Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Kosa lako ni siku ya kwanza ulipo kutana na huyo mama mkwe wako.

Unaonekana ni mchaga na unajiona mchaga wa kweli.

Mara nyingi hatutaki kujifunza universal tabia, tumeshikilia vitabia vya kikabila na majisifu mengi hayo ndio matokeo.

Kuna kidada kila kukicha lazima kipost mambo ya kikwao, ujinga sana.

Kuna rafiki yangu ni mtu wa iringa alioa huko huko kwenu, lakini huyo msichana alikua anajua nini anafanya.

Kwanza alijifunza tabia za wahehe, na maneno machache ya kihehe, walipata shida sana kukubali kwamba yule dada ni mchaga.

Hadi leo, anapiga magoti kuliko hata wadada wa kihehe anapo salimia .
 
Kwo wako 4 wanaume 3 mwanamke 1 xo Nina mashemeji 2 na wifi 1 na kila nikionana na huyo dada nampokea vizuri sana hata zaidi ya ndugu zangu mpaka mwenyewe ananishanga na kila akiondoka lazma nimpe zawad aondoke nazo hata akiwa na shida akiniomba ela huwa namtumia,mama naye ni hivyo hvyo siku mwanaye anaenda nyumban lazma nimfungashie zawadi za kwenda nazo ikiwemo na Wax za mama mkwe lakn bdo wananifanyia hivi yani naumia acha tu niliwapenda sana sana kutoka moyoni hv ninavyongea imebidi hadi nibadilishe line jana kwa muda wasinipate maana bdo walikuwa wananipigia na kujidai wananipenda kinafiki wakati mtoto wao kanambia kila ktu kila nikiongea nao wakiniigizia upendo naumia sana natamani niwambie ukweli wanachonifanyia Ila sitaki ndomana line nmezitoa kwa muda ili wasinipate mpaka hasira ziishe maana hasira zinaweza nifanya niwambie ukweli wao
How many in-laws (brothers and sisters) do you have and what type of relationship do you have with them? Unawatembelea au unawakaribisha vizuri? Your hubby ni mtoto wa ngapi kwenye familia yao?
 
Baba mtu kashafariki hayupo
DU POLE SANA, WATANZANIA WENGI KWA SASA WANA CHAGAPHOBIA, USILAZIMISHE UNAWEZA UKAPOTEZA MAISHA YAKO KAMA NDUGU HASA BABA NA MAMA MKWE HAWAKUTAKI. KAMA NI WIFE MATERIAL UTAOLEWA TU.
 
Yuko sahihi..wachaga hamchelewi kuleta mgogoro wa mirathi mkishawaondoa waume zenu
 
Asante mwaya ubarikiwe ntaufanyia kazi ushauri wako
 
Bottom line wanasema nini kuonyesha kuwa hawakupendi? Mchoyo, mwizi, muongo etc. Siyo rahisi kumchukia mtu bila sababu. Kwani hubby ameelezwa nini kiasi chakutoa line?
 
Ntaleta mrejesho usijali
 
Reactions: BAK
Na Mimi ndo nawashanga binadamu wa kwanza kumchukia mtu bila sababu Ila mchumba angu ananiambia amesha wazoea ndugu zake ndo walivyo Wana tabia ya wivu sijui wanaona nafaidi kuwa na ndugu yao hata sielewi nahisi kuchanganyikiwa hutoamin ndani ya siku 3 nmeshapungua kilo 10
Bottom line wanasema nini kuonyesha kuwa hawakupendi? Mchoyo, mwizi, muongo etc. Siyo rahisi kumchukia mtu bila sababu. Kwani hubby ameelezwa nini kiasi chakutoa line?
 
