Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Mchinga, Mkoani Lindi kupita Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Machi 2017, Salma ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akiwa ndio Mke wa Rais wa kwanza kuwa Mbunge nchini pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)

Salma.png
 
Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.

Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.

Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.

Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirisha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).
 
Mtu atayemkata huyu mama hayupo..

Hapo ndipo utakapojua ccm ina wenyewe na wenyewe ni kina nani

Mama Salma ameshapita asubuhii kabisa amechukua jimbo
Anaweza kukatwa na hamna kitu mtafanya,kwani si alishawahi kumwambia Mumewe anawashwa washwa?

Kwa sasa Mwenye Chama ni mmoja tu,wengine wote wameshatwa mkia na cha kufanya hakuna.
 
Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.
Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.
Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.

Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirirsha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).
Nani aliyekuambia ameenda kungombea kwa sababu ya pesa? Kama ameona akawatumikie wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu.
 
Nitakukumbusha.. uzi huu nitaufufua.. kama akikatwa nitaomba mods anipige ban mwaka mzima
Nasema hivi,yeye au rizone wakikatwa hakuna kitu watafanya zaidi ya kununa tu.

Ukiachana mwenye chama wengine wote ni ng'ombe waliokatwa mikia kwa sasa.
 
Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mchinga mkoani Lindi kupita Chama cha Mapinduzi (CCM).

Hivi huyu mama anatafuta nini cha zaidi ambacho hakukipata akiwa first lady? Si astaafu tu jamani!
 
Back
Top Bottom