mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mchinga mkoani Lindi kupita Chama cha Mapinduzi (CCM).
Anaweza kukatwa na hamna kitu mtafanya,kwani si alishawahi kumwambia Mumewe anawashwa washwa?Mtu atayemkata huyu mama hayupo..
Hapo ndipo utakapojua ccm ina wenyewe na wenyewe ni kina nani
Mama Salma ameshapita asubuhii kabisa amechukua jimbo
Nadhani zama zimeanza kubadilika, tujitahidi kuzoea, siku hizi kila kitu ni fasheni.watia nia wamekuwa wengi kushinda hata wapiga kura jamani au mnaonaje?
Acha aingie ulingoni apewe matusi ya kutosha/achafuliwe kwa sana tu ndipo atapata akili vizuri.Huyu mama angetakiwa atulie sasa aangalie mambo mengin ya kifamilia
Anaweza kukatwa na hamna kitu mtafanya,kwani si alishawahi kumwambia Mumewe anawashwa washwa?
Kwa sasa Mwenye Chama ni mmoja tu,wengine wote wameshatwa mkia na cha kufanya hakuna.
Wewe unaogopa matusi ?Mama Salma ni mwanamke na nusu. Chukueni form jamani. Acheni kuwaponda wanaochukuaAcha aingie ulingoni apewe matusi ya kutosha/achafuliwe kwa sana tu ndipo atapata akili vizuri.
Wamekalia kuwaambia watoto wa maskini wajiajiri lkn wao kutwa kulilia ubunge.
Nani aliyekuambia ameenda kungombea kwa sababu ya pesa? Kama ameona akawatumikie wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu.Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.
Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.
Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.
Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirirsha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).
Nasema hivi,yeye au rizone wakikatwa hakuna kitu watafanya zaidi ya kununa tu.Nitakukumbusha.. uzi huu nitaufufua.. kama akikatwa nitaomba mods anipige ban mwaka mzima
Hivi huyu mama anatafuta nini cha zaidi ambacho hakukipata akiwa first lady? Si astaafu tu jamani!Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mchinga mkoani Lindi kupita Chama cha Mapinduzi (CCM).