Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Interest zangu mimi kama mtanzania (maslahi ya taifa) kwani suala ni comflict of interest.

Mkuu eti John Kennedy akiwa rais wa US, huku Bobby Kennedy akiwa mwanasheria mkuu wake, kulikuwa na conflict of interest?

Kwanza, Bobby alikuwa mshauri wa kaka yake and he proved compitency. Pili, Hawakuwa ofisi moja kama walivyo akina Malecela pale NY.

Bush kuwa rais, huku Jeb Bush akiwa Gavana, na Baba mtu akiwa rais mstaafu kuna conflict of interest?

They were all elected officials katika level mbili tofauti za serikali. Jebb alichaguliwa na wakazi wa Florida wakati Bush alichaguliwa na wakazi wa USA. Baba mtu na mwanae wamefanya kazi katika vipindi viwili tofauti.

Paul Boman akiwa waziri na mdogo mtu Mark Bomani akiwa mwanasheria mkuu wa serikali kulikuwa na conflict of interest?

Hawakuwa wizara moja au siyo?

Masha akiwa waziri na baba yake mbunge wa EAC kuna conflict of interest?

Where do they meet kiutendaji? Huu mfano hauendani na hali halisi.

Aman Karume rais wa visiwani, Ali Karume balozi wetu Germany eti kuna conflict of interest?

Amani ni muajiriwa wa SMZ wakati Ali ni muajiriwa wa SJMT

Eti mkuu unasema kuwa hapo kuna tatizo na masilahi yako wewe au ya wengine? Eti haya ya conflict of interest ni ya kweli au ni fitina tu? Hivi labda sielewi maana kamili ya conflict of interest vipi mkuu ukituweka sawa on hilo?

Sina fitinana na mtu kama ni $$$$ sisi wote tuko kiwanjani hapa na tunazitengeneza. Pamoja na kuwa huyu mama (Mongella) amechemsa na si approve matendo yake. Kama unawatetea hawa wanafamilia (the Malecelas) kuwa katika ofisi moja pale NY basi huyu mama asipigwe majungu ya kumuajiri mke wa mtoto wake. We need to be fair and balance.
 
Hizo nafasi za ubalozi kama local staff mbona sio deal kabisa jamani? Labda hao wanaotumwa toka nyumbani lakini kama ni hizi kazi ambazo hata foreigners kibao wanapewa, mimi naona sio kitu cha kushikana mashati.

Huu upendeleo upo na utaendelea kuwepo kwasababu hao ndio wanakuwa na habari kama kuna kazi na hivyo rahisi kuwaambia ndugu zao waombe kuliko kijana mwingine ambaye hana hili wala lile. Hiyo inatokea hata kwenye private companies. Hata huku majuu tunaamini 60% ya kazi zinapatikana kwa kujuana. Kadri unavyokuwa na wafanyakazi wengi wa makampuni mbalimbali unaokunywa nao bia, kucheza nao golf, au uliofanya nao kazi zamani, ndivyo inavyokuwa rahisi kupata kazi mpya ukiamua kuhama au ukipoteza kazi uliyo nayo.

Conflict of interest ni zaidi ya hao wana ndugu wawili kufanya kazi shirika moja. Sheria za kimataifa zinaeleza wazi juu ya hilo. Ni tofauti na hili la mama Mongela kumwajiri mke wa mtoto wake kama msaidizi. Hata kwenye maadili ya kawaida tu, huwa inakatazwa kuajiri ndugu yako wa karibu kama msaidizi.

Kwahiyo tunampigia kelele mama Mongella kwasababu she was making $800.00/day na mkwe wake $400.00/day? Mimi nilidhani tunaongelea suala la maadili. Naona mama Mongella amekuwa mtoto wa kambo hapa kwani suala la akina Malecelas ubalozi wa TZ UN na suala la Mongella AU ni sawa. Siyo kwasababu mke wa Malecela (Jr/baharia) hatengenezi pesa nyingi haina maana maadili yakiukwe.
 
Kama unawatetea hawa wanafamilia (the Malecelas) kuwa katika ofisi moja pale NY basi huyu mama asipigwe majungu ya kumuajiri mke wa mtoto wake. We need to be fair and balance.

Mkuu tatizo hapa ni fitina, ishu ya Mama Mongella anatuhumiwa na Umoja Wa Chi za Afrika AU, kwa kuajiri ndugu zake na kuiba hela za AU, sio sisi hapa forum, tuhuma zimetoka AU na rais wetu ameambiwa mbele ya uso wake,

Ya Malecela ni yako wewe mkuu, toka ulipoanza swali lako sio kwamba ulikuwa hueleweki unakotaka kwenda, ishu ya Mama Mongella haiteteeki na wala haina mfano, kama ni conflict of interest bado unayo nafasi ya kutuelimisha hapa, AU wamesema Mama Mongella ameajiri ndugu zake kinyume na kanuni za AU mkuu, ishu hazifanani kabisaaa!

