Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Dr. Shein the next Tz President?!...God forbid. Whatever good have been said about him, his dullness is an obstacle. Siasa sio lele mama, inahitaji werevu. Hivi huyu jamaa tangu awe VP kuna kitu gani alikisimamia kikaonekana? In fact hata hiyo position aliyo nayo hafai hata kidogo.
 
Quote:-

Ni kweli watoto wake wana elimu ya juu; hata hivyo tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa sana zaidi za wengine kuwafanya wawe na qualification zaidi kwa kazi za aina fulani kuliko wenzao.

Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele, naomba kuuliza exactly unajaribu kusema nini hapa, maana hii topic ni ya Mama Mongella, Malecela amechomekezwa ili kujaribu kuiua na kuiharibu hii topic,

However, watoto wa Malecela, na Malecela mwenyewe wamesoma shule hiyo ni fact, wameomba kazi wakapitia kanuni za kuajiriwa na kuajiriwa, sasa unaposema "Tusikuze sana elimu zao kama vile ni kubwa zaidi za wengine" now tell me ni mtoto yupi wa Mkapa ana PHD? au wa Mwalimu mwenye PHD? Sasa kilichokuzwa hapa ni kipi kwamba hawana hizo PHDs au? Ni mwanachi yupi unayemjua aliyewahi kuwania nafasi ya kazi na watoto wa Malecela, akanyimwa huku akiwa na qualifications kama wao? I mean mbona mkuu huwa ninakuaminia kwa kichwa na wewe umeingia kwenye huu mkumbo wa Malecela haters, lakini kwa maneno ya kishule? duh! Mkuu shule haiwezi kuwa subtituted na majungu na fitina, aliyesoma amesoma asiyesoma hakusoma!

Quote:-

dosari fulani fulani hasa kwa vile kuna wakati Mzee Malecela alikuwa anafanya maamuzi bila kumwarifu mkuu wake wa kazi, jambo ambalo halikubaliki sehemu nyingi za kazi. Nyerere kumzuia Malecela asigombee mwaka 1995 kulitokana zaidi na hangover ya utawala wa Mwinyi, ambapo Malecela ndiye alikuwa mshauri wake mkuu, kuliko uwezo wa Malecela mwenyewe.
Today 01:22 AM


Mkuu Kichuguu, kwa kweli kuna aliyeiba code yako, kweli una-justify kitendo cha Mwalimu rais mstaafu kuingilia maamuzi ya taifa na kutuchagulia mkapa, ambaye hakuwahi kushinda uchaguzi wa ndani wa CCM hata mara moja kati ya karibu mara kumi alizogombea ujumbe wa NEC na CC? sasa kama nia na madhumuni yako ni kuamua maamuzi yote peke yako sasa kwa nini unaweka mawaziri?
Kwa hiyo mkuu wewe ukipewa uwaziri leo utakuwa yes man tu ili umridhishe mkuu wako wa kazi badala ya kuwasaidia wananchi?

Sasa what do you have to say kuhusu Mtei, aliyemkatalia ujinga Mwalimu, na kuanzisha Chadema ambayo siku zote unaiunga mkono mkuu? Mkuu nimesikitishwa sana na huu ujumbe wako kwa vijana wetu, yaaani sasa naomba nikuulize Mwalimu, alipotufikisha kiuchumi alikuwa akishauriwa na nani? Maana kwa maneno yako ambayo ni sawa na ya Mwalimu, ni kwamba Mwinyi was clean isipokuwa Malecela anayemshauri, na hasa alipomsahuri kuhusu Muungano maana wabongo matatizo yetu yote kimaisha na kisiasa yalikuwa yanasababishwa na Muungano is that so mkuu?

Mwalimu mbona hakuwahi kutuambia aliyekuwa akimshauri yeye vibaya mpaka kututia umasikini wa karibu miaka 50 nyuma? Ni nani aliyekuwa akimshauri? Yaaani hata wewe mkuu wa kichwa Kichuguu unaweza kujiunga na none argument, ili kumshambulia Malecela tu?

Kaazi kweli kweli!


