Mama mzazi wa Martha Mwaipaja alia kwa uchungu, akithibitisha kuwa mwanae huyo hamsaidii kutokana na mzozo na mdogo wake Beatrice

Mama mzazi wa Martha Mwaipaja alia kwa uchungu, akithibitisha kuwa mwanae huyo hamsaidii kutokana na mzozo na mdogo wake Beatrice

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mama mzazi wa Martha Mwaipaja amezungumza na kuthibitisha kuwa yale yaliyosemwa na mdogo wake, Beatrice Mwaipaja kuwa muimbaji huyo wa 'Hatufanani' hamsaidii.

Akizungumza kwa uchungu kwenye mahojiano na Wemu Online TV, Mama huyo amesema alizaa watoto watatu wakiwemo Martha na Beatrice wanaopishana miaka 2 ambapo mtoto wa kwanza alifariki dunia. Mume wake, baba yao Martha na Beatrice alifariki 1995.

Anasema hadi sasa ana wajukuu wanne tu, mtoto wa Martha ambaye ni wa kiume aliyezaa na aliyekuwa mume wake, watoto wawili wa Beatrice, na mmoja aliyeachwa na marehemu mwanae wa kwanza.

Pia, Soma: Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Amesema, Joan alienda kwa Martha kama mfanyakazi wa ndani na kwamba alimweleza kuwa ni mtoto yatima anayehitaji msaada. Mama huyo amedai kuwa kwa sasa Joan ndiye anayeamua kila kitu katika maisha ya Martha na kwamba yeye ndiye amekuwa akimzuia asimsaidie.

Ameeleza kuwa hata mjukuu wake, mtoto wa kuzaa wa Martha naye amekuwa akiishi maisha yasiyo na furaha. "Yule mtoto (Joan) ndiye ambaye ametanda pale sebuleni," ameeleza Mama Martha kwenye mahojiano hayo.

"Mtoto wangu mpaka ninamuita 'Martha hebu njoo umuangalie mtoto huku jua linampiga halafu ninyi mmekaa sebuleni, hujui' alikuja tu akashika tu kidevu akaangalia mwanangu, akaondoka. Mtoto yule hana raha na mama yake."

Mama huyo anasema amefanya kila awezalo lakini amemshindwa Joan. "Mimi kama mimi nimemshindwa, na ndio maana Beatrice ameamua kuongea, umma umsaidie, naomba mtusaidie," ameeleza.

Anasema Martha na Beatrice wameanza kugombana mara baada tu Joan alipoingia kwenye maisha ya Martha.

"Kwasababu [Joan] ameoana kwamba Beatrice anaufahamu kwamba huyu ndiye anamchanganya dada yake, kwahiyo akiangaza kuongea, huyu binti ndipo anaanza kugeuza maneno na kumpandikizia roho ya kwamba mdogo wako hakupendi."
 
Back
Top Bottom