Mama Samia akiweza kuvuka 2025, yatakuwa maajabu mapya ya ulimwengu!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kwa haya yanayoendelea sasa hapa Tanzania (ufujaji, upigaji na udalali wa rasimali za taifa), ni mwendewazimu pekee ( tena aliyevaa shati la kijani) anayeweza kuamini kuwa, Mama Samia anaweza kushinda kiti cha urais mwaka 2025. Naandika haya nikiwa na uhakika kamili kuwa, watanzania wengi sana (wakiwemo wanaCCM na makundi ya wanawake) wanamuona mama Samia kama kiongozi muoga, dhaifu na anayeongozwa kifikra na mtu au watu fulani wenye maslahi binafsi.

Mimi binafsi ninamuona Mama Samia kama kiongozi muungwana lakini mwenye uwezo mdogo wa kuweza kuongoza taifa.
 
Hii nchi ilikuwa bado haijafikia hatua ya kutawaliwa na Rais Mwanamke.

NB: Naomba nisieleweke kama mbaguzi. Ninawapenda akina mama. Na wana mchango mkubwa sana katika maisha yangu. Ika nina sababu za msingi.
 
Lazima apite, sisi chawa tupo
 
Kwa aina hii ya Raia? Huyo ahata 20100 anaweza tawala, hii nchi hata mtoto wako Mchanga anaweza itawala, Hii ndio ncji simple kutawala Dunia nzima
 
Kwa mfumo wetu jinsi ulivyo atapita kirahisi tu. Anachohitaji ni kuhakikisha CC ya chama wako happy na wameshiba, baada ya hapo ni wajumbe wa halmashauri na mkutano mkuu.

Ukifika wakati wa mpambano na vyama vya upinzani, atahakikisha katiba mpya ni baada ya uchaguzi mkuu, kwahiyo atakuwa na uhuru wa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama husasani wale wahuni wasiojulikana ambao kwa sasa wako chini yake moja kwa moja kuhakikisha anapata matokeo anayotataka.

Kwa mfumo huu, there is only one way of removing a sitting president, and it's not worth the risk. So people will just wait till 2030 and hope that they can make things right.
 
Nasubiria kuona kwenye kampeni kama ataruhusu maswali kutoka kwa wananchi wanyonge au ataendelea kuwarusha kwamba kero zao wapeleke kwenye vyombo vinavyohusika!
Kingine, sijui kama atahimili mikikimikiki ya kuzunguka nchi nzima akiomba kura za wananchi!!
 
πŸ€“ Ashindwe kwa opposition gani au ipi?? Yaani nani atamshinda kwa mfanoπŸ€“ wa chama gani? Huyu mumama baada ya kugundua opposition ni weak na disorganized ndani na nje ya chama chake akaona hata hakukua na haja ya kumzuia Mbowe gerezani na wala hakuna haja ya kuendelea kuzuia mikutano ya kisiasa. Hii ni baada ya yeye kuhakikisha angalau economically, socially and politically amefanya kitu ambacho anaweza simama mbele za watu kuelezea mafanikio.
 

Kwa jamii ya wa tz, na bunge hili? Anavuka vizuri tu. Utaja niambia
 
Leo kulikuwa na tafrani fulani pale Ubungo Plaza sijaelewa undani wake ila kundi fulani la UVCCM limeswagwa kwa fimbo na kuingia kwenye bus aina ya Eicher, halafu kulikuwa na tenga limeegeshwa karibu na gate linasubiri watakaokinukisha (kuna kakijikundi ni kama kalikodiwa vile)
 
Nakukumbusha before Hilo Kuna kikao nyeti zaid ya Hiko na ndicho kilicho muondoa Mh Lowasa. Kwenye hicho kikao huwa yeye sio mjumbe anajuwa mjumbe kama hataki kuendelea. End
 
Mmmmh Leo umesema hayo
 
Ni kiongozi muungwana Ila kazungukwa na kundi ambalo hawezi kujitoa, na bila Shaka wanamkaririsha kwamba Watahakikisha anashinda kwa kishindo. Tupiganie KATIBA kumaliza huu ugomvi.
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…