Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

ukiona kabeba mimba kajipanga
 
Kweli tumetofautiana,wengine furaha wanaipata kwenye kusaidia wengine.
Mungu ambariki sana
 
Hayo mambo ni yakawaida hasa kwa huku mikoa ya pwani kwasababu wengi wao uislamu umewalazimisha kwa msisitizo kuwa kumkirimu mwenye shida unapata thawabu
Uislam haujawalazimisha bali umewafundisha.

NB: Mimi sio Muislam..
 
Lakini wapemba hawana roho nzuri hata kidogo
Mtazame Hayati Maalim Seif au Rais Mstaafu Dr. SheIn, Dr. Hussein Mwinyi.

Wapemba wengi (almost 90%) ni watu waungwana sana.

NB: Sifanyi uchawa ili kupata favor au pesa, I'm talking the real thing.
 
Wakalim wako kila mahali wabaya wapo kila. Wakalim wapo kila kabila wabaya wapo kila kabila. Pongezi Kwa mama wa kizalamo respect mungu amzidishie
 
Wakati nakuwa nilikuwa nashangaa sana tabia kama hiyo ya mama yangu Mzaramo na kipato chake kidogo Cha ualimu, Yan pale nyumban Magomen ndugu na majiran walikuwa wanajaa hasa, wakat mwingine hadi wakat wa chakula ilitulazimu tuweke Sasa mduara. Haya yote tisa, kumi mzee wangu alifariki tangu mwaka 1999 kama sikosei ila mpaka Sasa ndugu wa baba walikuwa wakitoka Morogoro kwa wapogoro huko wanafikia nyumban Magomen na yeye bila kinyongo anawakaribisha. Na hao hao ndugu mzee alivyofariki walitaka nyumba iuzwe. Sasa huwa namuuliza bi mkubwa kwanini mpaka leo huwa unawapokea, huwa hunijibu kwa kucheka tu. Mungu amuweke sana bi mkubwa Kwan Sasa ana miaka 74.
 
Wakalim wako kila mahali wabaya wapo kila. Wakalim wapo kila kabila wabaya wapo kila kabila. Pongezi Kwa mama wa kizalamo respect mungu amzidishie
Yes mkuu wakarimu wapo kila pahala, lakini kesi za kupiga mapanga ulishawahi kuzisikia kwa makabila ya watu wa Pwani?? Hakika Mungu hakupi vyote. Mungu anakupa hiki kisha anakunyima kile. Watu wa Pwani Mungu kawapa utajiri wa roho, amewanyima Mali tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…