Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."

View attachment 1291137
Aiseee too sad

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ameonewa inasikitisha hasa kuona mama kama huyo analia mbele ya kamera ila kama ni kweli anayotuhumiwa no way lazima sheria zifuatwe kama wengine,huyu nikwasababu tu ya umaarufu wa kesi ya mwanae ila kuna wazazi wengi wanalia kwasababu watoto waliokuwa wanawategemea wapo nyuma ya Nondo
 
Usipofunzwa na wazazi utafunzwa na ulimwengu
Mama yeye anaona raha kutunzwa kwa pesa haramu ya malipo ya usaliti na kutukana watu
Mama waambie hao watoto waliobaki wakutunze
 
Dah umeugusa moyo wangu! Kinachoniuma wale wote waliokuwa wanashirikiana nae wamekaa pembeni anapata tabu peke yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe binafsi ulishakwenda kumtembelea gerezani mara ngapi? Au huyo bibi ulishawahi kufika kwake kumuachia angalau sukari nusu kilo?

Wanaomtesa Erick Kabendera pamoja na familia yake ni Watz wenzake. Hakika kuna majibu kwa machozi ya familia yake. Watz wenzake wasipomtetea basi ardhi italia kwajili yake kwani machozi yale yanamwagikia ardhini.

Sijawahi kwenda kumtembelea, na kama ni kumtembelea utambuwa wako wafungwa na mahabusu wengi wanaohitaji faraja na msaada kama ingetokea kwenda kumtembelea basi so yeye tu bali na wengine pia.
Kuna wafungwa na mahabusu wameonea huko na hata uwezo wa mwanasheria hawana na hawana hata mtu wa kupelekea Ndugu zao camera na waandishi waililie Serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."

View attachment 1291137
Kalamu na "keyboard' ndizo ambazo zilikuwa ni zana za kazi azitumiazo Kabendera kujipatia riziki zake. Alikuwa ni muajiriwa ambaye gazeti lililotumia uhariri wake, lilkuwa huru na wala halifungamani na itikadi za vyama, milengo ama mitizamo yenye kutaka kuufurahisha utawala wetu. Kwa hiyo alitimiza wajibu wake ijapokuwa wenye nchi hawapendi kabisa kukosolewa.

Maombolezo na machozi ya mama huyu si ya kuyabeza hata kidogo, yanagusa haki za mbingu ambazo neema na rehema huelekezwa, ambazo Muumba wetu hawezi kuwaacha salama wale wenye kwenda kinyume haki hizo kutoka kwa watesi wa waja zake aina ya huyu mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujipange wana JF si tuna hela sisi buku-buku kila mmoja wetu, tumpelekee huyu Mama. kila baada ya mwezi. muone mtakavyo barikiwa,

wale wote wanaotufuatafuata humu ndani ili tusitoe yetu maoni watatulia na homa za ghafla,

you will nevr know until you have tried

Max uko wapi?
 
Back
Top Bottom