Radhia Msuya, Mama Migiro, Mama Mwatunu, wote walikuwa serikali kwa wakati mmoja tena wizara ya nje, je kulikuwa na tatizo lako la conflict of interest au hiyo conflict imeanzia kwa Malecela?
 
Kwahiyo tunampigia kelele mama Mongella kwasababu she was making $800.00/day na mkwe wake $400.00/day?

Mama Mongella anapigiwa kelel na AU, sio sisi mkuu sisi tuntafakari tu tuliyoambia na AU!


Mimi nilidhani tunaongelea suala la maadili. Naona mama Mongella amekuwa mtoto wa kambo hapa kwani suala la akina Malecelas ubalozi wa TZ UN na suala la Mongella AU ni sawa.

Not even close mkuu, Mama Mongella ameiba na kuajiri ndugu zake kinyume cha sheria za AU, ama sivyo asingesulubiwa, kina Malecela sijui kama wavunja sheria ya kuajiriwa za nchi hebu tuwekee hapa mkuu tuache kuandikia mate mkuu!

Siyo kwasababu mke wa Malecela (Jr/baharia) hatengenezi pesa nyingi haina maana maadili yakiukwe.

Ni maadili gani hayo yaliokiukwa mkuu, tatizo hapa ni fitina tu hakuna mtoto hapa, mama Mongelal ni mwizi na ni mndugunization period, amevunja sheria za AU, kama Malecela amevunja sheria za Tanzani sema mkuu uwanja mkubwa huu hatutaki majungu bila Facts, FACTS za Mama Mongella ziko clear kuwa ameiba hela za AU, na ameajiri ndugu zake AU kinyume na sheria za AU,

Haya weka facts mkuu hapa tuchambue! Malecela angeweza kumuajiri mtoto wake kuwa daktari wake wa binafsi, kama Msuya alivyo je mkuu wangu si ndio ungekufa kabisaa? Mkuu weka sheria za nchi hapa zinasema nini kuhusu familia ya ukoo mmoja wanapoajiriwa kwa wakati tofauti, maana if yours is a point basi ina maana bongo tuna sheria zinazokataza ndugu kuifanyia kazi serikali yetu kwa pamoja, is that so mkuu au?

Sijawahi kuisikia hii mkuu, ndio maana ninasema kuna fitina hapo kwako mkuu maana ninawajua ndugu wengi sana wanaifanyia kazi serikali tena kwenye kitengo kimoja! Halafu kma Malecela anahusika na kuajiriwa kwao kama Mama Mongella anavyotuhumiwa na AU!
 
...Huyu mama mtu wa home, tunamjua vizuri tabia zake na nadhani imefikia wakati mnapotaka kumchagua mtu katika nafasi kama hizi jaribuni kwanza kuomba CV yake ya kiswahili, kabla ya hiyo ya kizungu.
....Jaribuni kupitia Taasisi zote nchini utaona kuwa viongozi wote wameweza kuzitumia nafasi zao kutoa ajira kwa ndugu zao.. ...Hilo swala la elimu kutupa nchi maendeleo ni imani ya wazungu na utaikuta ktk kamusi na vitabu vyenu nyie wasomi lakini reality ni kuwa elimu kwa mwafrika ni nyenzo itakayokuwezesha kushika nafasi ya KULA hivyo kuikomboa familia yako kiuchumi.

Pokea tano Mkuu!! Nashindwa kuongeza kitu hapo, ila kwa bahati mabya ndiyo ukweli wenyewe miaka 46 baada ya uhuru wetu.
Uliyoyaandika hapo yanaonesha jinsi Tanzania ilivyopoteza mwanamapinduzi, na jinsi huko ulipo wanavyofaidi knowkedge yako!..

Nilikuwa naombea kuwa hii ishu ya mama mongela isiwe ya kweli. Kwa bahati mbaya inalelekea kuwa ni ukweli mtupu. Binafsi nadhani baada ya kuwa CCM na kwenye Sirikali kwa muda mrefu alishajisahau, kwani CCM/Serikalini ni butua butua""BORA LIENDE"" tu, mama wa watu bila kufikiria kayapeleka hayo ya butua butua huko AU, yaani alishazoea kutoa maamuzi ya ajabu ajabu bila kuulizwa au kuwajibishwa.
 
Field Marshall es,
Nadhani jamaa hajaelewa tofauti kubwa kati ya sheria za UN, AU ama kimataifa na sheria zetu sisi Tanzania. NI kweli nakubaliana na wewe kuwa swala la mama Mongella haliwezi kulinganishwa kabisa na hilo la Malecela kisheria na pili hawa ndugu hawakujipa ajira wao isipokuwa ni uteuzi uliotolewa na mtu mwingine ama ngazi tofauti serikalini.