ES,

Nilikuwa nafuatitilia kwa makini sana taarifa kuhusu vitendo vya mama Mongella kwa vile niliwahi kusikia kichinini chini kukiwa na malalamiko ya aina hiyo. Hii thread ndiyo ilikuwa ya kwanza kuyatoa hadharani kwangu. Swala la Malecela limekuwa linajirudia rudia kiasi cha kuondoa flow ya thread yenyewe, ndiyo maana nikasema niweka ufahamu wangu kuhusu swala la Malecela na lisitumiwe kama ndiyo topik kubwa hapa.

(a) Watoto wa Malecela wameelimika kweli, lakini ni makosa kusema kuwa kila sehemu waliyopo ni kwa sababu ya elimu yao nzuri bila kuangalia influence ya baba yao. Unaweza usikubaliane na hilo lakini huo ni ukweli. Tofauti iliyopo baina ya watoto wa Malecela na alivyofanya mama Mongela ni kuwa Mongella aliwavuta kwa mkono wake wakati Malecela alikuwa hafanyi hivyo. Kwa hiyo kismingi, pamoja na influnce ya Malecela kutumika, inawezekana hakuna ethics zilizovunjwa wakati mama Mongela amevunja ethics za kazi zake kwa kuvuta ndugu zake.


(b) Kuna wanoadhani kuwa Nyerere alikuwa anamchukia sana Malecela. Mimi nawaambia kuwa hapana, uhusiano wa Nyerere na Malecela haukuwa mbaya siku zote ambapo Nyerere alipokuwa madarakani ama sivyo angemtupilia mbali kabisa. Kuna wakati, nadhani mwaka 1975 au 76 hivi, Malecela alijiamulia swala fulani la kuhusu suluhu ya mgogogoro wa nchi fulani afrika mashariki (nadhani Somalia) bila kumpa taarifa mkubwa wake. Ingawa hatua aliyochukua ilikuwa ni sahihi alikosea kwa kufanya hivyo bila kumpa taarifa mkubwa wake wa kazi. Nyerere alimpa onyo lakini hakumwondoa serikalini kwake. Malecela amekuwa kwenye serikali ya Nyerere hadi mwaka 1985 wakati Nyerere anondoka madarakani. Mwaka huo Malecela alishindwa kiti chake cha ubunge kwa hiyo Mwinyi alipoingia madarakani hakumpa position yoyote ya kabineti bali alimpa ukuu wa mkoa nadhani Iringa. Kipindi chote hicho ikiwa ni pamoja na tukio lile la 1983 la "...they can go to hell," Nyerere hakuwa na tatizo lolote na Malecela.


(c) It is very unfortunate kuwa Nyerere alitofautiana na Malecela wakati wa mchakato wa utezi wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995. Inajulikana kuwa Malecela alikuwa na support kubwa ya Mwinyi ambaye alishakuwa katika terms mbaya kisiasa na Nyerere wakati huo. Kwa hiyo imani yangu kubwa ni kuwa Nyerere alimuunganisha Malecela katika kapu moja na washirika wa Mwinyi na hivyo kumpinga. Inaweza kuwa inakuuma lakini that is exactly what happened.

(d) Umefanya makosa sana kudhani kuwa nilisupport uteuzi wa B. M. Kapa, nilichotoa ni maelezo ya kwa nini Nyerere alipingana na Malecela wala sijasema kuwa hiyo ilikuwa ni hatua nzuri au mbaya. Nadhani unakumbuka kuwa mwaka huo huo Nyerere aliwakataa pia akina J.K.I. Kwete pamoja na mwenzie E. L. O. Wasa lakini leo hii ndio wanaoutuongoza.
 
Nashukuru sana wana JF kwa hii tuhuma mimi naomba mwenye orodha ya majina ya hao ndugu zake aliowaajiri atuwekee hadharani. Kwa kifupi hali hii imelishushia hadhi taifa letu. Hana budi kujiuzulu wadhifa wake kabla hajafukuzwa.
 
