The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 11,197
- 14,771
Habari wakuu!
Tanzania inapita kipindi kigumu katika historia yake ya siasa za kiti cha urais. Niwaelezee wachache:
1. Nyerere
Huyu alipofariki mwaka 1999 nilishuhudia msiba wake. Kipindi hicho nilikuwa Lindi vijijini. Nilishuhudia kwa macho yangu watu wakilia msiba kama amefariki ndugu wa karibu. Pale kwenye kumuaga walizimia si watu chini ya 20 kwa huzuni. Japo alikuwa na wapinzani wake kama Kambona katika nyakati yake, ndani na nje alimaintain kuwa maarufu.
2. Mwinyi
Huyu alisifika kuwa mtu wa haki, mchamungu na asiyependa mawaa serikalini. Watanzania walimpenda sana. Siku anastaafu alipewa zawadi uwanja wa Samora pale Iringa – si chini ya maelfu matatu ya zawadi.
Japo hata yeye alijuta kuhusika na mikataba michafu ya mbuga zetu za wanyama, na kwa uzembe wake wanyama kibao walibebwa na Waarabu. Ni udhaifu wa Wazanzibari kujipendekeza kwa Waarabu wakiamini ni wao. Ila mpaka anafariki, aliondoka akiwa mioyoni mwa Watanzania, hususan kwa sababu alipostaafu aliishi mbali na siasa za chama, akabaki kuwa mzee wa taifa lote.
3. Kikwete
(Kabla sijamuongelea naomba ninywe maji kidogo… gudugudugudu…haaaa 😅). Najua wengi wanamchukia. Mimi pia simchukii ila nimeishusha heshima yake.
Kikwete alipoingia, kutokana na hisia za Watanzania wengi tuliokuwa ndani ya CCM, tuliamini kuna nguvu kubwa ya wivu iliyokuwa ikizuia nyota yake kali kupewa urais. Kimsingi, urais wa Mkapa ulikuwa wake. Ila huyu Mkwere alionesha ukomavu sana kwani alimtumikia Mkapa bila kinyongo na kwa heshima kuu.
Aidha, alijitahidi sana kwenye demokrasia na kuishi vyema na wapinzani wa serikali yake (walikuwa wanaenda kunywa chai Ikulu). Kitabia, Kikwete ukweli ni mtu mwema sana kwa binadamu yeyote. Lakini kutokana na udhaifu wake wa kuamini marafiki, alijikuta amejaza “watoto wa mjini” kwenye kazi – kama kina Ditopile, Kapuya n.k. Kukawa na wizi sana mawizarani na makashfa ya Escrow – yote yakawa matokeo ya usimamizi wake duni.
Huyu alistaafu kwa heshima zote. Alipojiharibia ni kutokubali kustaafu na kukaa benchi, akaendelea kushiriki makosa ya Mama kwa kigezo cha kupenya kuwa mshauri. Sasa Kikwete ana ushauri gani huyu? Wa kumpenyeza Mama bila ushindani? Nimeacha kuendelea maana huyu kashatoka mioyoni mwa Watanzania.
4. Magufuli
Huyu alipata umaarufu pengine unakaribiana na Nyerere kabisa. Alijua madhaifu na hasira za wananchi juu ya utendaji mbovu wa Kikwete. Akajikita kurekebisha – alianza kuondoa mitandao ya wezi wa kodi bandarini mpaka wengine wakajifilisi kwa kuogopa kukaguliwa.
Tatizo, alijisahau akaanza kutumia cheo kupambana na wabaya binafsi akiwemo Manji. Hakujua urais ni nafasi ya kiroho na takatifu (assistant God). Pia udhaifu wake kimaumbile – ni mpenda sifa na hapendi kosolewa. Ilimgharimu.
Aidha, hakuwa na elimu ya uchumi na sheria. Japo alikuwa na nia njema, alifanya maamuzi ya kijinga mengi yaliyotugharimu – ikiwemo kununua ndege mbovu na kuvamia mikataba ya madini kiholela. Lakini pamoja na yote, Watanzania walimpenda, aliondoka yuko moyoni mwao na walimlilia kweli kweli.
5. MAMA SAMIA
Nimeandika kwa herufi kubwa makusudi. Naomba niseme toka moyoni – bila chuki binafsi wala ushauri wa maslahi yeyote. Mungu anisaidie.
Asee Mama, hivi unaishi Tanzania kweli? Maana suala la kuwa Watanzania hawakutaki liko wazi balaa. Naomba usitume hao wa ofisini kwako kuwa wajanja kama Magu, yeye aliunda wakwake. Wambie wakurekodie vijiwe vya kahawa – wanakusemaje.
Watu hawachukii Uzanzibar wako – je, mbona hawakumchukia Mwinyi? Hawachukii uanamke wako – naamini atakuja Rais mwanamke na atapendwa. Watu wanachukia mambo haya:
Ingia mitandaoni. Je, unajua siasa sio coverage number one?
Kimsingi hakuna anayefuatilia uchaguzi. Mada zinazoongelewa ni:

- Ulivyojifanyia mkataba wa kuachia bandari na misitu yetu kwa Waarabu, na kutumia wapuuz (wasanii, waandishi, wabunge kama Msukuma) kusukuma hilo kwa nguvu licha ya kila taasisi kukukataza. Nauhakika Rais ajaye atakuja kuvunja yote.
- Utajiri wa waliochini yako usiomithilika. Hili sina ushahidi, ila mama, maneno mtaani ni kwamba mwanao Abdu ana assets za mabilioni alizopata kipindi chako kifupi wakati juzi tu alikuwa muuza matairi wa kawaida.
- Kikwete – huyu yuko branded na Watanzania kama mwana mtandao mtiifu wa Rostam. Mimi nimesikia tu, sijui vyema, ila vijiweni wanamchukia kuliko shetani. Yeye ndiye alishindwa kukushauri juu ya kuuchukua ugombea kiufundi. Sasa leo tunaamini wewe sio mgombea halali wa CCM.
- Lissu – nimeamini Watanzania ni ndugu. Laiti ungejua mamilioni wangapi wanamlilia Mwenyezi Mungu juu ya Lissu, niamini, hutaiacha dunia bila kujuta. Watanzania (akiwemo Kikwete) wanaamini unamuogopa na unamtesa bila hatia. Hata ukimuachia – bado wanaamini hufai.
- Utekaji – hii hata watoto wa chekechea wangeweza kukuambia. Wanaotekwa lawama 100% ni wewe. Sasa mtu kama Mdude – unatoa wapi macho makavu ya kutoongelea?
Ingia mitandaoni. Je, unajua siasa sio coverage number one?
Kimsingi hakuna anayefuatilia uchaguzi. Mada zinazoongelewa ni:
- Giggy Money kugombana na Anko T – sio sera zako.
- Diamond na Mbosso kugombana juu ya power.
- Zuchu kukosewa heshima na Wakenya.