Mama Mongella kwa kutumia nafasi yake aliwavuta ndugu zake na kuwapa ajira kinyume cha sheria hapo ndipo utata unapokuja hali hawa kina Malecela kwanza hakuna sheria tanzania inayokataza ndugu kupeana ajira kisha sidhani kama ni malecela mmoja aliyemvuta mwingine Ubalozini....Je, ikiwa walivutana kuna haja ya sisi pia kutunga ama kutumia sheria kama za wenzetu?

Jibu langu litakuwa ndio, trust me iwe serikalini ama shirika ajira za udugu zina matatizo makubwa baina ya wafanyakazi na mara nyingi huleta husda na huyu ndugu mwajiriwa kutoshirikiana vizuri ktk uzalishaji, naye hujiona boss kwa namna fulani - conflict of interest sio neno la kutungwa ila ni kupitia majaribio mengi imeonekana kuwa binadamu hatuwezi kutumikia bwana wawili...
 
Not even close mkuu, Mama Mongella ameiba na kuajiri ndugu zake kinyume cha sheria za AU, ama sivyo asingesulubiwa, kina Malecela sijui kama wavunja sheria ya kuajiriwa za nchi hebu tuwekee hapa mkuu tuache kuandikia mate mkuu!

Hizi bado ni allegations bwana mkubwa ni makosa makubwa sana kwa mzee mzima kama wewe kukaa mbele ya keyboard yako na kuropoka maneneo kama haya. Read out loud to yourself what you just wrote and hear how you sound. This kind of conclusion suggests that you are so blinded by prejudice that you can't see things straight.

Ni maadili gani hayo yaliokiukwa mkuu, tatizo hapa ni fitina tu hakuna mtoto hapa, mama Mongelal ni mwizi na ni mndugunization period, amevunja sheria za AU, kama Malecela amevunja sheria za Tanzani sema mkuu uwanja mkubwa huu hatutaki majungu bila Facts, FACTS za Mama Mongella ziko clear kuwa ameiba hela za AU, na ameajiri ndugu zake AU kinyume na sheria za AU

These are still allegations, the lady is not convicted yet. Again, this is just a confirmation of my earlier observation that you are too prejudice.

Haya weka facts mkuu hapa tuchambue! Malecela angeweza kumuajiri mtoto wake kuwa daktari wake wa binafsi, kama Msuya alivyo je mkuu wangu si ndio ungekufa kabisaa? Mkuu weka sheria za nchi hapa zinasema nini kuhusu familia ya ukoo mmoja wanapoajiriwa kwa wakati tofauti, maana if yours is a point basi ina maana bongo tuna sheria zinazokataza ndugu kuifanyia kazi serikali yetu kwa pamoja, is that so mkuu au?

Facts gani tena unahitaji wewe? Do you really need facts or you just want an interminable 20 pages debate wakati umeisha hukumu wenzako? You even went as far as using your little scare tactics of PhD. Pamoja na vimatusi vyako vya rejareja vya fitina na majungu wakati wewe ndiye unaongoza kwa fitina na majungu. Ni kinyume na maadili kuajiri wanafamilia moja kwenye kituo kimoja cha kazi. You don't have to be an Einstein to know this.

Balozi Maharage ana ndugu yake pale Foreign alikuwa anatumia jina la Maharage. Maharage mdogo alipoajiriwa Foreign, yeye albadili jina kuepuka masuala ya maadili. Kwani huyo Malecela wa India mpaka aje UN? Si angepelekwa kituo kingine?

Sijawahi kuisikia hii mkuu, ndio maana ninasema kuna fitina hapo kwako mkuu maana ninawajua ndugu wengi sana wanaifanyia kazi serikali tena kwenye kitengo kimoja! Halafu kma Malecela anahusika na kuajiriwa kwao kama Mama Mongella anavyotuhumiwa na AU!

Wakati wowote familia ya Malecela inapotajwa unakimbilia fitina na majungu. Vilevile, kuwajua kwako ndugu wengi walioajiriwa kitengo kimoja ambayo ni kinyume cha maadali does not justfy the fact that watu wamekiuka maadili na tuendelee kukiuka maadili.

Hii ni sawasawa na umekamatwa kwa wizi halafu unasema aaah, hata John ni mwizi na ninawajua wezi wengi tu. This is very stupid argument Mr. FM.
 
tz devil,
Hawa akina Malecela pamoja na elimu waliyo nayo wana asili ya upendeleo na kukosa maadili ktk kazi tangu Mzee JS, mtoto utafiti, Watoto wa UN! Hadi leo hakuna anayejua kwa nini Mwalimu alikataa Jonh asiwepo katika Mchakato wa CCM 1995. Sorry kutoka nje ya mada- ya Mongela!
 