Du,
JF kuna mengi! Mazuri na yanayoainisha mabaya ya watu. Hata usome vitabu vingapi- uchumbuzi mwingine kama huu huwezi kupata- sasa swala ni kama je ni yote ya kweli? This is another question!

Pokeeni 5 wachangiaji!
 
Du,
JF kuna mengi! Mazuri na yanayoainisha mabaya ya watu. Hata usome vitabu vingapi- uchumbuzi mwingine kama huu huwezi kupata- sasa swala ni kama je ni yote ya kweli? This is another question!

Pokeeni 5 wachangiaji!

Mzalendooooo.....

kweli kbs maneno unayosema,wewe ukitaka kuona raha JF basi ongelea issue za mzee JM,yaani kuna watu wachafu sana kwa data mpaka unabakia SPEECHLESS.

Mzee Es.....

duh sio utani kaka, MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE APEWE.
 
1.
(a) Watoto wa Malecela wameelimika kweli, lakini ni makosa kusema kuwa kila sehemu waliyopo ni kwa sababu ya elimu yao nzuri bila kuangalia influence ya baba yao.

Mkuu Kichuguu,ndio hasa maana ya kuwepo hapa JF ni kuweka mambo hadharani, tunasema hivi ya Mama Mongella yamewekwa hadharani, sasa kama una dataz jinsi Malecela influence ilivyotumika kuwaajiri watoto wake, mmoja mwenye PHD wizara ya Afya, Mwanasheria wa serikali wizara ya sheria, na mwanasheria wizara ya nje, na mkwe wake aliyeajiriwa ubalozi wetu Brussles akiwa mtoto wa makamu wa mwenyekiti wa Chadema, kwa nini usiuweke hapa? Tunasema hapo hapakuwa na influence bali ni uwezo kishule na kikazi maana so far hatujasikia malalamiko kwenye sehemu zao za kazi kama yaliyomkuta Mama Mongella, unless na wewe unaunga mkono maneno ya watoto wa viongozi wasifanye kazi maana sehemu wanazozifanyia kazi hawa wakuu tunazijua na wananchi wa huko wanafahamika na hatujasikia maneno sasa kwa nini usiweke wazi jinsi influence ya baba yao ilivyotumika kama ya Mongella kuajiri mke wa mtoto wake mbayo ndio hasa point ya msingi hapa mkuu? Influence ya Malecela ilitumika wapi kwenye seshsmu ya uajiri mkuu?

2. (b)
Kuna wanoadhani kuwa Nyerere alikuwa anamchukia sana Malecela. Mimi nawaambia kuwa hapana, uhusiano wa Nyerere na Malecela haukuwa mbaya siku zote ambapo Nyerere alipokuwa madarakani ama sivyo angemtupilia mbali kabisa.


Kama maneno yako ni kweli basi uhusiano wao ulianza kuharibika mwaka 1984 mwishoni, Mwalimu alipokuwa akikaribia kutoka, hilo tumeshalisema wazi kule kwenye Malecela na Legacy yake mkuu hebu kachungulie tena!

3.
Malecela amekuwa kwenye serikali ya Nyerere hadi mwaka 1985 wakati Nyerere anondoka madarakani. Mwaka huo Malecela alishindwa kiti chake cha ubunge
kwa hiyo Mwinyi alipoingia madarakani hakumpa position yoyote ya kabineti bali alimpa ukuu wa mkoa nadhani Iringa. Kipindi chote hicho ikiwa ni pamoja na tukio lile la 1983 la "...they can go to hell," Nyerere hakuwa na tatizo lolote na Malecela.

Mkuu haya ni yale yale, Mwinyi alipoingia madarakani Malecela, alikuwa kwenye Jumuiya ya Madola mkuu, South Afrika, hakuwepo bongo, na hata baada ya kurudi huko alipewa kazi ya kwenda Canada kufuatilia madeni ya EAC, ni mpaka aliporudi huko ndipo akapewa u-RC Iringa, Balozi London, na baadaye Waziri Mkuu. Kushindwa kwake kiti cha ubunge only baada ya kuwa Mwalimu anaondoka tunaelewa indetails what happened, ningekuomba mkuu ukaitefute ile tread ya Malecela na Legacy, na hili ya tukio la "They can go to hell", vipi mkuu ukituweka sawa aliposemea na alimuambia nani? Maana to this day bado ni mistery?

