Nashangaa mabibi na mabwana afya wanafanya kazi gani ,mimi nina experience kubwa sana ya kula kwa mama nitilie kulingana na shughuli zangu za porini kuchoma mkaa na ujenzi ,mara chache sana nakuwa home...Mambo niliyoyaona ya Uchafu:-
1. Maji wanayotumia kuosha/kusuzia vyombo yaani ni machafu hatari hawayabadilishi at all ,yaani wanaanza kusuzia kuanzia asubuhi hadi usiku,maji hadi yamedilika rangi na kuwa ya kijivu kwa povu la sabuni ,mimi kuepuka haya naenda na sahani yangu na kijiko changu nawaambia niwekeeni humu ,situmii vyombo vyao maana ni kulishana MIUCHAFU tu.
2.Kujichokonoa na vijiti vya Meno huku wakuhudumia wateja ,utakuja muhudumu mdomoni kaweka kijiti najichokonoa mijino then anakitoa anafuta na mkono mwingine bila hata kwenda kunawa anachukua sahani au bakuli anakupakulia chakula yaani Uchafu uchafu ,mimi mara nyingi namwita Manger nawaambia sehemu wanapotoa huduma ya chakula hautakiwi uweke mijti mdomoni utapoteza wateja.
3.Kufuta meza na "Sponchi" lenye maji ya sabuni kisha haendi kuosha mikono baada ya kushika spochi la sabuni ,akitoka hapo anaenda kushika chapati au maandazi anakuwekea yaani ni muchafu uchafu.
4.Kuna baadhi ya mama lishe huwa wanarudisha chakula alichobakisha mteja na kwenda kukichanganya na kilichopo na kuwapa wateja wapya.
5.Kutumia viungo vilivyoharibika kutengeneza mchuzi(nyanya masalo au maparachichi mabovu yaliooza kutengeneza juice) au kutumia unga au mchele mbovu ,mafuta wanayotumia kupikia ni yale waliyokaangia samaki au nyama hata kwa mwezi mzima hadi yanakuwa meusi kama mkaa.
6.Mijasho na Minywele kudondokea kwenye jungu la chakula ,utakuta mpikaji ana minywele hata hajafunika na mijasho "iyaaa: inamtiririka mingine inaingia kwenye jungu.