Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Yes. Upo sahihi mkuu. Wengi ni wa kipato cha chini, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo.

Kuna mama wa kizaramo alikuwa ni mama Lishe zamani wakati nipo mdogo. Alikuwa akimaliza kuuza chakula, ilikuwa lazima anibakishie wali na maharage. Si unajua tena sisi watoto wa uswazi tunavyopenda ubwabwa??

Mungu aendelee kumpa pumziko jema mama yule huko mbinguni..
Ni wachache wenye roho mbaya ndio hawafanyi hivyo ila wamama ntilie wengi hata ambao sio wa ukanda huo wanafanya sana hayo.
 
Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje?

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

From my experience, wengi wenu hamkusoma sana na mna vipato vidogo, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo mnoo.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara na sio mtu wa Pwani.
Sasa umetuandikia usenge Gani huu?
 
Ningeomba utushirikishe na sisi tumsaidie japo kwa michango kidogo kwa kadri tutakavyo jaaliwa.
Kama unaniamini unaweza ukanitumia kisha mimi nitampa na kumjulisha kuwa amepewa na wasamaria wema.

ANGALIZO: IF YOU CAN TRUST ME.
 
Mkuu Nilitegemea ulete namba ya binti huyo na anwani kamili ili mwenye chochote achangie lakini umeishia kumchambua tu , natamani ungefanya jambo kwa ajili yake ili hata huo ujauzito tuhangaike nao kama nikumsaidia pesa ya maandalizi ili anapojifungua tu awe na kila kitu .
 
Mwanamke mjamzito huwa anatia huruma fulani hivi.

Jana tulikuwa tunaongelea watu wanaokuja kwa Mwamposa kutoka mikoani na kukosa huduma za kijamii. Kuna jamaa mwanaume anasema ilibidi amuokoe mwanamke mjamzito aliyekuja kwa Mawamposa bila mwenyeji, akawa anaumwa, ikabidi jamaa amchukue ampeleke nyumbani kwake, ambako alikuwa na mke tayari, mpaka akaingia lawamani majirani wakawa wanamwambia mke wake kwamba huyo bwana kamletea mkemwenza.
Aisee
 
Sasa umetuandikia usenge Gani huu?
Hata kama ni vetting hazifanywi hivyo mbw* wewe. Unamtukana mtu hajakufanyia jambo lolote baya. Nenda U.K na Russia uone jinsi wanavyofanya vetting zao kama mtaona wanatukana.
 
Kabisa ila watu wengu hawalijui hili. Ukiwa unatoa kwa moyo Mungu anakurudishia zaidi yake.

Mimi huwa natoa niko hivyo, naambiwa toka mdogo nina huruma. Nimerudishiwa kwa mengi sana.
La mwishoni, nilikuwa na fundi ujenzi, nikamuona mlemavu mkaka anasotea miguu. Nikawaza bora angekuwa kwenye vibaiskeli vya kusukuma.

Ilikuwa njiani, nikakunja 20k, nikamuomba fundi, akampe. hakukuwa na parking. Ananiambia alishangaa sana, akamwambia mbona nyingi? Ina maana labda huwa anasaidiwa pesa chini ya hapo.

Tulichoenda kufata hatukukipata, tukageuza, nikamuona tena mmmh!!!
Safari hii nilishuka mwenyewe, alikuwa anaingia sehemu ya kula, ilikuwa asubuhi. Nikasalimiana naye na kumpa tena 30k alishukuru sana na ni mpole sana anaonyesha. Nikawaomba wahudumu wamuhudumie chochote, pesa anayo.

Mwezi huu nilimwambia mtu wa karibu, mradi mpya naotaka kuanzisha bahati nzuri ni mwana JF. Aliniongezea 5m. Ilinichukua muda kuunganisha ile 50k imelipwa imekuwa 5m. Nilitoa kwa moyo mmoja kwa yule kaka. So kwenye kutoa ndiyo kunakupokea.
yaaaah kutoa kwa moyo mkunjufu kuna faida sanaa.
 
Back
Top Bottom