4.
(c) Inaweza kuwa inakuuma lakini that is exactly what happened.

Mkuu labda inayekuuma ni wewe kuhusiana na Mama Mongella, mimi sijawahi kuwa na noma ila kazi yangu ni kuweka habari sawa ninapofahamu kwa kiongozi yoyote ninayemfahamu, I know Malecela kwanza ninam-admire mkuu kwa kuweza kufikia alipofikia na haters wake wote waliopo nchini kwetu, huo ni mfano mkubwa kwangu na vijana wengi kuwa riziki ya bin-adam hupangwa na Mungu, wewe ni kusimama imara tu huwezi babaishwa na mtu, the man Malecela did what he could, amesomesha watoto kama yeye alivyosoma na sasa wamesimama wenyewe na huku yeye saa hizi akipeta huko majuu baada ya kustaafu, sasa hivi anamwaga ma-speech tu huko majuu, for the last one month, leo kama sikosei atakuwa huko Universty Of Maryland, sasa kwa maisha ya bongo mtu unataka nini zaidi, kwa hiyo nafikiri anayeumizwa na mafanikio ya Malecela, huwa wanajionyehsa kwa maneno yao na sio vigumu kuyaona hayo maneno kwenye hii topic, mimi ninazimia na mzee kwa ujasiri wa kuweza kupambana na maadui na wanafiki, na wafitini nafikiri wake ni mfano mkubwa wa kuigwa!


5.
(d) Umefanya makosa sana kudhani kuwa nilisupport uteuzi wa B. M. Kapa,

Mkuu mimi nilifikiri msomi yoyote kama wewe, kwanza alipaswa kukemeea kitendo cha Mwalimu, kuingilia system yetu ya uchaguzi huku akiwa mstaafu, sasa kama unakuabliana na nacho ndio ninasema kuwa itachukua muda mrefu sana sisi wabongo kuendelea, pia ni madhara ya kitendo hicho cha Mwalimu, ndio na Mkapa akaamua kutuchagulia Muungwana, sasa mtu yoyote mbongo aliyeenda shule kama wewe nilitegemea kuwa anapaswa kukikemea kitendo hicho kiovu na hasa kulingana na yanayojiri sasa kuhusiana na tabia za Makapa alipokuwa kwenye power, yaanai wizi kama wa Mama Mongella, lakini Malecela hatujasikia kuwa ni mwizi, tuliambiwa na Mwalimu, Mkapa ni MR. CLEAN, lakini sasa tunamtaka aende mahakamani maan tumegundua kuwa Mwalimu alituvalisha mkenge! Leo in his absence tuna matatizo na wale aliotumabia kuwa ni wasafi, aliosema wachafu wala hatuna shida nao, Mwalimu was a human mkuu, hakuwa Mungu kama baadhi yenu mnavyoamini na haya maneno yenu, mkuu wangu sasa hivi kuna mikakati mikali inayotayarishwa kuhakikisha Mkapa kipenzi cha Mwalimu siku moja anatinga jela, maana maovu aliyoyafanya akiwa Ikulu hata robo hujayasikia, lakini yanakuja mkuu kuanzia next year!

Mkapa alikuwa kipenzi cha Mwalimu, so was Mama Mongella, tizama hii aibu mkuu kwa taifa letu? Kule kwenye zawadi ya MO tumekataliwa kwa sababu ya wizi wa Mkapa, na sasa huenda hatutapata uongozi international tena kwa wizi wa Mama Mongella, bado kuna wenye ubavu wa kutetea huu ufisadi, na kujaribu kuwalinganisha hawa na Malecela, only in Tanzania

Othwerwise, nimekusikia mkuu mana hii ni kwa mara ya kwanza ninakuona kwenye this kind of ishu!
__________________
 
Mimi nadhani ni kutokana na influence ya Baba yake yule Mkurungenzi alimwajiri- hata kama baadae alijafanya vizuri katika ngazi Masters na PhD. London!