Binti, kikubwa uwe umempenda kweli na ujitoe kuolewa na huyo mmakuwa wako. Mimi nke yangu ni Chagga kama wewe, wazazi wakati naoa hasa mama alikataa akisema ukioa mchagga utaenda kujenga kwao na bla bla. Nikamwambia wangu hayuko hivyo. Nikaoa mchagga wangu na sasa tuna mtoto ni zaidi ya umri wako. Kingine, kwa sasa yeye ndiye kipenzi cha mama ingawa wadogo zangu wameoa kabila letu ila hawamjali kama nke wangu anavyomjali. Kuna siku nilimuuliza kama anakumbuka alivyokuwa anasema, akasema ni maneno ya watu.

Zidisha kumleta mama mkwe karibu. Mfano ondoka huko ulipo ukae naye wiki moja alipo utaona atakavyobadilika mama mkwe wako to be
 
Huyo mama mkoloni.
Mimi ni mtu wa kusini mwanamke wangu ninayempenda ni mchaga .
Sitaki mtu yeyote aje kunipangia nimuoe nani
 
Ukoo huo utakiwi, unawaza kupeleka na mtoto asietakiwa, kumpa shida tu mtoto. Muhimu ujione una thamani kwanza kabla yake, kisha maisha yatasonga
 
Kila la heri na kama unampenda kiasi hicho usikubali kumpoteza kirahisi rahisi you have to fight for him I know that it won’t be easy especially taking into consideration that you’re fighting against the wish of Mama Mzaa Chema.

Kama mmekuwa pamoja kwa miaka mitano na yeye kukuona unastahili kuwa mkewe huyo mama hana haki ya kukatisha ndoto zenu kwa sababu tu ya kuwa Mchagga.
Ntaleta mrejesho usijali
 
Sawa naona sa hivi kuna Chaggaphobia inaendelea ila yote yaliozungumzwa nimejaribu kurelate katika Familia yetu na wake ndugu zangu waliowaoa ambao kimsingi wala siyo wachaga

1.Mnyakyusa huyu aliolewa na kwa sasa ndoa ina kama miaka minne changamoto ya hyu dada alikua mkorofi na mwenye dharau sana siyo tu kwenye familia yake tofauti na tulivyodhani bali hata kwetu sisi binafsi nakumbuka nlipita kwao Arusha kipnd hicho naelekea chuo nilichoshangaa chakula kikipikwa mezani dada wa kazi alikua akila mlo tofauti na watu wengine mfano sku ya kwanza kufika ilipikwa kuku na kitimoto nkashangaa dada yeye anakula majani ya kunde nlihuzunika mno na kumpa chakula changu nlichokua nimeongeza.

2.Mgogo Huyu nae kaolewa na ndgu yangu hana muda sana kwenye ndoa hyu nlisikia taarifa kutoka kwa watu kuwa ana Choyo,Dharau na muigizaji hatar nkashangaa hadi siku nlipothibitisha baada ya siku kupita kwao nkiwa kikazi Dom baada ya kukuta kwenye chumba chao cha dharura yan Store kukiwa na Masanduku makubwa ya nguo kama wote nlipouliza kwa beki 3 mbona nguo akasema nguo ni za mama nkamuliza zinavaliwa mbona ziko hovyo?akajibu hazivaliwi tena zimetupwa tu hko nkajiuliza si bora angewapa YATIMA au watu wasojiweza
Tukio lingine na dharau alilolifanya yule shemeji yangu nkiwa bado nipo hapo najiandaa kuondoka ni pale aliponiambia "NIMUOSHEE GARI LAKE tena alilohongwa na Bro. huku akijua mm na yeye tumelingana kiumri japo kanipita mwaka bila kusahau wadhifa wangu mm ni nani mpka anambie vile nkajikuta nimeshamjibu kwa dharau huku bwana ake yan Bro akiwa pale bila kuongea chochote

3.Mkinga,shemeji yangu yeye alikua na chuki binafsi sna juu ya ndugu na baadhi hta marafiki wa ndgu yangu na pia chao kilikua ni chao tu ilifikia kipind mdogo wetu wa kike alikua akifunga shule anapitia kwao kisha kurudi home Moshi sbbu wao wanaishi Moro na dogo alikua akisoma Moro.

