Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

It's around 10K per day and not exactly. Mkuu, 10K per day kwa familia ya watu watatu na mmoja wao ni mjamzito, unasema kuwa hiyo sio pesa ndogo?? Seriously??
Sio kwa maisha ya chumba sebule ya 30k kwa mwezi hata matumizi hayawezi kuwa makubwa. Kuna watu wanaishi 6 kwa kipato cha elfu 5 kwa siku na maisha yanasonga.
 
Mkono utoao ndo upokeao daima
Kabisa ila watu wengu hawalijui hili. Ukiwa unatoa kwa moyo Mungu anakurudishia zaidi yake.

Mimi huwa natoa niko hivyo, naambiwa toka mdogo nina huruma. Nimerudishiwa kwa mengi sana.
La mwishoni, nilikuwa na fundi ujenzi, nikamuona mlemavu mkaka anasotea miguu. Nikawaza bora angekuwa kwenye vibaiskeli vya kusukuma.

Ilikuwa njiani, nikakunja 20k, nikamuomba fundi, akampe. hakukuwa na parking. Ananiambia alishangaa sana, akamwambia mbona nyingi? Ina maana labda huwa anasaidiwa pesa chini ya hapo.

Tulichoenda kufata hatukukipata, tukageuza, nikamuona tena mmmh!!!
Safari hii nilishuka mwenyewe, alikuwa anaingia sehemu ya kula, ilikuwa asubuhi. Nikasalimiana naye na kumpa tena 30k alishukuru sana na ni mpole sana anaonyesha. Nikawaomba wahudumu wamuhudumie chochote, pesa anayo.

Mwezi huu nilimwambia mtu wa karibu, mradi mpya naotaka kuanzisha bahati nzuri ni mwana JF. Aliniongezea 5m. Ilinichukua muda kuunganisha ile 50k imelipwa imekuwa 5m. Nilitoa kwa moyo mmoja kwa yule kaka. So kwenye kutoa ndiyo kunakupokea.
 
Mkuu, mbona hata wanaume kwa wanaume wanafanyiana sana u-snitch. Nothing stinks like a snitch.
Bora kwetu ni wachache sana ila huo upande wao ni balaa zaidi.

Kuna ke wafanya biashara wote nna ukaribu nao na kwa kiasi fulani wananiamini ila hawa viumbe sijui wanachukiana kwa sababu gani. Nikiwa na huyu lazima amseme yule vibaya na vice versa is true ila mimi kimya huwa nawasikiliza tu. Cha ajabu ni wakikutana wanavyochangamkiana utadhani hawajabebeana chuki moyoni 🙌

Hao ni wawili ila wapo wengi mifano ni mingi sana.
 
Please ninaomba tusiingize dini katika mada hii mkuu. Please please please my dear brother..
Mada kama ina husu wema na ubaya moja kwa moja inausika kidini piq ...maana dini ni kujua mema na mbaya kisha ukatenda mema na kuyaacha mabaya ...tumia akili ila kuna kitu kinaitwa unafiki wa kidini hicho ni kutenda mabaya na kuacha mema kisha kujitukuza kuwa una dini
 
Bora kwetu ni wachache sana ila huo upande wao ni balaa zaidi.

Kuna ke wafanya biashara wote nna ukaribu nao na kwa kiasi fulani wananiamini ila hawa viumbe sijui wanachukiana kwa sababu gani. Nikiwa na huyu lazima amseme yule vibaya na vice versa is true ila mimi kimya huwa nawasikiliza tu. Cha ajabu ni wakikutana wanavyochangamkiana utadhani hawajabebeana chuki moyoni 🙌

Hao ni wawili ila wapo wengi mifano ni mingi sana.
Duuh. Balaa.
 
Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje?

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

From my experience, wengi wenu hamkusoma sana na mna vipato vidogo, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo mnoo.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara na sio mtu wa Pwani.
Hata wewe ulipo, jaribu kufanya utafiti wa kukaa na ndugu baki, au yatima ukimtunza, lazima kuna wepesi flani Mungu huuleta katika maisha yako.

Huyo mama ni mzoefu anajua anachokifanya.

Ugali wa mtu mmoja unaweza kuliwa na watu wawili na maisha yakasonga.
 
Back
Top Bottom