Are you trying to say that we have two family members in one station? Who is protecting my interest?
there's a storm a-brewing. . . .

354026960_85f41657da_o.jpg
 
tz devil,
Hawa akina Malecela pamoja na elimu waliyo nayo wana asili ya upendeleo na kukosa maadili ktk kazi tangu Mzee JS, mtoto utafiti, Watoto wa UN! Hadi leo hakuna anayejua kwa nini Mwalimu alikataa Jonh asiwepo katika Mchakato wa CCM 1995. Sorry kutoka nje ya mada- ya Mongela!

This will be interesting...nadhani dawa ni kupata popcorn
 
Kwanza, Bobby alikuwa mshauri wa kaka yake and he proved compitency. Pili, Hawakuwa ofisi moja kama walivyo akina Malecela pale NY.

Mkuu rais Kennedy, alichaguliwa na wananchi na yeye binafsi akamchagua Bobby, mdogo wake kuwa AG wake, yaani mshauri wake wa sheria pamoja na shughuli zake zingine, sasa wewe unasema hawakuwa ofisi moja, kwa hiyo hakukuwa na conflict yako of interest,

Pili unaongelea Compitency, wakati mtoto wa Malecela aliyeko huko NY ni proven mwanasheria liyekwisha zifanyia law firm mbali mbali na NGOs bongo, kabla ya kuingia huko foreign, na kwa wale wanaoijua vizuri foreign, mnajua kuwa hata siku moja hawawezi kupeleka kilaza UN, besides toka aende huko mkuu ningekuelewa kama ungesema kuwa ameharibu kazi, hilo hatujasikia hata siku moja, kama ni mke wa baharia, huyo alikuwa Brussels tena ubalozi wetu kule, na ni mtoto wa makamu na muasisi wa Chadema, sasa can you imagine enzi zile kuajiriwa na serikali ukiwa mtoto wa makamu wa Chadema? Wakati Nyaki alifukuzwa ubalozi kwa sababu tu ya kumkaribisha Mtei mwenyekiti wa Chadema, meaning kwamba huyu dada ni qualified, baada ya kusoma diploma ya lugha mbali mbali kule Belgium, sasa hiii ni kabla hajaolewa amefanya kazi pale for 5 years, na baadaye kuhamia NY akafanya kazi for 8 years,

Sasa mkuu hebu weka mambo hapa wazi what this has to do na Mama Mongella anyeshutumiwa kwa wizi na undugunization?
 
1.
Hizi bado ni allegations bwana mkubwa ni makosa makubwa sana kwa mzee mzima kama wewe kukaa mbele ya keyboard yako na kuropoka maneneo kama haya. Read out loud to yourself what you just wrote and hear how you sound. This kind of conclusion suggests that you are so blinded by prejudice that you can't see things straight.

Zingekuwa bado ni allegations basi msaidizi wake ambaye ni mke wa mtoto wake asingerudi nyumbani mkuu kukimbia uchunguzi , ambao umeshakamilika na waliomchunguza SADC na KGM, wasingeshauri Mama aondolewe na hata kum-brief rais wetu kule Adis, Katibu wa bunge la Tanzania, amesema kuwa Mama Mongella anatakiwa kulipwa na bunge la Tanzania, sasa ilikuwaje akaenda kudai alipwe kule Adis kwa kazi hiyo hiyo aliyokwisha lipwa na bunge letu? Na kasema kuwa tayari ameshaletewa repoti ya huo uchunguzi, mama anaombwa kusema hataki kwa nini na yeye siku zote ni bingwa wa kusema Beijing?

Sasa exactly what is your point eti hizi bado ni allegations? Wakati mashirika mawili independent yaliyomchunguza yamesha shauri aondolewe, na msaidizi ameshakimbia tayari, unasema ni allegations? Hivi ni kweli ninasoma sawa sawa or what eti hizi ni allegations? Allegations wakati tayari head of state wetu ameshafahamishwa? Mkuu unajua maana ya diplomatic relations? huwezi mwambia rais wa nchi au head of state kuwa kuna allegations kuhusu mwanachi wake, unamfahamisha kuwa kuna kesi, unamuonyesha uchunguzi na hukumu, kama rais wetu alivyofahamishwa, hakuna majungu wala blindness hapo ni mama kuondoka tu kama mke wa mtoto wake alivyotangulia kwa kusoma alama za nyakati mapema!

2.
Facts gani tena unahitaji wewe? Do you really need facts or you just want an interminable 20 pages debate wakati umeisha hukumu wenzako?

