Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Ina maana kina zitto na kina maria sarungi wamemtekeleza huyu mama pamoja na kumtumia kote kule kabendera wakishirikiana na mabeberu? Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Nae ajifunze akitoka, alipokuwa anatumika hakujua kuna mama na ndugu zake wanamtegemea.?Wacha ale jeuri yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu akishakula whats next au faida
 
Mbona ccm hawaposti hii clip kumjulisha rais wa wanyonge kuna mwananchi anateseka
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."


View attachment 1291137

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo mambo ya laana kuna watu hawayafikirii aise! Muhimu ni kutii mamlaka na kujiepusha kushindania na wenye mamlaka vinginevyo mnyonge utaishia kuumia

Sent using Jamii Forums mobile app
kwelii mkuu ...... mm binafsi nikiangalia chain iliyoko nyuma yangu huwa naishia kuwa mpole tuu forthe sake of watu walioko nyuma yangu
 
Hukumu ya Malinzi umeisikia ? kabla ya hapo mashitaka yake ungeweza kudhani hukumu yake ingekuwa kunyongwa , kumbe wakati mwingine hizi kesi zinakuwa za kutengeneza
basi tusubiri mahakama itoe hukumu na sio hukumu zote zinakuwa nyepesi....tusifananishe tuache mahakama ifanye kazi yake......na ukweli utabaki kwamba sio lazima mama yake ajue mwanae anachokifanya
 
Back
Top Bottom