Mama Samia ameingia kwenye mtego wa wafanyabiashara kubembelezwa kulipa kodi, tumekwisha!

Mama Samia ameingia kwenye mtego wa wafanyabiashara kubembelezwa kulipa kodi, tumekwisha!

Maombi yangu siku zote ilikua mama asiingie mkenge wa wafanya biashara maana tunajua kitakachotokea.

Bahati mbaya mama ameuvaa mkenge wa wafanya biashara. Tusitegemee chochote cha maana kufanyika kwa miaka 4 ijayo. Mama mwenyewe amekiri kua kwa kauli yake makusanyo yatashuka, unajiuliza kwa nini yashuke?

Mama ana matumaini kua makusanyo yakishuka baada ya muda yatapanda, yatapandaje? Nini kitayapandisha?

Ukiona kiongozi hayuko firm and strong kwenye kodi, basi ujue hiyo nchi iko doomed to fail. Nashukuru hayati alikua wazi kwenye hilo, alikua wazi na firm kwenye hilo

Kodi ni jambo ambalo halihitaji kubembelezana, hakuna mfanyabiashara anaetaka kulipa kodi, awe tajiri mkubwa awe mdogo hakuna. Kipindi kile Magufuli anaingia kina Azam walikutwa wanakwepa kodi ya kutosha,itakuaje kwa wafanya biashara wadogo na wa kati? Hilo liko wazi kodi ni jambo ambalo hakuna mfanya biashara anataka kulisikia.

Hakuna mfanyabiashara atakaelalamika ikiwa mfumo wa kukusanya kodi ni dhaifu, hayupo. Maana mifumo dhaifu ya kukusanya kodi ni faida kwa wafanya biashara.

Siku zote wafanya biashara hawako tayari kulipa kodi kwani itawapunguzia mapato yao.

Hizo nchi za ulaya hawabembelezani kwenye kodi na kila mwananchi anajaza tax returns awe na kazi awe hana kazi. Nchi zote zilizoendelea hawana cha msalia mtume kwenye kodi.

Sisi tunabembelezana kuhusu kulipa kodi halafu tunaenda kuomba msaada na mikopo kwa watu ambao hawabembelezani kwenye kodi, hizi ni akili ama matope?

Tanzania nchi yenye watu 60m inaenda kuomba msaada Finland nchi yenye watu 5m wakazi wa Dar tu wanazidi wananchi wa Finland, ama Norway 5m ama Sweden 10m, hii ni akili kweli? Na sababu no moja tu, Finland kila mtu analipa kodi na hakuna kubembelezana na ukikwepa kulipa kodi unafilisiwa kabisa.

Mama ameanza kupenda cheap popularity, ameanza kucheka na nyani atavuna tu mabua.
Ingependeza zaidi kama ungejikita kwenye kauli zake specific, na kuchambua kauli hii ina madhara haya, zaidi ya kutoa tuhuma za jumla tu.

Nchi ina mfumo wa kodi za kionevu na zisizo wazi. Kutoza sana kodi kunaua biashara.

Haya ni mambo ambayo wachumi wanayajua yamesemwa kuanzia enzi za Ibn-Khaldoum (1381) mpaka Arthur Laffer katika "Arthur Laffer's Curve".

Tunapojadili na kukosoa, tujadili kwa vigezo vya data.Sio unakosoa huna hata reference ya kisomi moja tu!

Hebu jifunze Laffer's Curve hapa kwanza.



 
Isingepata kodi wapi? Toka kelele zimeanza kupigwa, ndo kwanza mapato yalikua yanaongezeka kila mwezi. Kwa ufupi, mama kaingia mtegoni, huku kwenye kodi asingepagusa kabisa. Miradi yote itasimama, tutaanza bakuli tena.
Unafanya biashara gani?
100% kila siku kampuni zinafungwa kwa nini unakuwa mvivu!
Nenda ata serekali za mtaa wata kuambia utashangaa! Biashara zinavyo fungwa kwa speed ya hatari!
Akuna kitu kitacho haribu ukuwaji wa ubongo wa mtu kama kutokuwa mdadisi!!
Jifunze kudadisi kutafakari kabla ubongo wako hau jafa nusu hutaweza kuufufua tena!
Me sipo jamiiforum kufanya mizaha!
Biashara nyingi kwa wamiliki kutambua au kuto kutambua faini wanazo lipa TRA sasa hivi pamoja kodi wanalipa kwa kutumia mtaji na mishahara pia wana lipa kwa kutumia mitaji yao!

Nisuala la muda!
Msimamishe kibarua yeyote anayefanya kwenye kiwanda au kampuni yeyote iliyopo karibia na pande zako muulize tu vipi uzalishaji upoje hko kazini kwenu?
Vipi biashara ina fanyika?
Ndio utajua ni wapi mzee alikuwa ana tupeleka!
 
Mimi nataka Kila mtanzania alipe lkn Hawa wanao lalamika kwenye mitandao naomba nao watuonyeshe wanavyo lipa sio kutaka wengine ndoo walipe wakati wote tunajenga tz,na ningeshauri nida tuwe tunalipia angalau 500 kwa mwezi,hii ni hela nyingi sana,msipende wengine wakamliwe,wote ni watz,tunajenga tz,iwe fahari kwa Kila mtz kuonyesha unavyo lipa,Kama wewe hulipi kaa kimyaa,shida yetu kwenye mdomo tuko vzr lkn kwenye action ni ziro distance,nawatakaia karume day
Kila mtanzania analipa kodi. hata mtoto mdogo analipa kodi. Kuna hii Value added Tax (VAT), hiyo ni kodi. Imo kwenye kila bidhaa za viwandani unazonunua dukani na baadhi ya huduma mfano huduma za mitandao ya simu. Ukinunua vocha kuna VAT mle. Sasa nirudi kwenye hii kodi anayotakiwa kulipa mfanya, biashara. Analipa kwasababu anafanya biashara, kwenye mazingira ya Tanzania. Lakini pia hata hawa wafanyakazi nao pia walipa kodi. Tena watu wanao ongoza kulipa kodi bila kusumbua tena bila kutumia nguvu ni wafanyakazi. Wao kodi inakatwa moja kwa moja kwenye mshahara wao.
 
Back
Top Bottom