Mama Salma Kikwete ampongeza Waziri Makamba kuwapa mitungi 100 ya gesi, Spika atolea ufafanuzi

Mama Salma Kikwete ampongeza Waziri Makamba kuwapa mitungi 100 ya gesi, Spika atolea ufafanuzi

Familia imeficha mengi, kweli alionekana kwenye kampeni zake ila hatuwezi jua nyuma ya pazia, wakati mwingine mtu anafanya jambo kukwepa mauza uza katika jamii

Hivi kweli uyu mama na wa kuendelea na ubunge, alafu eti unaamushwa na spika uchangie, mama ambae umekua unampikia Rais wa nchi chakula kwa miaka 10 , kwa shida gani , kwa kukosa nini, uyu ameshindwa kulieshimisha taifa kama mke wa kiongonzi mkubwa aliemaliza mda wake
Kuna jambo litafuata hapo, siyo ubunge kama unavyodhani. Kikwete hazichezei tope bila sababu.
 
Mama Salma Kikwete akichangia bajeti ya nishati na madini leo, alimpongeza January Makamba kwa kuwapa kila mbunge mitungi ya gesi 100.

Lakini baada mwisho wa section ya spika akasimama kutolea maelezo juu ya hili, kwa ufupi.

Kuwa jamii isielewe vibaya juu hili ni ajili ya wabunge kwenda kwa wananchi kuwafundisha kutumia mitungi na umuhimu wa gesi.

Pia bajeti ya kuwapa wabunge mitungi 100, isiwape wasiwasi wananchi pesa imetoka wapi, Ni hela ya bajeti , ambayo wabunge wamepitisha mwaka Jana.

Swali; Kwanini spika kajitahidi sana kutetea hii issue ya mitungi mia ya Makamba?
Bahasha yake haiwezi kukosa 50M
 
Dhana ya kutumia gesi ni nzuri sana katika nchi yetu ambayo miti ipo hatarini kuteketea kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni.
Nampongeza Rais SAMIA kwa akili zake nyingi.
 
Dhana ya kutumia gesi ni nzuri sana katika nchi yetu ambayo miti ipo hatarini kuteketea kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni.
Nampongeza Rais SAMIA kwa akili zake nyingi.
Kutumia gesi haiwezekani, ni propaganda tu hiyo. Kabla ya gesi walipaswa kupunguza umaskini kwanza.

Mtu anayeishi chini ya dola 1 anawezaje kutumia gesi wakati kuni anaokota bure.

Ikifika siku Tanzania maskini wakawa 20% tu, basi hiyo 80% inaweza kutumia gesi japo napo sio rahisi. Mwalimu mwenye familia ya watu watano hataweza kutoboa kutumia gesi pekr yake bila kuwa na mkaa
 
Dhana ya kutumia gesi ni nzuri sana katika nchi yetu ambayo miti ipo hatarini kuteketea kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni.
Nampongeza Rais SAMIA kwa akili zake nyingi.
Dhana ni nzuri ya kuondoa negative energy kwa watu na teknolojia zilizopitwa na wakati, tatizo waliopewa dhamana hiyo hasa huyu wa nishati anajua anachopambania, yeye haya mambo ya kugawa mitungi angepunguza ila angejikita kwenye kunufaisha nchi nzima kwenye eneo lake la nishati, Moja yeye anahusika na umeme na watu wanahitaji umeme ushuke bei ili watumie vitu vya kurahisisha kazi na vya teknolojia mpya waondokane na ujinga wa kupoteza muda na taifa lipate watu werevu mfano mpaka Sasa watu wengi hawajui kufua kwa kutumia mashine hata sehemu kama hospital Sasa huko ndo angegawa hizo mashine badala ya hayo majiko kwa wabunge, pili upande wa mafuta ya kuendesha mitambo na usafiri huko kidogo ameanza kufanya vizuri, Hilo la vituo vya mafuta kujengwa sehemu nyingi ili watu wanaoweza kutumia mafuta wayapate bila kikwazo na usafiri kwa vile ni hitaji la muhimu kwa watu na bidhaa basi wasikwame kabisa na huko vijijini vituo vya mafuta vifike vingi ili barabara zijengwe ila kwenye Bei ajitahidi ipungue, tatu hiyo gesi yake Sasa anayogawa mitungi bila gharama za gesi kushuka haitasaidia nchi watu masikini kuishi kisasa yeye agawe mitungi sehemu maalumu tu ila gesi ndo ishuke Bei ili kila mtu aweze kutumia gesi na Hilo swala lake la uchafuzi wa mazingira litakwisha au kupungua sana, na haya mambo ya kupunguza Bei ndo nchi inatakiwa kufanya ili watu wake wazoee kutumia hivi vitu maana wengi wanaishi Bado kama watu wa kale hawataki mabadiliko na wasipobadilika wanaleta shida kwenye jamii maana hawatasitaalabika Sasa hiyo ya kushusha Bei ingetuonyesha kwamba anadhamila ya kuleta mabadiliko na kuondoa ujinga kwa watu wanaopenda kuishi kama watu wa kale.
 
Back
Top Bottom