Mama Mongella, amehukumiwa na SADC na KGM ya Kenya mkuu, na mimi kama mbongo ni wajibu wangu kusema maoni yangu kama Mtanzania niliyeabika kwa vitendo viovu alivyovifanya Mama, it is a shame na haiteteeki kabisa mkuu, kwa kifupi ni aibu n I have nothing to do with it just deal with facts kuwa mama ni mwizi na mndugunization, waliosema ni AU, kwa kushauriwa na SADc na KGM, na wamemfahamisha rais wetu, sio mimi mkuu ni just facts hizo! Kama ni ndugu yako I do not care mkuu hapa hatuangalii uso wa kiongozi hapa ni mawe tu!

3. [
B]You even went as far as using your little scare tactics of PhD. [/B]

Malecela, ana PHD, watoto wake wawili wanazo PHDs, Watoto wake wawili wana Masters, na mmoja ana BA, hizi ni facts mkuu sio opinion zangu, sasa exactly what is your problem kwamba hao wazungu waliwapa tu hizo PHDs kwa sababu ni Malecela? is that so? Scare tactits kama watoto na baba wasingekluwa nazo hizo PHDs, lakini wanazo sasa inakuwaje scare tactics? Scare tactics ni pale unaposema una picha za rais akiwa uchi wakati huna mkuu!

4.
Pamoja na vimatusi vyako vya rejareja vya fitina na majungu wakati wewe ndiye unaongoza kwa fitina na majungu.

Sijawahi kuweka matusi ya reja reja huwa ninaweka vitu straight ninachosema na siku zote ninaeleweka hapa, off course ninaongoza kwa fitina na majungu kwa sababu siku zote ninaweka nyeti za mfisadi ambazo wewe huwezi kuzipata, kwa hiyo ni lazima ziwe majungu kwako na fitina, kama hukulalamika Rosemary Nyerere kuwa mbunge na kaka yake Makongoro kuwa mbunge at the same time kuwa inakuletea conflict of interest, lakini ukaona kwenye Malecela tu ndio problem kwako basi hiyo ndio fitina yenyewe na majungu mkuu!

5.
Ni kinyume na maadili kuajiri wanafamilia moja kwenye kituo kimoja cha kazi. You don't have to be an Einstein to know this.

Tanzania hatujawahi kuwa na haya maadili, Mwalimu alikuwa mwenyekiti wa TANU mdogo wake Joseph Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Wa TANU, yaani TANU Youth League, Bomani akawa waziri mdogo wake Mark akawa AG, Malecela akawa waziri Kaka yake Lusinde akawa Waziri pia, Mwapachu akawa waziri mdogo wake Juma Mwapachu akawa Balozi na sasa ni katibu wa EAC, leo Radhia ni Director Foreign, dada yake ni katibu mkuu wa wizara, Mama Migiro alikuwa waziri wa nje, mdogo wake Radhia akawa HOC London, je ni yeye Mama Migiro aliyempa huo u-HOC? Mkuu Tanzania hatuna hiyo sheria ya maadili ya ndugu au wananchi wa familia moja kufanya kazi pamoja, unless sasa ipo kwa sababu tu ya Malecela, taht is a joke tena a big one mkuu!

6.
Balozi Maharage ana ndugu yake pale Foreign alikuwa anatumia jina la Maharage. Maharage mdogo alipoajiriwa Foreign, yeye albadili jina kuepuka masuala ya maadili.

Tanzania hauna haya maadili mkuu, huyo Maharage kama ni kwei aliamua kubadili jina mwenyewe tu kwa kutokujiamini, maana basi Karumes wangekua wa kwanza kubadili majina mkuu, wakifuatiwa na Mtengetis, halafu Mwapachus, Cheyos, sasa hawa mbona hawajabadili majina ili wa-fit hayo maadili yako mkuuu na kina Maharage?

7.
Kwani huyo Malecela wa India mpaka aje UN? Si angepelekwa kituo kingine?

Mkuu haya maswali yanahitaji kupelekwa foreign, ambako kuna pannel inayoamua nani aajiriwe na nani aende wapi, we do not do that hapa JF, na mimi binafsi I have nothing to do with it, ninachojua ni kuwa msichana ni mwanasheria tena wa kuaminika sana mkuu, maana huwezi pewa kile kituo cha UN bila kichwa haijawahi kutokea, tena ukafanye kazi na Dr. Mahiga, duh!

8.
Wakati wowote familia ya Malecela inapotajwa unakimbilia fitina na majungu. Vilevile, kuwajua kwako ndugu wengi walioajiriwa kitengo kimoja ambayo ni kinyume cha maadali does not justfy the fact that watu wamekiuka maadili na tuendelee kukiuka maadili.

