Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje??

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara..
Km hujui wengi wenye vipato hivyo ndo Wana roho mzuri,fuatilia utaona kulinganisha na wenye uwezo
 
sasa ww ushasema binti ni yatima..kuna baraka kubwa sana kumtunza yatima pia kuwasaidia wajane na maskini..hata marehemu mengi na matajiri wengine walisaidia sana yatima kuwasaidia makumdi hayo ni sadaka kubwa sana..ila wengi tunapuuza kisa eti hatuna undugu nao tumejaa roho mbaya na ubinafsi..ni watu wachache tu wanaojua siri iliyopo kwenye kuwasaidia maskini,wazee,wajane na yatima waache wavune hizo baraka pia hio ni kinga kubwa sana kiroho..
 
Nililelewa na mama wa kambo tangu nikiwa 2yrs old nikiri tu kuwa yule mama alinilea vizuri mno na Mungu ampe maisha marefu.Mama mzazi mwenyewe anampigia salute yule mama wa kambo
Unarikiwe Kwa kuona Hilo,mama angu kawalea 6 watt wa nje ila malipo yake ,nimesema sitakuja Lea mtt was mtu
 
Yes , I can elaborate it .
Yesu alitoa mifano mingi.
Mmoja alisema wazinzi na walevi watawatangulia kuingia kwenye ufalme wa mbinguni alimaanisha kuwa kuacha tabia ya uzinzi na ulevi haitoshi kukudanya uingie mbinguni ikiwa moyo wako huwaza mabaya juu ya mwingine, au ikiwa huleti furaha katika maisha ya mtu mwingine.
Kuhusu haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo hamtairithi mbingu maana yake ni kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa na moyo safi na matendo safi zaidi kuliko watu wa dini.
Yaani you should do more than religious people they do.
Hapo mwisho nakubaliana na we ila hapo mwanzo ,km nakumbuka vzr hao waliambiwa hawatainiga mbinguni
 
Yes , I can elaborate it .
Yesu alitoa mifano mingi.
Mmoja alisema wazinzi na walevi watawatangulia kuingia kwenye ufalme wa mbinguni alimaanisha kuwa kuacha tabia ya uzinzi na ulevi haitoshi kukudanya uingie mbinguni ikiwa moyo wako huwaza mabaya juu ya mwingine, au ikiwa huleti furaha katika maisha ya mtu mwingine.
Kuhusu haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo hamtairithi mbingu maana yake ni kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa na moyo safi na matendo safi zaidi kuliko watu wa dini.
Yaani you should do more than religious people they do.
Okay..
 
Wandengereko wako karibu zaidi na wangindo, wamatumbi kitabia kuliko wazaramo.
Wazaramo wako karibu na wakwere na wadoe.
Mkuu wandengereko na wazaramo ni kitu kimoja.

Boga Maneremango (Kisarawe) kwenye original wazaramo na Rufiji wamepakana.

Ndio maana unaona huko kote wana mambo yao ya unyago ambayo DC Magoti alikuwa akipambana nayo, na wanaoana sana.

Vinginevyo hoja ya mada issue sio ukabila ni maternal instincts tu za wanawake, previous experience ya mtu and humane (kuna binadamu wana-huruma tu), nothing to do with tribe but individual behaviour only that not every good deed is documented in the world.
 
Upande wa mama yangu wandekereko na wameoana na wazaramo.

Kisarawe ndio kwenye wazaramo haswa; na inapakana na Rufuji.

Wakerwe na (wazaramo na wandekereko) watu tofauti.
Asante sana kwa kunipa elimu ya ziada ndugu yangu..
 
Roho watu wanazo, tatizo ni binadamu hawa washenzi sana.
Nilimlea mjinga mmoja alinifunza akili ya kuwa na roho mbaya.
Saidia achana nae.
Kuna mmoja kaiba pesa kabisa cash huku nilimkaribisha tu asipigwe baridi akafa nje huko.
Mnyarwanda.
Mwingine mbongo mkimbizi mbali huko.
Kumkaribisha kaenda kwenye kesi zake kanishtaki kumnyanyasa ili apate papper zake.
Mi sina habari.
Huyo binti anaweza kuja kum dissapoint sana tu mama muuza samaki akabaki na wenge.
Binadamu hawa acha tu.
 
Hongera! Siku hizi umetelekeza chama cha CCM. Huweki uzi kusifia tena. Wewe pamoja na malaria sugu mepotea sana

Umenichekesha

Mimi nawekaga nyuzi kufanyaje!!!

Basi haunifahamu Coco chanel wa JF, maana kuandika naandika na kama kawa soon Mama tena itaanza
 
Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje??

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara na sio mtu wa Pwani.
hiyo ni tabia ya mtu na sio ya kabila,huyo mama Mungu atamlipa mema
 
Back
Top Bottom