Mkuu tunakataa maneno ya kudhani, tunataka facts kama za Mama za Mongella, kuwa ameiba na kuajiri ndugu zake, hizo ni facts sio kudhani! Dr. Mwele ni level nyingine kabisaa yaaani mwanamama anayekwenda majuu kwa siku moja tu kufundisha wazungu darasaani unasema aliombewa kazi? Sasa huoni ni kwa nini bongo hatuwezi kuendelea mtu ambaye ni good kwenda Europe kuwafundisha wa-tish unasema bongo aliombewa kazi? Jamani mengine haya ni aibu hata kuyaweka hapa JF! Mkuu tizama maneno yako hapo juu yanavyojichanganya!
 
Mkuu tunakataa maneno ya kudhani, tunataka facts kama za Mama za Mongella, kuwa ameiba na kuajiri ndugu zake, hizo ni facts sio kudhani! Dr. Mwele ni level nyingine kabisaa yaaani mwanamama anayekwenda majuu kwa siku moja tu kufundisha wazungu darasaani unasema aliombewa kazi? Sasa huoni ni kwa nini bongo hatuwezi kuendelea mtu ambaye ni good kwenda Europe kuwafundisha wa-tish unasema bongo aliombewa kazi? Jamani mengine haya ni aibu hata kuyaweka hapa JF! Mkuu tizama maneno yako hapo juu yanavyojichanganya!


ES kama ulisoma Tanzania naomba usione ajabu kwa hili! Hata ukienda mlimani watu bado wanaajiriwa kwa kigezo cha GPA. Kwa maana nyingine usipokuwa na GPA ya 3.9 na kwenda mbele huchukuliwi, wanasahau kwamba kuna watu wanaondoka na GPA ndogo wakienda mbele wanafanya wonders. Yet hawa wenye GPA kubwa ndo wanakuwa vilaza mpaka kesho kutwa! Hili mifano iko mingi sana. Kwa hiyo hilo la mtoto wa JSM kuombewa kazi na baadaye kuja kuwa very competent ni kitu cha kawaida kwa Tanzania.

Kuhusu watoto wa Samweli, mi naomba nikubaliane na uchambuzi wako kwamba vijana wamesoma, lakini vile vile hoja ya Kichuguu iko makini sana. Huwezi undermine influence ya jina (ingawa hakuna ubaya katika hili maana hajafunja sheria katika TZ yetu). kama ulisoma post yangu jana, niliandikia hili la undugunization haliwezi kuisha hata Kristo akirudi, cha muhimu tupigane wanaoingia wawe qualified na competent. Kama mpaka juzi Koffi Anani kidogo apoteze kazi yake kwa sababu ya mtoto wake kupewa tenda UN, we easily know kwamba hili bado ni tatizo kubwa saa sehemu mbali mbali duniani, sasa piga picha ya Tanzania how likely are we to enforce such rules za kuwazuia watoto wa wakubwa kuajiriwa sehemu kama hizo za wazee wao.

Mongella amekuwa accused na recommendations zimetoka kwamba aondolewe kazini. NADHANI HAPO HAKUNA UBAYA, LET HER GO Accountability demands consequences and she should be prepared to accept them.
 
Hivi kati yenu humu hakuna mwenye supporting data za kumconfront nazo huyu ES maana naona anawabully ile kisawa sawa

Sikubaliani naye kwa mengi lakini anaonekana ni consistent sana na hizo rebuttal zake

JF kiboko
 
Hivi kati yenu humu hakuna mwenye supporting data za kumconfront nazo huyu ES maana naona anawabully ile kisawa sawa

Sikubaliani naye kwa mengi lakini anaonekana ni consistent sana na hizo rebuttal zake

JF kiboko



Game umenifurahisha sana na hii post yako!! FMES anajulikana..... kawaida linapokuja swala kuhusu JSM...yanakuwa mengine!! Kweli JF ni encyclopidia ya wengi humu!

Heri ya Xmass na mwaka mpya mkuu!
 