Ninasema kuwa ni majungu kwa sababu mopja muhimu, nayo ni kwamba sijawahi kusikia Malecela akituhumiwa na shutuma mpya, zaidi ya zile zilizoanzishwa na Mwalimu, in 85, na 95, so far sijawahi kusikia anything new, halafu ninasema ni majungu na fitina kwa sababu siku zote huwa hakuna ukweli, mkuu tafuta hotuba ya Kikwete siku Malecela alipostaafu rasmi, jinsi alivyomtukana Mkapa mbele ya uso wake na Mwalimu, na alisema haya haya ninayoyasema kuwa ni "......majungu na fitina, ndiyo yamesababisha tumchukie Malecela tena hasa sisi viongozi wa juu wa CCM, wananchi hawana kosa ila sisi viongozi wa juu kuanzia wa zamani mpaka wa sasa, na hasa waliostaafu....." Mkuu haya maneno yalisemwa na Rais wa Jamhuri yetu, sasa je na yeye ni kama mimi ambaye kazi yangu kukimbilia kusema majungu na fitina, hebu jaribu kujitokeza na something new against Malecela, just for a change, lakini kusema ninatumia scare tactics kwa kusema ukweli kwamba Malecela na watoto wake wanazo PHDs, Masters, na BA, wakati viongozi wengi wanaomchukia hawana na watoto wao hawana, basi ninakubali kuwa unasema ukweli mkuu!

Ndio maana hiyo hatuba hujawahi kuiona hata siku moja kwenye media zetu, maana ni too much kwa watu ambao wamekuwa wakimtukana mzee bila sababu just necause Mwalimu alisema, lakini ninaifanyia kazi itaanza kupatikana siku za karibuni sana mkuu, mambo siku hizi ni hadharani, si unajua ingekuwa zamaani haya ya Mama Mongella yangezimwa tusingeyasikia mkuu, ila ni aibu kwa taifa letu, Malecela amefanya kazi UN akiwa na in his 20s, akahamia OAU yaanai AU ya sasa akiwa in his 20s na 30s, akahamia EAC akliwa in his 30s, akawa foreign minister wetu wa kwanza akiwa in his 40s, mbona hatukuwahi kusikia kuwa ni mwizi, au mndugunization? sasa WHY Mama Mongelal, tena now?

9.
Hii ni sawasawa na umekamatwa kwa wizi halafu unasema aaah, hata John ni mwizi na ninawajua wezi wengi tu. This is very stupid argument Mr. FM.

Mkuu kwenye ukweli uongo hujitenga, nafikiri nimesema ya kutosha kuhusiana ukweli wa ishu, sasa labda niwaachie wananchi waamue! Ila stupid argument huwa sio tabia yangu, na kama ingekuwa nisingekuwa FMES. Na sina apologies kabisa kama Mama Mongella anakuhusu mkuu.

Ahsante Mkuu!
 
tz_devil + Kigeugeu

Jambo la msingi hapa ni sheria zipi zina-govern wapi UN, AU na mashirika mengi ya kimataifa yameweka wazi sheria zao kuhusu ndugu kufanaya kazi sehemu/shirika moja, very clear hairuhusiwi.

Undugunization ni kitu kibaya sana, hakuna anayekataa na hata Mkandara amejaribu kuonyesha kuwa ni wakati muafaka sasa serikali ikaliweka wazi hili jambo la ndugu kufanya kazi sehemu moja.

Swali tunalojiuliza hapa ni je wapi au ktk kipengele kipi serikali imesema ndugu wasiajiriwe sehemu moja, hebu tuanzie hapo kwanza kwenye policy ndio tuanze kunyoosha vidole.

Kama ni allegation kwa Mongella, kama ni kweli kuwa kaajiri mkwe wake basi ni AIBU kwa Taifa period, kwani sisi watanzania ndio tunatakiwa kulijua hilo kuwa kaajiri mkwe wake, kama ni kweli na bado tukakaa kimya. AU wameleta allegations. JK akawa bubu, beef iko wapi, je ni kweli kaajiri mkwe wake pengine hili liwe ndio swali la msingi.

Kama sio kweli then Mongella is clean according to rules za AU period.
 
Hawa akina Malecela pamoja na elimu waliyo nayo wana asili ya upendeleo na kukosa maadili ktk kazi tangu Mzee JS, mtoto utafiti, Watoto wa UN! Hadi leo hakuna anayejua kwa nini Mwalimu alikataa Jonh asiwepo katika Mchakato wa CCM 1995.

Mkuu Kigeu geu,

Heshima mbele kaka, huu uwanja ni mkubwa sana na mpana, labda uweke wazi hizo tabia zao za upendeleo walizonazo, maana kama nilivyosema Malecela, amefanya kazi UN, OAU(AU), EAC, Tanzania, CCM, ni wapi mkuu kuliwahi kuwa na malalamiko ya yeye na upendeleo? Weka wazi mkuu hapa ndio maana tuko hapa JF kumkoma nyani mchana kweupee!,

Lakini ninashukuru kwamba unakubali kuwa kina Malecela, kitabu kinapanda kuanzia baba mpaka watoto, as opposed na maadui zake, ambao watoto wao tunawasikia tu hapa bongo shule hawana wala kazi, lakini wananunua majumba na magari ya kifahari, je mkuu unajua wanapata wapi hizo hela?