Sasa shida ikaja kuna siku dogo alikua akisumbuliwa na tumbo la P akawa anaomba hawezi hta kutoka chumban kwake na hvyo akamwagiza beki tatu kilichofuata yule huyo mwanamke akamwambia beki tatu amwambie aache kujilegeza matokeo yake dogo mpka akapoteza damu nyingi na kulazwa hospitalin huku uhai wake ukiwekwa rehani. Hapo bado visa vingine kama vile kusoma text za dogo kwa lazima kwenye simu zake na kumwambia bro na mimi kuwa dogo ni mhuni

4. Mjita huyu nlipewa story yake by the way alieoa alikua ni ndugu yangu mtoto wa mjomba hyu mwanamke alikua ni Bahili to the extent hata ukifika kwake hta maji ya kunywa hupati licha ya kufunguliwa mabiashara chungu nzima na mumewe lakini hela yake kubwa ilikua haijulikan inaenda wapi yan hta chumvi hawez nunua atapigiwa mme simu
Siku mtoto kaumwa kampgia mme simu hajapokea kapigia ndgu wa mme simu haijapokelewa mtoto kazidiwa mpka kashikwa na degedege matokeo mtoto kaparalyse

#YOTE HAYA YANAAKISI NINI HASA KATIKA HUU UZI NA NYUZI NYINGINEZO KUWA WANAWAKE AU WATU KUTOKA MAKABILA MENGINE WANAONEKANA THEY ARE SO PERFECT YAN HAWANA HATA CHEMBE YA UBAYA NDANI YAO ILA KWA WACHAGA NDO WAHUNI,WAKOROFI,WAUAJI YAN KILA SIFA MBAYA NI WAO

Lakini ikumbukwe kuwa anayesisitiza UKABILA ndio mkabila Na pia kikubwa Huku JF watu wengi mnainekana kuwa na chuki binafsi tu juu ya WACHAGA au watu kutoka Kask sababu kuna kitu either wamewazidi hamna au mnataka mkiige kwao mwishowe Hamuwezi



Asaalam Aleykum
 
Na ndokinachoniumiza hizi vurugu angefanya kabla ya mahari Mimi ningejikataa zangu ila swala la kunilipia mahari ni Kama wamenitia nuksi hata tukiachana kupata mtu nahisi itakuwa shida coz naskia kulipiwa mahari na kuvalishwa Pete ni Kama Agano
Hiyo ni kweli kwa uchagani hata kwenye vitabu vitakatifu Vina depend wazazi hawataweza tena kupokea mahari mara mbili. Ila nahisi kuna Mila itatakiwa kufanyika!

Kama wazazi wa kijana wameshaanza kuleta Mushkeli na umewashawishi imeshindikana.

Ingia kwenye Maombi umuombe Mungu akuonyeshe kama huyo mume ni wako kweli ama la au ongea Na Baba yako kuna namna flani kule moshi wanafanyaga mila yao huwa wanapanda majani flani ndani ya suku flani yakichipua Basi ni barka kwako

Yasipochipua huyo si wa kwako.


Huyo kijana akikuoa Bila baraka za wazazi wake amini nakuambia hiyo ndoa Itakuwa ngumu sana since day hivi unaendaje kwenye Harusi bila Mama mkwe au Baba mkwe?

Wazazi na ndg watakuona Umemwekea Mtoto wao kitu wewe si MCHAGGA bana!!!

USILAZIMISHE!!
 
Una kibarua Inabidi sasa Umtongoze mamakwe Akukubali . achana nae kwani Wanaume wameisha? Mchagga gani unaolewa mbali hivyo?
 
Mama mkwe tayari amevuka mipaka ameonyesha sura yake halisi licha ya kijana kumvisha Binti pete hataki kujua Aibu ya binti kwa wazazi wake. Mamamkwe ni mtu mwenye Elimu ni Mwalimu. Ni mtu mwelewa ameona amwaribie binti tu sababu zikiwa ni Kabila.
 
Unaakili sana
 
Hahahahhaa na kweli watasema nmemloga japo kwetu tumeokoka sijawahi kwenda kwa mganga toka nizaliwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…