kwelii mkuu ...... mm binafsi nikiangalia chain iliyoko nyuma yangu huwa naishia kuwa mpole tuu forthe sake of watu walioko nyuma yangu
Huyo sio mwanae wa kwanza wa mama kabendera kupata matatizo ndio maana anasema Katika watoto wote Kabendera ndio Yuko vizuri kwake aliwalea watoto wake ki hooligan huyo mama bila kujua urembo una mwishoKwahiyo wote wanaofanya mambo kinyume hawakulelewa vizuri? Sidhani kama kuna mzazi anamlea mwanae ili aje kupata matatizo mbeleni
Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo mambo ya laana kuna watu hawayafikirii aise! Muhimu ni kutii mamlaka na kujiepusha kushindania na wenye mamlaka vinginevyo mnyonge utaishia kuumia
Sent using Jamii Forums mobile app
MkuuMtoto usimchekee kwenye malezi aweza kupangisha shida mbeleni.Mama kabendera ajilaumu mwenyewe kulea watoto hovyo
Kumtukana Rais nje ya mipaka ya nchi ni kulitukana Taifa, kuungana na wahujumu wa rasilimali zetu (ACACIA) na kudidimiza juhudi za mkuu wa nchi wa kuzipigania ni swala lisovumilika, alivuka mipaka.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yapo zaidi ya haya, maana hata rangi ya ngozi yako tu, inaweza kukupeleka Lupango. Hii ni rangi tu wala si kosa lako. Hivyo msifikiri walioendelea hawana magereza! Vitendo vibaya alivyofanya Kabendera, ksma ni kwenye nchi hizo - utaishia GuantanamoKwa Africa sio kwa jamii zilizoelimika uyakuti haya
Uko sahihi Yohana mbatizaji alikatwa kichwa aliposhindana na Herode.Mtu akishindana na mamlaka awe tayari kichwa chake kuwekwa kwenye gogo la mchinja kichwa na asipige yowe kikiwekwa kichwa chake kwenye gogo la chinja chinjaMkuu
Haya Mambo ya kupimana ubabe na mamlaka za kidunia, zilileta madhara makubwa hata kwa Yesu Kristo mwenyewe.
Nimeona pia na kusoma mauaji na mateso makubwa unapotaka ku 'prove wrong' serikali yeyote. Hata mbinguni ushindani huu kimamlaka na nguvu kulifanya Lusifer na malaika wengine waasi. Mwenyezi Mungu akamtupa huku ulimwenguni.
Steve Biko na vijana wa aina yake leo ni history kule Africa Kusini, no one cares whether they were fighting for justice or not.. Ni kovu kwa familia zao.
Kupingana na utawala, kuuchongea au kushawishi wengine waupinge, hata kama upo sahihi au hapana, lazima matokeo yake uwe tayari kuyakabili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaamini kabendera alitakatisha pesa ?Nimemuonea huruma sana huyu bibi na sisi watoto tujifunze tunapokuwa sehemu tujifunze tutii mamlaka tunawapa tabu sana wazazi wetu
Naunga mkono hoja, Erick asamehewe bure!Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.
Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.
Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.
Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”
"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.
Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.
"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.
Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.
"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."
View attachment 1291137
Unaamini kabendera alitakatisha pesa ?
Fuatilia hukumu ya Jamal Malinzi naamini utajifunza kituWewe unatumia vigezo gani kuamini kwamba alikuwa hatakatishi pesa?
Tena huyo inatakiwa anapotoka huko korodani zisiwe zinaning'inia ili iwe fundisho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wacha kamba wewe, wewe unafahamu zaidi ya mwenyewe Kabendera? Serikali ina taasisi ya kuchunguza mambo mengi sana sio mtu moja tu anaamua. Unafahamu jinsi Serikali zinavyofanya kazi zake?Fuatilia hukumu ya Jamal Malinzi naamini utajifunza kitu
Myopic thinking! Unadhani mtakatishaji anagawa pesa kwa mama! Waulize akina Sigh kama wana access na hizo pesa.Kabla hujafa hujaumbika , hivi kama kweli Kabendera ni mtakatisha pesa huyu mama angelia namna hii ? endeleeni na ukatiri wenu lakini mtakuja kulipa tu
Hata mm namuonea huruma Sana bibi yangu huyuNimemuonea huruma sana huyu bibi na sisi watoto tujifunze tunapokuwa sehemu tujifunze tutii mamlaka tunawapa tabu sana wazazi wetu