1.
(a) Watoto wa Malecela wameelimika kweli, lakini ni makosa kusema kuwa kila sehemu waliyopo ni kwa sababu ya elimu yao nzuri bila kuangalia influence ya baba yao.
Mkuu Kichuguu,ndio hasa maana ya kuwepo hapa JF ni kuweka mambo hadharani, tunasema hivi ya Mama Mongella yamewekwa hadharani, sasa kama una dataz jinsi Malecela influence ilivyotumika kuwaajiri watoto wake, mmoja mwenye PHD wizara ya Afya, Mwanasheria wa serikali wizara ya sheria, na mwanasheria wizara ya nje, na mkwe wake aliyeajiriwa ubalozi wetu Brussles akiwa mtoto wa makamu wa mwenyekiti wa Chadema, kwa nini usiuweke hapa? Tunasema hapo hapakuwa na influence bali ni uwezo kishule na kikazi maana so far hatujasikia malalamiko kwenye sehemu zao za kazi kama yaliyomkuta Mama Mongella, unless na wewe unaunga mkono maneno ya watoto wa viongozi wasifanye kazi maana sehemu wanazozifanyia kazi hawa wakuu tunazijua na wananchi wa huko wanafahamika na hatujasikia maneno sasa kwa nini usiweke wazi jinsi influence ya baba yao ilivyotumika kama ya Mongella kuajiri mke wa mtoto wake mbayo ndio hasa point ya msingi hapa mkuu? Influence ya Malecela ilitumika wapi kwenye seshsmu ya uajiri mkuu?
2.
(b)
Kuna wanoadhani kuwa Nyerere alikuwa anamchukia sana Malecela. Mimi nawaambia kuwa hapana, uhusiano wa Nyerere na Malecela haukuwa mbaya siku zote ambapo Nyerere alipokuwa madarakani ama sivyo angemtupilia mbali kabisa.
Kama maneno yako ni kweli basi uhusiano wao ulianza kuharibika mwaka 1984 mwishoni, Mwalimu alipokuwa akikaribia kutoka, hilo tumeshalisema wazi kule kwenye Malecela na Legacy yake mkuu hebu kachungulie tena!
3.
Malecela amekuwa kwenye serikali ya Nyerere hadi mwaka 1985 wakati Nyerere anondoka madarakani. Mwaka huo Malecela alishindwa kiti chake cha ubunge
kwa hiyo Mwinyi alipoingia madarakani hakumpa position yoyote ya kabineti bali alimpa ukuu wa mkoa nadhani Iringa. Kipindi chote hicho ikiwa ni pamoja na tukio lile la 1983 la "...they can go to hell," Nyerere hakuwa na tatizo lolote na Malecela.
Mkuu haya ni yale yale, Mwinyi alipoingia madarakani Malecela, alikuwa kwenye Jumuiya ya Madola mkuu, South Afrika, hakuwepo bongo, na hata baada ya kurudi huko alipewa kazi ya kwenda Canada kufuatilia madeni ya EAC, ni mpaka aliporudi huko ndipo akapewa u-RC Iringa, Balozi London, na baadaye Waziri Mkuu. Kushindwa kwake kiti cha ubunge only baada ya kuwa Mwalimu anaondoka tunaelewa indetails what happened, ningekuomba mkuu ukaitefute ile tread ya Malecela na Legacy, na hili ya tukio la "They can go to hell", vipi mkuu ukituweka sawa aliposemea na alimuambia nani? Maana to this day bado ni mistery?
4.
(c) Inaweza kuwa inakuuma lakini that is exactly what happened.
Mkuu labda inayekuuma ni wewe kuhusiana na Mama Mongella, mimi sijawahi kuwa na noma ila kazi yangu ni kuweka habari sawa ninapofahamu kwa kiongozi yoyote ninayemfahamu, I know Malecela kwanza ninam-admire mkuu kwa kuweza kufikia alipofikia na haters wake wote waliopo nchini kwetu, huo ni mfano mkubwa kwangu na vijana wengi kuwa riziki ya bin-adam hupangwa na Mungu, wewe ni kusimama imara tu huwezi babaishwa na mtu, the man Malecela did what he could, amesomesha watoto kama yeye alivyosoma na sasa wamesimama wenyewe na huku yeye saa hizi akipeta huko majuu baada ya kustaafu, sasa hivi anamwaga ma-speech tu huko majuu, for the last one month, leo kama sikosei atakuwa huko Universty Of Maryland, sasa kwa maisha ya bongo mtu unataka nini zaidi, kwa hiyo nafikiri anayeumizwa na mafanikio ya Malecela, huwa wanajionyehsa kwa maneno yao na sio vigumu kuyaona hayo maneno kwenye hii topic, mimi ninazimia na mzee kwa ujasiri wa kuweza kupambana na maadui na wanafiki, na wafitini nafikiri wake ni mfano mkubwa wa kuigwa!
5.
(d) Umefanya makosa sana kudhani kuwa nilisupport uteuzi wa B. M. Kapa,
Mkuu mimi nilifikiri msomi yoyote kama wewe, kwanza alipaswa kukemeea kitendo cha Mwalimu, kuingilia system yetu ya uchaguzi huku akiwa mstaafu, sasa kama unakuabliana na nacho ndio ninasema kuwa itachukua muda mrefu sana sisi wabongo kuendelea, pia ni madhara ya kitendo hicho cha Mwalimu, ndio na Mkapa akaamua kutuchagulia Muungwana, sasa mtu yoyote mbongo aliyeenda shule kama wewe nilitegemea kuwa anapaswa kukikemea kitendo hicho kiovu na hasa kulingana na yanayojiri sasa kuhusiana na tabia za Makapa alipokuwa kwenye power, yaanai wizi kama wa Mama Mongella, lakini Malecela hatujasikia kuwa ni mwizi, tuliambiwa na Mwalimu, Mkapa ni MR. CLEAN, lakini sasa tunamtaka aende mahakamani maan tumegundua kuwa Mwalimu alituvalisha mkenge! Leo in his absence tuna matatizo na wale aliotumabia kuwa ni wasafi, aliosema wachafu wala hatuna shida nao, Mwalimu was a human mkuu, hakuwa Mungu kama baadhi yenu mnavyoamini na haya maneno yenu, mkuu wangu sasa hivi kuna mikakati mikali inayotayarishwa kuhakikisha Mkapa kipenzi cha Mwalimu siku moja anatinga jela, maana maovu aliyoyafanya akiwa Ikulu hata robo hujayasikia, lakini yanakuja mkuu kuanzia next year!
Mkapa alikuwa kipenzi cha Mwalimu, so was Mama Mongella, tizama hii aibu mkuu kwa taifa letu? Kule kwenye zawadi ya MO tumekataliwa kwa sababu ya wizi wa Mkapa, na sasa huenda hatutapata uongozi international tena kwa wizi wa Mama Mongella, bado kuna wenye ubavu wa kutetea huu ufisadi, na kujaribu kuwalinganisha hawa na Malecela, only in Tanzania
Othwerwise, nimekusikia mkuu mana hii ni kwa mara ya kwanza ninakuona kwenye this kind of ishu!
__________________