Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Nasemaga kila siku humu, wazaramo pamoja na mapungufu yao ila, Kama kuna kitu wamefanikiwa ni kutokuwa na stress, huwa wanaridhika na vitu vidogo sana kwenye maisha
Wabarikiwe sana....hawa ndiyo wa kuoa na kuolewa nao.
Hakuna mbaba mzaramo humu ndani?🤦
 
Hata wewe ulipo, jaribu kufanya utafiti wa kukaa na ndugu baki, au yatima ukimtunza, lazima kuna wepesi flani Mungu huuleta katika maisha yako.

Huyo mama ni mzoefu anajua anachokifanya.

Ugali wa mtu mmoja unaweza kuliwa na watu wawili na maisha yakasonga.
Ukifanya jambo kwa nia njema, Mungu anakuwekea ulinzi automatically..
 
mkuu hilo ni tukio moja, nikieleza hapa huwez amini jamaa ana roho mbaya mnooo.
ila yeye sasa anapenda saidiwa balaa, mtaa anao kaa hakuna mtu anapatana nae. ofisini ni mtu mkubwa tu ila akijua haumkubali ama una urafiki na mtu asiye mkubali basi anakupiga zengwe ufukuzwe

kifupi jamaa ana roho mbaya sana
Shetani hilo.
 
Yes, mkuu. Watu wengi wa Pwani wakiwemo wazaramo na Wandengereko, licha ya watu kuwasema kuwa wanatabia za uswahili kupenda taarabu na singeli, ni watu wenye mioyo mema mnoo..
Sasa kupenda taarabu na singling ni kosa?? Si ndo asili yao?? Nyue wasukuma na wakurya mbons mnapenda ngoma zenu? Uswahili huku ndo asili yake!
 
Wengi ni wale wale tu na hali zao
Yes. Upo sahihi mkuu. Wengi ni wa kipato cha chini, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo.

Kuna mama wa kizaramo alikuwa ni mama Lishe zamani wakati nipo mdogo. Alikuwa akimaliza kuuza chakula, ilikuwa lazima anibakishie wali na maharage. Si unajua tena sisi watoto wa uswazi tunavyopenda ubwabwa??

Mungu aendelee kumpa pumziko jema mama yule huko mbinguni..
 
Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje?

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

From my experience, wengi wenu hamkusoma sana na mna vipato vidogo, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo mnoo.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara na sio mtu wa Pwani.
Ningeomba utushirikishe na sisi tumsaidie japo kwa michango kidogo kwa kadri tutakavyo jaaliwa.
 
Back
Top Bottom