Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje??

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara..
Mchanganyiko, mara mzaramo, mara mnyakyusa, mkoa wa Mara. Ulitaka kutuambia makabila au wema wa muuza samaki kwa mjamzito ?
 
Wema usiizidi Akiba, Huenda hakuna kinachoharibika kwa huyo mama hata kama anamsaidia.
 
Mwanamke mjamzito huwa anatia huruma fulani hivi.

Jana tulikuwa tunaongelea watu wanaokuja kwa Mwamposa kutoka mikoani na kukosa huduma za kijamii. Kuna jamaa mwanaume anasema ilibidi amuokoe mwanamke mjamzito aliyekuja kwa Mawamposa bila mwenyeji, akawa anaumwa, ikabidi jamaa amchukue ampeleke nyumbani kwake, ambako alikuwa na mke tayari, mpaka akaingia lawamani majirani wakawa wanamwambia mke wake kwamba huyo bwana kamletea mkemwenza.
Chai
 
Kwa Taarifa Yako, na ufanye utafiti watu wenye vipato vidogo ambao unawatazama kama maskini, ni matajiri wakubwa wa Roho na ni wepesi kusaidia wenye shida kuliko matajiri wenye uwezo mkubwa! Na hii ndio maana Ile ya heri walio maskini mana watakuona ufalme wa Mungu! .kuwafikia matajiri kuwaomba msaada ni ngumu mpaka wao watake mwisho wa mwaka kama hauu wakatoe masazo ya mwisho na makamera! Wewe kwakua umeona Hilo na wewe weka mkono hapo! Nisaidie wako wapi nikaguse maisha Yao na Mungu aniinulie watu waguse maisha yangu pia! We shine by lifting others!
tajiri anauogopa umaskini hataki kabisa chezea hela yake kwa upumbavu wa kuita msaada maana anajua hata siku akifirisika hao alio wasaidia ndo wakwanza kumbeza ko hataki hali hii
 
roho nzuri ama mbaya ni mtu kuzaliwa nayo

nna mshikaji wangu ana roho mbaya ana roho ya uchoyo hata yeye analijua hilo

kuna siku tumekaa analaumu kwa nini mtoto wake wa kwanza ni me hana roho ya mbaya (uchungu na kitu chake )

anamfurahia mtoto wake wa kike kumfata roho ya uchoyo (yeye anaita uchungu na kitu chake)
 
Wewe ujaelewa ninacho maanisha ...kuhusu ulicho uliza ni kwamba nilimaanisha wazaramo awajikwezi wanaroho nzuri kuliko makabila mengi ...sasa hayo makabila mengine watu wake kiasili ni wabinafsi na wana roho mbaya wakichanganya na dini zao wanazo zitumia kinafiki ndiyo inakua balaaa
Mkuu, mimi ni mtu wa mkoa wa Mara, ila makabila ya Pwani wengi hawajasoma sana lakini wana mioyo ya utu na upendo mno..
 
Yesu alitoa mifano mingi sana, na mmoja wa mfano huo ni huu "Haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo hamtairithi mbingu"
Kuna watu tunadharau dini zao, kuna watu hawana muda na mambo ya ibada lakini haki zao ni kubwa kuliko viongozi wa dini.
 
roho nzuri ama mbaya ni mtu kuzaliwa nayo

nna mshikaji wangu ana roho mbaya ana roho ya uchoyo hata yeye analijua hilo

kuna siku tumekaa analaumu kwa nini mtoto wake wa kwanza ni me hana roho ya mbaya (uchungu na kitu chake )

anamfurahia mtoto wake wa kike kumfata roho ya uchoyo (yeye anaita uchungu na kitu chake)
Aiseee huyo jamaa yako ana roho ya ibilisi kabisa
 
Sijajua umetoka jamii gani na Mnatabia gani hasa kwenye utu na ubinadamu, ila ni kawaida sana, mfano wanyakyusa wana ndugu wa hiari wengi sana, na makabila mengi tu wamasai, wasukuma, wameru ndio usiseme unabatizwa hadi jina la ukoo
Okay. Asante kwa kunipa elimu..
 
Back
Top Bottom