TANZIA Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019

TANZIA Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019

Mwanae wamempachika kosa la uongo ili wamfunge mdomo, mama wa watu amekaa hospitali siku zote akiamini kuna siku angemuona tena mwanae, na ninaamini amefikwa na mauti akijua mwanae ataachiwa, bahati mbaya waliomshikilia mwanae ni wanyama, makatili, wauaji, wasiojali utu, najua wapo watakaosema Erick ana kosa ni mtuhumiwa, lakini mimi nasema hilo walilompa ni la uongo, kwa sababu halina dhamana wameamua kumficha mahabusu ili asiendelee kuandika zile makala zake.

Wamemnyan'ganya mwanae haki yake ya kumuona mama yake siku za mwisho wa uhai wake, iko siku Mungu atawalipia wote walioguswa na msiba huu, Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya mama mzazi wa Eeick mahala pema peponi, Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kawaida yetu kama watanzania na imezoeleka palee tunapokutwa na msiba wenye kuvuta hisia za watanzania wengi viongozi wetu hutoa salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na familia ya wafia

Kama tulivyozoea, tunaomba kusikia salamu za rambirambi zikitumwa kwa wanafamilia na ndugu wa mama mzazi wa Erick Kabendela aliyefariki leo hii


Huu msiba ni wetu sote
 
Duh, surface route cause inaweza kuwa maswaibu anayopitia kijana wake nini?
Ni kawaida yetu kama watanzania na imezoeleka palee tunapokutwa na msiba wenye kuvuta hisia za watanzania wengi viongozi wetu hutoa salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na familia ya wafia

Kama tulivyozoea, tunaomba kusikia salamu za rambirambi zikitumwa kwa wanafamilia na ndugu wa mama mzazi wa Erick Kabendela aliyefariki leo hii


Huu msiba ni wetu sote
 
jd41,
Kuna wakati nahisi kama mungu hayupo? Alie fanya dhambi kwa huyu kijana na kumfanya mama yake afe, atakufa mdomo wazi
 
Ni kawaida yetu kama watanzania na imezoeleka palee tunapokutwa na msiba wenye kuvuta hisia za watanzania wengi viongozi wetu hutoa salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na familia ya wafia

Kama tulivyozoea, tunaomba kusikia salamu za rambirambi zikitumwa kwa wanafamilia na ndugu wa mama mzazi wa Erick Kabendela aliyefariki leo hii


Huu msiba ni wetu sote
Tuma kwanza wewe. Hivi amekufa kwa ajali au kifo cha kawaida?
 
Watanzania wangapi wanafariki kila siku? kwamba marehemu mama Kabendela ni special sana?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni bibi yetu alipata mateso makubwa yaliyosababisha Mtoto wake aliekuwa akimtunza kubambikiziwa mashtaka mazito ya uongo wa wazi, hili usilipinge la kubambikiziwa Kama hauko upande ule unalielewa kuwa ni kesi za uongo zinazowekewa watanzania Kwa awamu hiii ila Kama uko upande ule ruksa Kupinga.

Hivyo Watanzania wengi walikuwa wakifuatilia hali yake na wengi kifo kimewagusa mno tena wengi wanesononeka na kutokwa na machozi kutokana na mazingira ya kifo, na ukiangalia sana kuna watu wakubwa serikalini hufa Lakini hawagusi watu wengi hivyo, kwa mantiki hiyo msiba wowote ule unaogusa mioyo ya watu Wengi hupaswa kuwa msiba wa kitaifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena na wao mama azo wafe katika mateso makali
MUNGU amuweke mahala pema mama Kabendera..mnaosababisha mama zetu wafe kwa mawazo mlaaniwe vizazi vyenu vyote, mama zenu, shangazi zenu, binamu zenu, watoto wenu, wajukuu zenu na mpaka kuku wenu wafe pia kama ambavyo wamekufa ndugu zetu kwa sababu zenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bibi yetu alipata mateso makubwa yaliyosababisha Mtoto wake aliekuwa akimtunza kubambikiziwa mashtaka mazito ya uongo wa wazi, hili usilipinge la kubambikiziwa Kama hauko upande ule unalielewa kuwa ni kesi za uongo zinazowekewa watanzania Kwa awamu hiii ila Kama uko upande ule ruksa Kupinga, hivyo watanzania wengi walikuwa wakifuatilia hali yake na wengi kifo kimewagusa mno tena wengi wanesononeka na kutokwa na machozi kutokana na mazingira ya kifo, na ukiangalia Sana kuna watu wakubwa serikalini hufa Lakini hawagusi watu wengi hivyo, kwa mantiki hiyo msiba wowote ule unaogusa mioyo ya watu Wengi hupaswa kuwa msiba wa kitaifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo eti watz wengi. Mtoto wake aache apate alichokuwa anakitafuta kwa hao mabeberu. Si unawaona last time walihudhuria hapo Kisutu? Walishindwaje kumsaidia huyo mama kama alikuwa kweli anahitaji msaada wa pesa za matibabu?

Kabendera anapata alichokuwa anakitaka kuna uwezekano hata Mwenyezi Mungu ameamua kumpa somo hili ili ajifunze siku nyingine aache kutumika na mabeberu.
 
Kila nafsi Itaonja Umauti.
Sisi ni wa Mungu, Na kwake tutarejea.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Msiba hauzoeleki.
Mama anauma.


Pumzika kwa amani Mama. Raha ya milele akupe ee Bwana na Mwanga wa milele akuangazie.

Pole yao wafiwa.

Ila wandungu ningewashauri mdhibiti hisia zenu kwenye kuomboleza huu msiba hapa jukwaani. Mnaweza mkapitiliza na kukufuru Mungu kwa kudhani kwamba uwepo wake Kabendera uraiani ungeliweza kuzuia umauti wa mzazi wake. Vitu vingine ni kudra na kadari za Mwenyezi Mungu kama kweli tunaamini uwepo wa Mungu. kwakua hakuweza kuzuia maradhi asingeliweza pia kuzuia umauti.

Pole Kabendera kwa mapito haya unayopitia kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom