Mama mkwe nimemueleza aje amchukue binti yake kama anaona mimi namtesa

Wanawake wamageuka "competitors" wa wanaume na sio "partners".......inahitaji akili ya Hali ya juu sana kuishi na competitor
 
Wanawake wamageuka "competitors" wa wanaume na sio "partners".......inahitaji akili ya Hali ya juu sana kuishi na competitor
 
Demu wako uliyemfukuza getto alikubali kuondoka?
 
Mkuu mafundi wote tunafanya hivo pale kwa mchina ...mimi ni kama ilikuwa Bahati mbaya
Bahati haipo mbaya mkuu, chukua hii kwa faida yako, ukiwa unafanya kazi kwa Mchona au Muhindi, usiwaibie, hawa watu ni hari sana na ndiomaana huwa hawapendi kupeleka Case mahakamani, usione hajabu hata hiyo boda ikapotea na ukaendelea kupata tabu.
 
Pole sana ndugu mdau, nashindwa kumtetea mwanamke mwenzangu. Alipoambiwa kwenye shida na raha, sijui alifikiria ni hadithi. Kuna kupata na kukosa, afya na ugonjwa. Mtu wako ni muhimu kuliko hali mnayopitia

Siku ya siku neema ikikushukia tena atavaa sura gani? Pole ndugu mdau, kipindi cha mpito. Kama kuna watoto jitahidi wasikose vya msingi wakati bado unajikusanya. Sina la ziada
 
Umepiga kwenye mshono,....
 
Nataka kukukamatisha makosa wewe mwenyewe.

Ninahisi hivi:
Wakati ukimuoa ulijimwambafy sana kumuonesha uwezo wako mkubwa wa kimaisha upo juu, kwamba upo welloff, hutaki kukopa kwa mtu, wewe ni mboga7 na ulikuwa unamwachia 'maburungutu' wakati ukienda job nk nk.

Hayo yote uliyafanya mwanzo kabisa mwa ndoa yenu, mwenzako akayakariri na sasa dunia imekufosi kubadili mfumo wako.

Huyo mkeo ni aina ya wanawake wanaoitwa 'mama wa nyumbani', kachume ulete, ambaye hatakiwi kushirikishwa chochote katika mitikasi ya utafutaji.

Na mawazo ya kusurvive, yabuni wewe, yatekeleze wewe na usimshirikishe maana yeye hayamhusu, wanawake wa hivyo mbona wapo?

Kutaka kumrejesha kwao utatengeneza migogoro ya kushindwa zaidi.

Tuliza akili zako, jielekeze katika utafutaji wa ridhiki kisha badili life style yako.

Kama kurudi kwao arudi yeye mwenyewe bila ushiriki wako, akisha kuondoka urejee jukwaani hapa ili tukushauri jambo la kufanya.
 
For better for worse ni kwa wanawake tu wakiwa na matatizo tuwavumilie, hakuna application kwa mwanaume akiwa na hali ngumu.

Ni vile tunakuwa hatujui yajayo lakini ilifaa hata duka asipewe yeye mamlaka.
 
Hapo hakuna mke. Sasa mgawane mauzo pasu kwa pasu. Biashara itajiendesha vipi? Ndiyo maana wanaume tuna rip mapema. Tunabeba mizigo mingi ndani mioyo yetu.
 
Kwanini ufanyie kazi maneno ya lawama kutokana na mawazo yako mwenyewe ambayo mleta mada hata hajayaongea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…