Lakini nitashukuru ukituwekea upendeleo na Malecela?
 
Quote:-
"mama wa watu bila kufikiria kayapeleka hayo ya butua butua huko AU, yaani alishazoea kutoa maamuzi ya ajabu ajabu bila kuulizwa au kuwajibishwa."

Heshima mbele mkuu Choveki,

Very thoughtful na right to the point! Halafu guess what sasa wabongo hatupati tena hizi nafasi, maana Mama Tibaijuka naye bado ana sooo zito sana kuhusiana na undugunization kule UN Nairobi, huenda ni kweli CCM tumezoea hii tabia sasa tukienda nje inakuwa aibu kwa taifa zima, hapa pamoja na u-CCM wangu lakini siwezi kupingana na FACTS, tumezoea ujinga kwenye uongozi sasa tukipelekwa nje ndio hivi tunaonekana mara moja, yaani kweli mimi leo nkamuajiri mke wa mtoto wangu kuwa msaidizi wangu kwenye Firm ya kimataifa?

I mean where is the common sense jamani Tanzania? Yaaani hata mtoto mdogo huwezi kumuelewesha akaelewa this one, kule international kuna watu kibao wameenda shule, sasa wewe unajizolea tu uozo wa uongozi bongo na klwenda kuji-expose huko kwa watu jamani aibuu hiii!
 
Note to ES

ukitaka kumquote mtu wewe bonyeza QUOTE kisha then itakuwa rahisi zaidi kwako kuendelea na majibu

Sitaki kuingilia huu mjadala kwani unaendelea vizuri zaidi tai yano na TZ devil

 
Mkuu GT,

Heshimambele nimekusikia, tatizo langu ni muda ndio maana huwa siwezi kufuatilia hayo ya quotes, lakini ninaaamini huwa ninaeleweka, lakini nimekusikia mkuu, hili tunasoma darasa hakuna noma hapa!
 
nimefuatilia mjadara huu kwa makini ingawa kuna sehemu kadhaa nilizoachwa nyuma na mjadala umekuwa unzaa matawi mbalimbali. Hata hivyo nimeona nichangie kidoho kulingana na uelewa wangu kuhusu Malecela:

(a) Ni kweli watoto wake wana elimu ya juu; hata hivyo tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa sana zaidi za wengine kuwafanya wawe na qualification zaidi kwa kazi za aina fulani kuliko wenzao. Influence ya baba yao imetumika katika kuwafanya wapate nafasi hizo ukiachia wawili tu: Mwele Ntulli (ambaye ana Ph.D. kutoka University of London na anafanya kazi inayoendana kabisa na utaalamu wake), na Secelela (ambaye ana M.D. kutoka University of Dar es Salaam na anafanya kazi kulingana na utaalamu wake huo.)


(b) Uhusiano wa Malecela na Nyerere haukuwa mbaya sana kama watu wanavyodhani; in fact Nyerere alikuwa akimuamini sana Malecela kuliko watu wengi ambao hawakukaa kwenye kabineti yake kwa muda mrefu. Nyerere alipokuwa akimchukia mtu, alikuwa anamwondoa kabisa kwenye system yake na asingempa nafasi yoyote ile. Hata hivyo mtagundua kuwa Mzee Malecela aliitumikia serikali ya Nyerere hadi aliposhindwa uchaguzi wa Bunge mwaka 1985 wakati Nyerere anaondoka madarakani. Pamoja na kuaminiana kiuwezo vile kulikuwa na dosari fulani fulani hasa kwa vile kuna wakati Mzee Malecela alikuwa anafanya maamuzi bila kumwarifu mkuu wake wa kazi, jambo ambalo halikubaliki sehemu nyingi za kazi. Nyerere kumzuia Malecela asigombee mwaka 1995 kulitokana zaidi na hangover ya utawala wa Mwinyi, ambapo Malecela ndiye alikuwa mshauri wake mkuu, kuliko uwezo wa Malecela mwenyewe.
 
Quote:-

Ni kweli watoto wake wana elimu ya juu; hata hivyo tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa sana zaidi za wengine kuwafanya wawe na qualification zaidi kwa kazi za aina fulani kuliko wenzao.

Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele, naomba kuuliza exactly unajaribu kusema nini hapa, maana hii topic ni ya Mama Mongella, Malecela amechomekezwa ili kujaribu kuiua na kuiharibu hii topic,

However, watoto wa Malecela, na Malecela mwenyewe wamesoma shule hiyo ni fact, wameomba kazi wakapitia kanuni za kuajiriwa na kuajiriwa, sasa unaposema "Tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa zaidi za wengine" now tell me ni mtoto yupi wa Mkapa ana PHD? au wa Mwalimu mwenye PHD? Sasa kilichokuzwa hapa ni kipi kwamba hawana hizo PHDs au? Ni mwanachi yupi unayemjua aliyewahi kuwania nafasi ya kazi na watoto wa Malecela, akanyimwa huku akiwa na qualifications kama wao? I mean mbona mkuu huwa ninakuaminia kwa kichwa na wewe umeingia kwenye huu mkumbo wa Malecela haters, lakini kwa maneno ya kishule? duh! Mkuu shule haiwezi kuwa subtituted na majungu na fitina, aliyesoma amesoma asiyesoma hakusoma!