Dr. Shein the next Tz President?!...God forbid. Whatever good have been said about him, his dullness is an obstacle. Siasa sio lele mama, inahitaji werevu. Hivi huyu jamaa tangu awe VP kuna kitu gani alikisimamia kikaonekana? In fact hata hiyo position aliyo nayo hafai hata kidogo.


Sasa wewe unataka kutuambia huyo JK ana kipi ambacho Shein hana?
 
Hivi kati yenu humu hakuna mwenye supporting data za kumconfront nazo huyu ES maana naona anawabully ile kisawa sawa

Sikubaliani naye kwa mengi lakini anaonekana ni consistent sana na hizo rebuttal zake

JF kiboko

Unajua mtu akiwa ana facts na wewe huna lazima akumalize. Sasa wengi hapa hawana facts ambazo ES anazo na ndio maana atawa-bully sana. Lakini pia nataka tu niseme kuwa viwango vya elimu walivyo navyo watoto wa mzee malecela ni vya kawaida kwa standards ya kazi wanazofanya na mimi nawapongeza sana- Namjua yule wa NIMR na nimeshasoma papers zake kadhaa -hakuna ubishi kwamba yule dada ni brilliant. In fact ame-publish articles zake katika journals zenye very high repute and impact factor, sasa haya mambo ya GPA ni kasumba ya TZ.

WaTZ tunatabia ya kuangalia qualifications zaidi kuliko ulichokifanya kutokana na hizo qualifications. Ndio maana tunang'ang'ania sana kuitana kwa vyeo: Prof, Dr, Mheshimiwa. Lakini ukimuuliza mtu umefanya nini na haya ma-titles anakuwa mum. Acheni nongwa, wale watoto wa mzee wanakula kwa jasho na akili zao walizozifanyia kazi, yaani they worked hard to get what they are getting. Wasihukumiwe kwa sababu baba yao aliwahi kuwa kiongozi, wahukumiwe kwa kazi wanazozifanya.

Sasa inawezekana mzee malecela directly au indirectly ali-influence watoto wake kupata kazi. Lakini hili haliwezi kuwa kosa la watoto au la malecela mwenyewe especially kama hakuna sheria iliyovunjwa. Hata ukienda kwenye restaurant na Riziwani kwa mfano, the moment wahudumu wanajua huyu ni mtoto wa Rais mtaanza kupata different treatment,sasa hapa utamlaumu vipi JK au Riziwani mwenyewe? Hii ipo hivyo so naturally popote. Tofauti ya kesi ya Mongela ni kwamba yeye kalazimisha ndugu zake kuajiriwa kinyume cha taratibu za ajira za AU achilia mbali kama wana sifa au hawana. Mbaya zaidi yeye ameenda kuiba mahela ya wanachama AU. Huyu hateteiki, yaani lazima ashughulikiwa sana tu.
 
Hivi kati yenu humu hakuna mwenye supporting data za kumconfront nazo huyu ES maana naona anawabully ile kisawa sawa

Sikubaliani naye kwa mengi lakini anaonekana ni consistent sana na hizo rebuttal zake

JF kiboko

Mkuu DrWho,

Ukiwa na the dataz na unapambana kwenye hoja na watu wenye hearsay, jua ushindi ni wa uhakika kwako. Hicho ndicho kinatumiwa na FMES. Kwenye hili la mzee Malecela yeye ana data zilizopikwa zikaiva, wengine wetu tunatumia data za vijueni, bado mbichi. Zikiguswa tu zinaonekana hazijaiva na kutupwa pembeni.

Inabidi ifike mahali tukubali kwenye haya masuala ya mzee Malecela hakuna jipya lililobaki kujulikana. Kilichobaki you can either love him or loathe him.
 
Mkuu tunakataa maneno ya kudhani, tunataka facts kama za Mama za Mongella, kuwa ameiba na kuajiri ndugu zake, hizo ni facts sio kudhani! Dr. Mwele ni level nyingine kabisaa yaaani mwanamama anayekwenda majuu kwa siku moja tu kufundisha wazungu darasaani unasema aliombewa kazi? Sasa huoni ni kwa nini bongo hatuwezi kuendelea mtu ambaye ni good kwenda Europe kuwafundisha wa-tish unasema bongo aliombewa kazi? Jamani mengine haya ni aibu hata kuyaweka hapa JF! Mkuu tizama maneno yako hapo juu yanavyojichanganya!

