Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Ramso ni msanii wa vichekesho na mtoto wa pekee kwa mama yake, ambaye inasemekana ametekwa na watu wasiojulikana baada ya kuposti video akimtaka Rais Samia ajiuzulu kwani hakuna anayemtaka.
Mama yake ametoka hadharani kuomba msaada wa mwanaye kupatikana ikiwa ni wiki mbili toka mwanaye achukuliwe na watu wasiojulikana.
"Jamani Watanzania mimi ni mama yake Ramso. Rafiki yake Ramso alinipigia simu, nikamuuliza mbona unanipigia simu wewe? Ramso yuko wapi? Akasema mama ndio maana nikakupigia simu, nataka tuonane, tuongee. Nikamwambia sawa. Rafiki yake akaja, nikaonana naye na kuongea naye.
"Akaniambia mama, nilikuwa nimelala chumbani kwangu na Ramsey amelala chumbani kwake usiku wa saa saba. Cha kushangaza niliskia kelele moja tu, basi, kimya. Nikatoka hapo nikaingia chumba chake nikakuta hayupo ila nikakuta simu yake ipo kitandani. Nikatoka nikaenda kuwaamsha majirani nikamwambia jamani mimi Ramso simuoni. Tukamtafute hapa na pale hatujapata,tukatoka hapa tukaenda kituo cha polisi kutoa taarifa wakasema sawa, watafanya uchunguzi lakini mpaka sasa hivi mama sijapata jibu lolote wala nini na ndio maana nikakutafuta wewe.
Pia soma GE2025 - Msanii wa Vichekesho, Ramso atekwa na watu wasiojulikana, aliposti video akimtaka Samia ajiuzulu
"Alivyoniambia hivyo na mimi sikufanya makosa, nikatoka nikaenda kituoni. Nikaelezea kama ilivyokuwa, wakaniambia sawa, tutafanya uchunguzi. Wanafanya uchuzi wanavyodai wao wenyewe hapa na pale lakini mpaka sasa hivi yapata wiki mbili, naenda na kurudi, wananizungusha tu lakini mpaka sasa hivi mwanangu Ramso sijamuona. Sielewi mimi nifanye kitu gani na sielewi niende wapi.
"Kwahiyo jamani chondechonde mwanangu Ramso katika tumbo langu ni huyu mmoja tu ambaye namtegemea, kwahiyo naombeni atakayemwona Ramso muda wowote anitafute anipigie simu.
"Na licha ya kunipigia simu, atakayemuona Ramso mimi nitampa milioni mbili. Milioni mbili hizo sina mkononi, nitauza kibanda changu Kisemvule ambacho nimejenga juzijuzi tu, nitampa mradi mambo mengine yaishe, mwanangu aonekane. Chondechonde naomba mnisaidie jamani." - Amesema mama Ramso
Siku kadhaa kabla kutekwa kijana Ramso alipost video akiwa kweny mazingira ya porini akisema kuwa kuna watu wanamfuatilia baada ya kupost video aliyomwambia Rais Samia ajiuzulu, akawa anaiomba Serikali msahama.
Ramso akiwa anaomba msamaha vichakani
Alichowahi kuongea kwa kumwambia Rais Samia ajiuzulu kwani watu hawamtaki