TANZIA Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019

TANZIA Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019

The soul and spirit of that mom,shall search a truth and a way to a rightous.
 
The soul and spirit of that mom,shall search a truth and a way to a rightous.RIP.
 
bila kuweka siasa mama kabendere ameacha laana moja nzito ambayo itatembea na mtu kama sio watu .
tena kama roho yake ilisamehe ndo mtaona cha moto mana atakachowaonesha Mungu mtajuta.

tuache dhambi ndugu zangu
 
MUNGU amuweke mahala pema mama Kabendera..mnaosababisha mama zetu wafe kwa mawazo mlaaniwe vizazi vyenu vyote, mama zenu, shangazi zenu, binamu zenu, watoto wenu, wajukuu zenu na mpaka kuku wenu wafe pia kama ambavyo wamekufa ndugu zetu kwa sababu zenu!
Tehe tehe laana ikurudie mwenyewe na kizazi chako,mwenye kazi ya kutoa laana ni Mungu,acha kujipa kazi isiokuhusu
 
Salaam za Erick Kabendera kwa Watanzania kufuatia msiba wa Mama yake Mzazi, Kanisani Chang’ombe Dar es Salaam
3/1/2020

Ndugu Waombolezaji,

Mabibi na Mabwana.

Mimi naitwa Jebra Kambole. Ndiye Wakili wa Erick Matungwa Nolasco Kabendera ambaye ni mmoja wa watoto wa Mama Verdiana Mujwahuzi ambaye tunamuaga hapa kanisani hii leo.

Yeye, kama ambavyo mtoto yeyote angetaka, alitamani kuwa nanyi hapa katika wakati huu lakini kwa sababu ambazo nyote mnazifahamu, ameshindwa kuungana nasi hapa.

Siku hizi tatu zimekuwa ngumu sana kwa Erick. Katika jambo gumu ambalo nimewahi kulifanya kama Mwanasheria ni hili la kumpelekea Erick taarifa za kufiwa na mama yake.

Anapitia katika wakati mgumu sana na nawaomba mumuweke katika maombi yenu ili hatimaye kikombe hiki anachokinywea kwa sasa kimuepuke.

Erick amejaribu kuandika ujumbe kwenu ambao alitaka niusome mbele yenu.

Amepata taabu sana kuandika na kufuta ili kufikisha ujumbe anaoutaka. Ameniambia ametumia na karibu kurasa 20 kuandika ujumbe huu usiku mzima wa jana. Anaandika na kufuta.

Ndiyo sasa nimejua kwamba kumbe kuna wakati hata waandishi mahiri nao hukwama kuandika!!!!

Hatimaye ameweza kuandika kwa ufupi yafuatayo;

Naomba niwasomee.

Kuna Mama mmoja.
Anafariki mara moja,
msiba mara moja.
Uchungu wa kuondokewa na mama ni mkubwa sana, hasa anapokuwa ameondoka na umeshindwa kumuaga kama ilivyotokea kwangu.

Hata hivyo nimefarijika kwa Watanzania wote walioguswa na msiba huu bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na kunisaidia kumsitiri Mama yangu.

Upendo huu umeonyesha nchi ambayo nimeipenda na naipenda kutoka moyoni. Shukrani za dhati ziwafikie watu wote kwa upendo wao na ushiriki wao kufanikisha msiba wa Mama yangu.

Mwenyezi Mungu na awabariki sana na kuwaongezea pale mlipopunguza kwa ajili yangu.

Mtuombee.
 
We live once and die once.
Go mama, go Verdiana.

We shall meet again in heaven where we have a place and prizes.

Pole sana Eric Kabendera, Mungu akupunguzie uchungu na kukupa uvumilivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huna huruma huwezi kupata hisia ya tukio hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu najisikia sympathy sana kwenye tukio hili, ninachomaanisha ni kwamba mambo yetu mengi tunayoyafanya aidha yawe right au wrong tujitahidi tuwafikiria na wale wanaotutegemea kwa ukaribu zaidi kwa sababu chochote utachokifanya dhidi ya serikali lazima kiwe na madhara makubwa zaidi kwako.
 
Back
Top Bottom