ES,
Tafadhali tujadiliane tu kwa heshima- tu watu wazima swala mtu anajichanganya you're going too far unnecessarily!

Watanzania wanaoenda US kuongea ktk mihadhadhara ni wengi tu- wanasiasa na hata Malecela na watoto wake, wanafunzi n.k! It is ridiculous kusema JSM na watoto wa JSM ni wasomi na wana nafasi kuliko Watanzania wengi- ndo maana kila leo wako US!

what is so special na hao watu wamefanya nini huwa na wanakulipa wewe unapowatetea kwa kupindisha ukweli siku zote? Je A re they any Nobel Price Laureates dunia isiwafahamu?

Es one key problem you have consistently misrepresented JSM na sasa watoto wake- kila Mtanzania akisona your reaction over elimu, maisha ya siasa ya JSM inaonekana una bias- which is not necessary intentional! May be mnahusiana!

Are you a spokesperson kwa hawa Watanzania? Hata kama ni hivyo you mis represent them- we need a fair presenation of reality! Kama among one of 'Malecelas' JSM au mtoto wake akija hapa JF na kusema if they are the most educated na wana hali nzuri Tanzanians na watoto wengine wa viongozi wa Tanzania kama ulivyosema ni wavuta bangi tuu -hawana la maana na sii lolote and so their parents have failed in parenting sisi tungewasikiliza!

In a nutshell you're misrepresenting JSM family knowingly or unknowingly! Au kama wewe ni mtoto au ndugu wa mzee JSM hapo US tujue tu- ila tambua you are representing negatively familia ya mzee wetu JSM!

Heshima mbele Mkuu!
 
hoja ni ubadhilifu uliofanywa na mama mongella na si mzee malechela na familia yake. nadhani ni vyema tukiendelea
na suala la mama mongella.

pamoja na kwamba katika fomu za kuomba kazi un inabidi utaje kama unaye ndugu wa karibu hayo si ajabu sana kukuta katika shirika la umoja wa mataifa mtu na mkewe wanafanya shirika moja (labda kama mtu na mkewe haihesabiwi ni ndugu). suala hapa ni mmeingiaje katika shirika hilo. mfano mtu kakutana na mwenziwe hapo katika shirika wakaoana hilo halina nongwa watu hao wanaendelea kuwepo. aidha inawezekana mtu na mkewe au nduguye wakaomba kazi katika mashirika mbali na wakapitia mcheketo unaotakiwa na wakapata kazi sidhani kama hilo ni tatizo. tatizo linakuja pale mhusika anapokuwa kwenye nafasi anapoamua kumuajiri nduguye (nadhani hili ndilo linalomhusu mama mongella).

nashangaa inapokuwa hoja pale ambapo afisa mdogo (ki madaraka/cheo)wa ubalozi anapofanya kazi na nduguye ambaye ni local staff. labda idaiwe huyo local staff kaajiliwa na huyo afisa wa ubalozini.
 
Hii thread imenifunza mambo mengi, tuendelee, nasoma tu!!!

Yaani nimepata data na nikajiona kama as if naishi sea view au maeneo ya osterbay, heee kushituka kumbe niko opposite na pub hapa Sinza!

Mama ametuabisha sana, ametuvua nguo, tunaaminika kwa uongozi shupavu sasa du, tumebakia na Migiro na Tibaijuka... wakituangusha hao tumeliwa!!!
 
Kumbe lisemwalo lipo,
Zamani wakati wa vugu vugu la kumtafuta mgombea ukuu wa kaya, nilikutana na mzee mmoja wa Kikelewe.., nami nikawa namchombeza kwamba huyu mama Angefaa kuwa mkuu wetu wa kwanza mwanamke, Yule mzee alingaka sana!! akadai huyu mama hafai kabisa, nika muuliza kwanini?? akatoa maelezo meeengi ya ubaya wake, lakini kwa ujumla wake mie nilichukulia kwamba ni wivu.. na sikuwa nime mkubalia hoja yake japo nilinyamaza ili mjadala usiwe mrefu!, Sasa ndo nime elewa kumbe yule mzee kuna kitu alicho kuwa anakijua na kukiona ndani ya mama huyu!

