Mama wa Martha Mwaipaja akihojiwa na Wemu Online TV, mama mzazi wa Martha amesema alizaa watoto watatu wakiwemo Martha na Beatrice ambao wamepishana miaka miwili, amesema mtoto wake wa kwanza alifariki miaka ya nyuma hivyo wamebaki Martha na Beatrice
Mama huyo amesema aliyoongea Beatrice ni kweli kuwa Martha hamhudumii mama yao huyo
Mama huyo amesema yeye ana wajukuu wanne tu ambao wawili ni watoto wa Beatrice, mmoja ni mtoto wa mwanae aliyefariki na mjukuu wake mwingine ni mtoto wa kiume ambaye ni mtoto wa Martha
Hivyo amesema Joan sio mjukuu wake na wala Joan sio mtoto wa Martha bali Joan alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Martha ingawa aliambiwa na Martha kwamba Joan ni yatima anamlea
Mama huyo amesema Martha hamhudumii hata mwanae halisi wa kiume anapata shida
Mama huyo amesema ni kama Joan ndie mwamuzi wa mwisho kuhusu maisha ya Martha. Huku akisema kuna wakati aliponea chupuchupu kutapeliwa kiwanja chake na Joan kiwanja ambacho alinunuliwa na mwanae
Mama huyo amesema mifarakano ilianza kuibuka Joan alipoanza kuwa karibu na Martha kwa madai kwamba Joan amekuwa aligeuza maneno kuwagombanisha Martha na Beatrice
View: https://youtu.be/-rsmiaXel2s?si=1Xq2ewRxZONUkk8o
Tazama Video hii