Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwani kabendera alifanya kosa gani linalomfanya astahili kunyongwa?.Kosa alilofanya huyu dogo kwa taifa hili alistahili kunyongwa,sema Magufuli anahuruma sana
Nimemuonea huruma sana huyu bibi na sisi watoto tujifunze tunapokuwa sehemu tujifunze tutii mamlaka tunawapa tabu sana wazazi wetu
kwani kabendera alifanya kosa gani linalomfanya astahili kunyongwa?.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani alikuwa anamshirikisha mama ake kwenye utakatishaji?Kabla hujafa hujaumbika , hivi kama kweli Kabendera ni mtakatisha pesa huyu mama angelia namna hii ? endeleeni na ukatiri wenu lakini mtakuja kulipa tu
Unalazimishwaje? Unalazimishwa na nani? Kwa hiyo unaweza pia kulazimishwa ku.......wa?
Mkuu wewe Ni mwanaume au Ni mwanamke?Inasikitisha. Kuna mtu kanitumia hiyo video whatsapp na sikutaka kuifungua nikaamua kuidelete, ingenitoa machozi.
WameshapostMbona ccm hawaposti hii clip kumjulisha rais wa wanyonge kuna mwananchi anateseka
Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka kusema angejua asingemuombea msamaha?mama anaweza kuwa hajui mwanae anachofanya
Sio issue ya uraia tena? Kumbukeni dunia duara, wako wapi kina Gaddafi?Kumtukana Rais nje ya mipaka ya nchi ni kulitukana Taifa, kuungana na wahujumu wa rasilimali zetu (ACACIA) na kudidimiza juhudi za mkuu wa nchi wa kuzipigania ni swala lisovumilika, alivuka mipaka.
Sent using Jamii Forums mobile app
jenga hoja kwa kujibu hilo swali
Laana hushika hata kizazi cha nne,hivyo hata wewe taabu+dhiki+upumbafu ulio nao ni matokeo ya laana za walio kutangulia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Haijalishi jinsia mkuu. Rudi kwenye mada punguza dharau za kipumbavu. Viongozi wako wakubwa kabisa wanatoa machozi hadharani umeshawahi kuwauliza jinsia zao?.Mkuu wewe Ni mwanaume au Ni mwanamke?
Na Kama utakuwa phillipo mwanaume Inasikitisha Sana kwa ujumbe ulioandika. Ama kweli kila kukicha idadi ya wanaume inaendelea kupungua kwa kasi Sana mtaani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Daima tukumbuke haya tunayo watendea watoto wa wenzetu kwa kutumia vyeo tulivyopewa na wananchi ndivyo watoto wetu watakavyo tendewa huku tukishuhudia ,wakati huo hatutaweza kufanya lolote sababu tutakuwa hatuna mamlaka yoyote.Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.
Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.
Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.
Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”
"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.
Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.
"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.
Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.
"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."
View attachment 1291137