Kwa kweli katuangusha sana!
 
Hivi mtu wa Kigurunyemb, au kule Nkasi, au Mabokweni, au Ndali anaguswa vipi na mama huyo kupata nafasi ya kula na kutafuna? Tumepiga kelele ya upotevu wa mamilini benki kuu na mambo mengine je wanakijiji wenzangu wanaweza kushawishiwa vipi kuona kuwa maisha yao duni yanahusiana moja kwa moja na utawala ulio madarakani? Sasa hivi tuhuma hizi kwa wananchi wengi ni picha ya samaki tu hayawahusu.

Wengine wanaweza kufikiri hivyo hivyo kuwa kama na mimi ningepata nafasi ya kula kama mama Mongella na mimi ningetafuna vile vile. Baadhi yetu hatuoni ubaya wa matumizi mabaya ya ofisi ndio maana hakuna mwana CCM mmoja aliyejitokeza hadharani kulaani kitendo cha Mkapa kutumia ofisi yake vibaya. Sasa zikipigwa hizi kelele halafu JK akatokea na kusema "mwacheni mama huyu aendelee na utumishi wake msimsingizie" mnafikiri wananchi watakuwa interested wakati "rais kashasema"?

Kitu kimoja ambacho nakiona ni mgawanyiko uliopo kati ya "elite" wa Tanzania na wale ambao ni wananchi wa kawaida tu. Walio elite wanataka kupata nafasi za "kutumbua" na wale walioko mtaani wanatamania nafasi za kutumbua.

Kibovu zaidi ni kutumbua bila kuwa na ubunifu. Sijaona mtanzania akatumbua na kuanzisha biashara yenye kutoa ajira au faida.
 
Huyo Mwele Ntuli wakati akimaliza Bsc Mlimani 1980s- na ni kweli alifaulu kawaida kama wanafunzi wengine. Nakumbuka wakati huo Tanzania ilikuwa ndo inaanzisha kitengo cha Utafiti- Wizara ya Afya. Wakati huo qualification ya kupata kazi kule ilikuwa ni GPA kubwa na walioajiriwa wakati huo waliajiriwa kwa GPA kubwa. Huyu mtoto mama yake (marehemu) alimleta kumwombea kazi kwa Mkurugenzi kwa vile alikuwa na GPA ndogo na alikuwa msichana.

watanzania ni watu wa ajabu sana. yaani akikuzida shule ya chekechea basi anatarajia kwamba ni haki yake toka kwa Mwenyezi Mungu akushinde chuo kikuu na hata kazini.

Mwelecela ana PhD toka London University, ana uzoefu wa kazi wa muda mrefu tu. Lakini bado Watanzania wanamsengenya kwasababu kuna waliokuwa na GPA nzuri kuliko yake for her bachelors degree.

Dr.Seche Malecela anajulikana kwamba ni kipanga toka sekondari mpaka Muhimbili. Ninavyoelewa mimi Muhimbili is the toughest college in Tanzania. Kwa msingi huo nawaheshimu wahitimu wote waliotokea Muhimbili.

Sikubaliani na mengi anayosema FMES au approach yake kwa masuala mbalimbali. Lakini hili la watoto wa Malecela[Mwele & Seche] niko pamoja naye 100%.

Katika viongozi wetu wa awamu ya kwanza nadhani Malecela na Msuya wamejitahidi sana katika malezi na elimu. Huwezi kusikia vijana wao wamepigana ktk baa, au wameshitakiwa kwa domestic violence.

NB:
wako watoto wa viongozi wanaokunywa baa na kukataa kulipa.wengine wanatia ngeu spouces wao kwasababu wao ni watoto wa wakubwa.
 
Back
Top Bottom