Mama ntilie Tanzania wachafu; wa Rwanda wana usafi wa hali ya juu

Mama ntilie Tanzania wachafu; wa Rwanda wana usafi wa hali ya juu

Hili jambo halihitaji ripoti ya utafiti. LIKO UCHI. Tatizo bongo tunadekezana sana. Hao wasimamizi wa afya wakisema sheria zifuatwe tutaanza kulia hawajali wananchi wanyonge. Tukitaka mama ntilie wasafi tuache sheria ichukue mkondo wake.
 
Ni vile nchi yao ndogo tu sasa ikiwa chafu wangekuwaje? Ila tangu nakua watu wachafu walifananishwa na wanyarwanda, nimekua nikabahatika kuishi nao hao watu ni wachafu na wavivu ovyo kabisa, mitandao inadanganya sometimes
PK effect. Vile Rwanda na watu wake leo ni matokeo ya Kagame. Na kwa kua ni ka nchi kadogo rahisi kudhibiti na kusisimua mabadiliko kwa urahisi. Tz imejaa vichwa vyenye laana.
 
Tusijisahau na kuwalaumu tu mama ntilie, je wateja wanaweza kumudu gharama za usafi wa baadhi ya gharama au wateja ndiyo wanaosababisha mama ntilie kuleta mazoea katika biashara zao.
Usafi wala sio gharama ki hivyo, kutenganisha jagi la kunawia na la kuchotea maji safi kwenye ndoo au sufuria ni gharama sana??
 
Nashangaa mabibi na mabwana afya wanafanya kazi gani ,mimi nina experience kubwa sana ya kula kwa mama nitilie kulingana na shughuli zangu za porini kuchoma mkaa na ujenzi ,mara chache sana nakuwa home...Mambo niliyoyaona ya Uchafu:-

1. Maji wanayotumia kuosha/kusuzia vyombo yaani ni machafu hatari hawayabadilishi at all ,yaani wanaanza kusuzia kuanzia asubuhi hadi usiku,maji hadi yamedilika rangi na kuwa ya kijivu kwa povu la sabuni ,mimi kuepuka haya naenda na sahani yangu na kijiko changu nawaambia niwekeeni humu ,situmii vyombo vyao maana ni kulishana MIUCHAFU tu.

2.Kujichokonoa na vijiti vya Meno huku wakuhudumia wateja ,utakuja muhudumu mdomoni kaweka kijiti najichokonoa mijino then anakitoa anafuta na mkono mwingine bila hata kwenda kunawa anachukua sahani au bakuli anakupakulia chakula yaani Uchafu uchafu ,mimi mara nyingi namwita Manger nawaambia sehemu wanapotoa huduma ya chakula hautakiwi uweke mijti mdomoni utapoteza wateja.

3.Kufuta meza na "Sponchi" lenye maji ya sabuni kisha haendi kuosha mikono baada ya kushika spochi la sabuni ,akitoka hapo anaenda kushika chapati au maandazi anakuwekea yaani ni muchafu uchafu.

4.Kuna baadhi ya mama lishe huwa wanarudisha chakula alichobakisha mteja na kwenda kukichanganya na kilichopo na kuwapa wateja wapya.

5.Kutumia viungo vilivyoharibika kutengeneza mchuzi(nyanya masalo au maparachichi mabovu yaliooza kutengeneza juice) au kutumia unga au mchele mbovu ,mafuta wanayotumia kupikia ni yale waliyokaangia samaki au nyama hata kwa mwezi mzima hadi yanakuwa meusi kama mkaa.

6.Mijasho na Minywele kudondokea kwenye jungu la chakula ,utakuta mpikaji ana minywele hata hajafunika na mijasho "iyaaa: inamtiririka mingine inaingia kwenye jungu.
 
Binadamu kale aliliwa sababu ya spiritual. Kulikuwa na ibada maalum inayoleta maana ya mtu kuliwa. Unakula paka ina mana bata huwaoni au?
Mkuu, mimi nakula kuku wa kienyeji na kitimoto mara moja moja. Sijawahi kumla paka, ila kama kuna wanaokula, sitashangaa. Hii dunia ina mengi nisiyoyajua, ikiwa ni pamoja na tamaduni za watu.
 
Ripoti inaweza mama ntilie anaweza kujikuna kwapa na maeneo mengine akakupakulia chakula bila kunawa
 
PK effect. Vile Rwanda na watu wake leo ni matokeo ya Kagame. Na kwa kua ni ka nchi kadogo rahisi kudhibiti na kusisimua mabadiliko kwa urahisi. Tz imejaa vichwa vyenye laana.
TZ ingekuwa na dictator kama Kagame na raslimali zake zote ilizonazo, Nina uhakika tungekuwa first World tunashindana na nchi za Europe au at least South Africa
 
Back
Top Bottom