Mama Samia ameingia kwenye mtego wa wafanyabiashara kubembelezwa kulipa kodi, tumekwisha!

Ingependeza zaidi kama ungejikita kwenye kauli zake specific, na kuchambua kauli hii ina madhara haya, zaidi ya kutoa tuhuma za jumla tu.

Nchi ina mfumo wa kodi za kionevu na zisizo wazi. Kutoza sana kodi kunaua biashara.

Haya ni mambo ambayo wachumi wanayajua yamesemwa kuanzia enzi za Ibn-Khaldoum (1381) mpaka Arthur Laffer katika "Arthur Laffer's Curve".

Tunapojadili na kukosoa, tujadili kwa vigezo vya data.Sio unakosoa huna hata reference ya kisomi moja tu!

Hebu jifunze Laffer's Curve hapa kwanza.


 
Isingepata kodi wapi? Toka kelele zimeanza kupigwa, ndo kwanza mapato yalikua yanaongezeka kila mwezi. Kwa ufupi, mama kaingia mtegoni, huku kwenye kodi asingepagusa kabisa. Miradi yote itasimama, tutaanza bakuli tena.
Unafanya biashara gani?
100% kila siku kampuni zinafungwa kwa nini unakuwa mvivu!
Nenda ata serekali za mtaa wata kuambia utashangaa! Biashara zinavyo fungwa kwa speed ya hatari!
Akuna kitu kitacho haribu ukuwaji wa ubongo wa mtu kama kutokuwa mdadisi!!
Jifunze kudadisi kutafakari kabla ubongo wako hau jafa nusu hutaweza kuufufua tena!
Me sipo jamiiforum kufanya mizaha!
Biashara nyingi kwa wamiliki kutambua au kuto kutambua faini wanazo lipa TRA sasa hivi pamoja kodi wanalipa kwa kutumia mtaji na mishahara pia wana lipa kwa kutumia mitaji yao!

Nisuala la muda!
Msimamishe kibarua yeyote anayefanya kwenye kiwanda au kampuni yeyote iliyopo karibia na pande zako muulize tu vipi uzalishaji upoje hko kazini kwenu?
Vipi biashara ina fanyika?
Ndio utajua ni wapi mzee alikuwa ana tupeleka!
 
Kila mtanzania analipa kodi. hata mtoto mdogo analipa kodi. Kuna hii Value added Tax (VAT), hiyo ni kodi. Imo kwenye kila bidhaa za viwandani unazonunua dukani na baadhi ya huduma mfano huduma za mitandao ya simu. Ukinunua vocha kuna VAT mle. Sasa nirudi kwenye hii kodi anayotakiwa kulipa mfanya, biashara. Analipa kwasababu anafanya biashara, kwenye mazingira ya Tanzania. Lakini pia hata hawa wafanyakazi nao pia walipa kodi. Tena watu wanao ongoza kulipa kodi bila kusumbua tena bila kutumia nguvu ni wafanyakazi. Wao kodi inakatwa moja kwa moja kwenye mshahara wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…