Quote:-

dosari fulani fulani hasa kwa vile kuna wakati Mzee Malecela alikuwa anafanya maamuzi bila kumwarifu mkuu wake wa kazi, jambo ambalo halikubaliki sehemu nyingi za kazi. Nyerere kumzuia Malecela asigombee mwaka 1995 kulitokana zaidi na hangover ya utawala wa Mwinyi, ambapo Malecela ndiye alikuwa mshauri wake mkuu, kuliko uwezo wa Malecela mwenyewe.
Today 01:22 AM


Mkuu Kichuguu, kwa kweli kuna aliyeiba code yako, kweli una-justify kitendo cha Mwalimu rais mstaafu kuingilia maamuzi ya taifa na kutuchagulia mkapa, ambaye hakuwahi kushinda uchaguzi wa ndani wa CCM hata mara moja kati ya karibu mara kumi alizogombea ujumbe wa NEC na CC? sasa kama nia na madhumuni yako ni kuamua maamuzi yote peke yako sasa kwa nini unaweka mawaziri?
Kwa hiyo mkuu wewe ukipewa uwaziri leo utakuwa yes man tu ili umridhishe mkuu wako wa kazi badala ya kuwasaidia wananchi?

Sasa what do you have to say kuhusu Mtei, aliyemkatalia ujinga Mwalimu, na kuanzisha Chadema ambayo siku zote unaiunga mkono mkuu? Mkuu nimesikitishwa sana na huu ujumbe wako kwa vijana wetu, yaaani sasa naomba nikuulize Mwalimu, alipotufikisha kiuchumi alikuwa akishauriwa na nani? Maana kwa maneno yako ambayo ni sawa na ya Mwalimu, ni kwamba Mwinyi was clean isipokuwa Malecela anayemshauri, na hasa alipomsahuri kuhusu Muungano maana wabongo matatizo yetu yote kimaisha na kisiasa yalikuwa yanasababishwa na Muungano is that so mkuu?

Mwalimu mbona hakuwahi kutuambia aliyekuwa akimshauri yeye vibaya mpaka kututia umasikini wa karibu miaka 50 nyuma? Ni nani aliyekuwa akimshauri? Yaaani hata wewe mkuu wa kichwa Kichuguu unaweza kujiunga na none argument, ili kumshambulia Malecela tu?

Kaazi kweli kweli!
 
Ni kweli watoto wake wana elimu ya juu; hata hivyo tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa sana zaidi za wengine kuwafanya wawe na qualification zaidi kwa kazi za aina fulani kuliko wenzao. Influence ya baba yao imetumika katika kuwafanya wapate nafasi hizo ukiachia wawili tu: Mwele Ntulli (ambaye ana Ph.D. kutoka University of London na anafanya kazi inayoendana kabisa na utaalamu wake), na Secelela (ambaye ana M.D. kutoka University of Dar es Salaam na anafanya kazi kulingana na utaalamu wake huo

Kichuguu,

Naafikiana na wewe na nashkuru kwa ufafanuzi!
Huyo Mwele Ntuli wakati akimaliza Bsc Mlimani 1980s- na ni kweli alifaulu kawaida kama wanafunzi wengine. Nakumbuka wakati huo Tanzania ilikuwa ndo inaanzisha kitengo cha Utafiti- Wizara ya Afya. Wakati huo qualification ya kupata kazi kule ilikuwa ni GPA kubwa na walioajiriwa wakati huo waliajiriwa kwa GPA kubwa. Huyu mtoto mama yake (marehemu) alimleta kumwombea kazi kwa Mkurugenzi kwa vile alikuwa na GPA ndogo na alikuwa msichana. Mimi nadhani ni kutokana na influence ya Baba yake yule Mkurungenzi alimwajiri- hata kama baadae alijafanya vizuri katika ngazi Masters na PhD. London!

Hao wa UN ni wazi kama ilivyo kwa watoto wengine wa vigogo ni influence ya JS- pamoja na kuwa na uwezo wao wa kawaida!

Halafu ES anavyokuza elimu ya akina ‘Malecelas' ndo anaharibu kwani ni elimu ya kawaida- kuna waliosoma pamoja na hao watoto- wana uwezo tu wa kawaida na exporure kutokana na nafasi ya mzee wao.
 
Back
Top Bottom