Pole sana kwa Familia yake na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampokee na amlaza mahala pema peponi. Tuacheni kuihusisha Kazi ya Mungu kwa Matukio yetu na hasa kwa tukio la Mwanae kwani hapa tutakuwa tunaingilia Kazi yake. Hakuna ambaye anajua kama Mwanae angekuwepo angeishi hadi hivi leo au labda angekufa tokea Kitambo. Najua ni Pigo Kubwa sana kwa Erick na litamuumiza sana kwakuwa yupo matatizoni na sina uhakika kama Sheria za Tanzania au nchi zingine huwa zinaruhusu Mahabusu au Mtuhumiwa au Mfungwa atolewe Gerezani kwenda Kumzika Mzazi wake ila ninachomuomba tu Erick ajikaze, apambanie Haki yake basi pale akitoka huko ataenda Kuzuru mahala ambapo Mama yake Mpendwa amelala Milele. Hata hivyo kupitia hiki Kifo na tukirejea nyuma jinsi Marehemu alivyokuwa akiomba Mwanawe asamehewe tunaweza Kujifunza Somo zuri sana la kwamba tunatakiwa tuwe makini sana hasa katika Nyakati hizi pale unapojipambanua kuwa Mpambanaji kwa Kwanza Kujiuliza je, huna Kundi Kubwa la Watu ambao wanakutegemea huko nyuma? Na kama lipo je, yakikupata ya Kukupata umeshawaandalia Maisha ya Wao kuishi vyema hata kama Wewe utakuwa matatizoni na wale wenye Chuki nawe? Je, hawa ambao wanakushangilia Mitaani na Mitandaoni Siku yakikupata ya Kukupata watakuwa bega kwa bega na Wewe au hata Kuwasaidia Watu wa Familia yako wakiwa na Shida? Mwisho namalizia tu kwa kusema kuwa mambo mengine huwa tunayalazimisha wenyewe na mengine tunalazimishiwa hivyo tujitahidini mno kuwa makini na kamwe tusiwaamini Watu ambao wapo karibu yetu kwani Siku zote Kikulacho Ki Nguoni mwako.
Poleni nyote kwa Msiba huu na pole tena Kwako Erick Kabendera.