KWA WAO, KWANI UTAMADUNI WA JEURI, KIBURI,DHARAU NA UKATILI NI SEHEMU YA MAISHA YAO.LAKINI HIZI ZA MCHANGANYIKO NA MAKABILA MENGINE HAZIDUMU, KWANI TABIA HIZO NI SUMU KALI KWENYE UPENDO. ZINGINE ZIPO ZIPO TU KWA SBB YA MACHO YA WATU.

NI UKWELI HAWA WATU WANAONGOZA KUOLEWA/KUOA NA NI HAWA HAWA WANAONGOZA KWENYE TALAKA. SEMA KWENYE TALAKA HAKUNA MBWEMBWE KAMA HARUSINI.
PITIA TAARIFA ZA MIGOGORO YA NDOA NA TALAKA KULE KKKT, RITA, MAHAKAMA ZA MWANZO,NA USTAWI WA JAMII. NDOA ZA HAWA WATU SIO, NI CHACHU SANA.

SIONGEI KWA UBAYA, NI VEMA WAO KWA WAO WAKAOANA, KINYUME NA HAPO JIANDAE KWA NDOA NGUMU!
 
Dogo langu lilikomaa na kuoa mchaga, tukalikatalia mhehe na mchaga wapi na wapi.?
Akasema Kweli wachaga ni changamoto ila kwa aliyemuoa yeye yupo safi.
Tukaibariki ndoa yao.!
Kila movie lazima ianze na trela, sahiz yupo steji ya trela ila kashaa choka.
Mchaga akiigiza kupenda utasema nipo na Malaika, ila ngojea mzae muwe na vimali kidogo, wengi akili zao huwa zinajichaji.
 

Wamama mkwe sielewagi wana matatizo gani na wakwe zao Yani Karibu wote wanafanana tabia..

Chamsingi Mkifanikiwa kuoana Ni vema mkaishi mazingira tofauti na nyumbani
cha kushangaza hata huyu akiolewa baadaye atakuja kuwa mwiba kwa mke/wake za watoto wake.
 
Uko sahihi
 
Huwajui Wachaga wala hujawahi kuishi nao acha kuleta taharuki.
Mods wanatakiwa kufuta hii comment maana inaleta taharuki
 
Mkuu watu wengi wanawaamini wanaowapenda na kuwaamini kama wewe utaacha ajazwe maneno na wewe unaonesha kutomuamini hapo kweli atatetereka na maamuzi yake ila kama nyote lenu moja lako lake lake lako mbona simple tu na ahueni zaidi ni kua nakuletea mirejesho kila uchwao hiyo nafasi nzuri ya wewe kujua mashambulizi ya upande wa pili na jinsi ya kuyakabili
 
Kusema kweli mikoa ya Mbeya na Iringa kwenu ukisema unaoa uchagani hakuna anayekuelewa.....sijui wachaga waliwafanya nini wazee wetu, nimeishi mikoa yote, wazee wengi wamewasusia watoto wao Proposal za kuoa uchagani
sorry to say this na natumai watu hawataipokea in a negative way maanake maswala ya kabila na taifa ni mambo sensitive kwa tulio wengi

sijawahi kuentertain ubaguzi wa aina yoyote naamini watu wote tuko sawa na tabia depends na mtu na mtu japo maeneo anayotoka mtu pia yanachangia katika tabia yake

nadhani hii kasumba ipo kutokana na watu kushuhudia wanawake au wanaume wa maeneo Fulani kutoka mahali Fulani wakiwa na tabia za aina Fulani na ni kwa asilimia kubwa ,sasa mtu akishaona kwa mtu wa kwanza wa pili na watatu basi anatia tiki kwamba wote wako hivyo,mf tulio wengi tunaamini wakurya ni wapigaji ,wahehe wana hasira sana,waha waaminigu na wanajua kupenda n.k

Mfano mimi ninayo mifano iliyo hai katika jamii yangu

1.kuna jamaa mmoja mke kashikilia kila kitu and she wants to be the last say,yaani anamuendesha huyo jamaa sijapata ona and bora kabla hawajapata watoto,baada ya kupata watoto ndo ikawa balaa wife akawa hamjali jamaa hata kidogo ila watoto tu,mpaka kuna siku jamaa alicharuka alimbadilika mwanadada huyo mpaka hakuamini na akaondoka home mazima alikaa kitambo sana huko mpaka mwanadada alipoomba aombwe msamaha na kumwomba jamaa arudi,ilichukua muda sana kumrudisha jamaa,ila kwa sasa nafuu ipo kwa mbaaaaaliii ila bado anataka kuwa kichwa cha familia

2.kuna jamaa mwingine yeye ndo katia fora tena yeye alionywa na baba yake tokea mapema akaambiwa huko siko,hakusikiliza,basi sasa hivi ni kwamba hana undugu na ndugu yake yeyote ni yeye tu na mke wake,wakati wana vishida shida zilikuwa zinaiva vizuri tu,ila baada ya kupata vipesa vya hapa na pale uchonganishi baina ya ndugu ukaanza mara oohh kila kitu wanamtegemea mume wangu na mambo mengine mengi sana ya kukera nafsi,kifupi anataka kumuendesha mume wake na mpaka na ndugu zake,sasa kwa kuwa ndugu zake waligoma kuishi chini ya kivuli chake sasa hana undugu tena na ndugu zake kabaki yeye na mke wake tu.

3.Mwingine yuko Tanga huko,Tangu walipofunga ndoa,wazazi wa kiumeni wamekuwa wakilalamika hawapati msaada wa aina yoyote ile,kijana ni dokta na ana pesa ya kutosha tu ,sikilizia ukweni sasa wakwe wasikohoe kidogo tu atakwenda upesi na kumwaga mapene kama yote

4.Mwingine yuko Mwanza huko,yeye mke wake anadai mpaka shilingi mia tano ambayo wifi mtu aliomba kwa ajili ya kununua kitu Fulani walipokuwa matembezini pamoja,labda akawa hana chenji wakati wifi mtu yeye anaweza hata wakala wote na bili akalipia ya wote bila shida au nauli n.k aliwahi mpaka kumlipisha wifi yake 5000 kwa ajili ya mafuta ya gari ya mume wake,walipanga kwenda wote mahali basi mke kampanga wifi mtu mume wake kasema yeye hana pesa ya mafuta wifi akatoa 5000 ya mafuta just imagine dada yako leo analipishwa pesa kwa ajili ya mahali ambako wanaenda na mkeo tena kwa manufaa yao wote,nyumbani kwake wadada wa kazi hawakai hata akivuja chupa inakatwa kwenye mshahara,mdada wa kazi akiumwa pesa yake ndo itumike kwenye matibabu


So inawezekana mama kaona wanawake wawili watatu kutoka huko ambao wanaleta shida kwenye ndoa zao labda kama mimi nilivyoshuhudia hizo ndoa nne zenye mushkeli wa wake, kwa hiyo limemuathiri na akafikia muafaka kuwa wanawake wote wanaotoka huko wana tabia hizo hizo zisizopendeza kwenye ndoa,japo amebugi kama alikuwa na dhana hiyo kichwani kwa nini hakukataa na kuzuia process zote zisiendelee kuliko kusubiria mpaka wamekula ngombe mzima na kubakiza mkia tu?I think that is not fair kabisa aisee,mama ajifikirie upya.
 
Na ndokinachoniumiza hizi vurugu angefanya kabla ya mahari Mimi ningejikataa zangu ila swala la kunilipia mahari ni Kama wamenitia nuksi hata tukiachana kupata mtu nahisi itakuwa shida coz naskia kulipiwa mahari na kuvalishwa Pete ni Kama Agano
 
Asante sana Mimi na msimamo mchumba wangu naye ana msimamo Ila Mimi nakosa tu amani naona Kama inaweza fika sehemu labda akajikatia tamaa kutokana na hii changamoto maana duniani nako Kuna mengi
hilo haliwezi kutokea kama wewe utamproove wrong mama mkwe wako na huyo mume wako,

lakini ukimfanya mumeo aione ndoa chungu au kufanya mambo yoyote ambayo sio,utamfanya mumeo ajutie kutomtii mama yake sikuzote za maisha yake na utampa mama mkwe nguvu ambayo haijawahi tokea,lakini ukiwaproove walikosea kumzuia kijana wao kukoa,mumeo atatembea kifua mbele na kamwe hatojutia uamuzi wake wa kwenda kinyume na mama yake na mama utamtia aibu ambayo haina mfano wake,na wewe unaweza kuwa chanzo cha kurudisha upatano kati yake na mama yake na hilo litakuwa chachu ya mapenzi yenu sikuzote.
 
Njoo nikuoe.Acha wenge.
 
Na ndokinachoniumiza hizi vurugu angefanya kabla ya mahari Mimi ningejikataa zangu ila swala la kunilipia mahari ni Kama wamenitia nuksi hata tukiachana kupata mtu nahisi itakuwa shida coz naskia kulipiwa mahari na kuvalishwa Pete ni Kama Agano
hakunaga kitu kama hicho,kwenye mapenzi sikuzote victim huwa anakuwaga salama,kama kwa kweli hakuna tabia yoyote mbaya uliyowaoneshea au hakuna baya lolote ulilowahi kuwatendea na kama kweli wewe ni wife material na hukuwa na mawzo ya kumteka mume wako mtarajiwa na kumfanya wako pepe yako umtenganishe na wazai na ndugu zake kwa ujumla na huyo mchumba wako akaamua kukuacha turst me uko salama kabisa na utapata mtu mpaka usiamini macho yako tena ndani ya muda mfupi.

lakini kama kunaindication umeonesha za taa nyekundu,ulikuwa na mipango yako unayoijua wewe kichwani mwako mkishaoana awe wa kwako peke yako kwao ndo goodbye hapo una kila sababu ya kuogopa ikiwa huyo mchumba wako akiamua kukuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…