Mama Samia: Paul Makonda alisimama ndani ya Bunge la Katiba na kusema mimi nafaa kuwa Makamu wa Rais na Bunge zima likashangilia!

Mama Samia: Paul Makonda alisimama ndani ya Bunge la Katiba na kusema mimi nafaa kuwa Makamu wa Rais na Bunge zima likashangilia!

Hivi Mbunge ana nguvu kuliko Mkuu wa Mkoa ?
Tena mkoa kama DSM.?
Hujui kuwa akitokea mkuu wa mkoa mtoto wa baba kama alivyokuwa yeye basi hawezi hata kufurukuta kwenye hilo jimbo!!
Mkuu wa mkoa wa DSM ni mtu mkubwa sana ! Ni mbunge gani anaweza kumwita Mfanyabiashara na kumpa kazi yoyote anayoitaka ifanyike na ikafanyika!!
Mkuu wa mkoa wa DSM hata mawaziri wanamuheshimu.
Hapo sasa tutaanza kutafsiri ukabila lakini sio vinginevyo. Kijana anachagua anachotaka yeye na sio jamii au mkuu wa nchi aliyempa kazi ya kumsaidia kujenga mkoa wake na anakimbilia jimbo tena lililokua Tarafa tu miaka ya nyuma.
Acheni kusifia mambo yasiyofaa.
Wajumbe wameona Ndungulile anafaa kuendelea na ni mwanachama wa CCM sisi tuheshimu maamuzi yao.
Na mwenyekiti alisema mahali penye Mbunge wa CCM atakayepitishwa kuendelea basi asipingwe. Yani yeye ni Mbunge aliyepo tumkate ili asubiri uteuzi wakati kuna mtu mwenye tamaa amekataa uteuzi na Ubunge ukamkataa kwenye kura za maoni.
Huku kubwebwa namna hii ni ili tu afaidi kodi za watanzania au ni kwa manufaa ya nani?
Ndio maana nchi zetu tunarithishana visasi.

Akitokea Rais mwingine huko mbeleni ndio maana Mara nyingi Mali za watu kama hao zinafanyiwa figisu mpaka wafilisike mana wanaonekana wazi walikua wanatafutiwa namna ya kula kodi ya wananchi huku wengine wakionekana hawafai na wanakatwa bila sababu.

October ni uchaguzi wa Vyama vingi kumbuka hilo ,CCM.
Nimekuelewa bwashee!
 
Kumbuka Ubunge unapingwa Mahakamani .
Lisu amerudi na watu wana data zote za lile jina halisi la yule mtu.
Yeye asubiri uteuzi tuu lakini sio ubunge wa kuchaguliwa.
Alikosea sana huyo kijana .

Nitaamini kabisa kuwa nchi hii kuna ukabila na urafiki mkubwa katika utawala.

Huyo kijana alipewa heshima kubwa sana kupewa ukuu wa mkoa wa DSM. Ni mtu asiyefaa tu na mwenye tamaa anayeweza kuacha nafasi ya ukuu wa mkoa mkubwa kama DSM na kukimbilia Ubunge wa jimbo. Tamaa tu ndiyo inayomwandama. Na yote hiyo ipo wazi huyo mtu sio msafi ndio maana anakimbilia Ubunge mana kula ukishachaguliwa hakuna kutumbuliwa.

Umri wake bado ni mdogo alikua na nafasi ya kumsaidia mh. Rais kwenye nafasi yake aliyoaminiwa ya Ukuu wa mkoa na baada ya miaka kumi angegombea Ubunge baada ya Rais kustaafu.
Sasa amekimbia kazi iliyompa umaarufu na kukimbilia Ubunge akilenga Uwaziri.

Na pia tunatatizo la kuwa na nchi inayoamini katika kutumia nguvu kwa kila kitu badala ya akili ndio maana kila mtu analenga ubunge na uwaziri na utawala ili awaendeshe watu kama Punda na sio kama watu wenye akili ya kukosoa na kutoa wazo mbadala.

Makonda hastahili kabisa kabisa kumtoa Ndungulile kwenye Jimbo kwa sababu tu ya kabila lake.
Noo,tusiwe na taifa la namna hiyo. Alipewa heshima kubwa sana kuwa mkuu wa mkoa mkubwa kuliko na wenye pato na mipango mikubwa sana kuliko hata baadhi ya Wizara. Sasa anataka nini ? Wakati wapo vijana wengi sana wa umri wake ambao hawana ajira na wana maisha magumu sana na wengi wana Elimu na uwezo mkubwa kuliko yeye.

Kama Makamu wa Rais anaona huyo Makonda basi amrudishe kwenye kazi yake ya awali kwenye Chama na Serikali.

Uchaguzi huu CCM wasiubeze sana. Huku uchaguzi ndio utakaoamua urahisi au ugumu wa Rais atakayekuja wa awamu ya sita 2025- 2030. Wakiwapuuza wajumbe basi wanaweza wakawapitisha watu wao mwaka huu ila 2024 CCM itapasuka vibaya sana na Lisu atachukua nchi kirahisi au Membe.

Wajumbe ndio wanaopiga kampeni Nyumba kwa nyumba,kitanda kwa kitanda.Mkitumia mamlaka yenu kuwapuuza wajumbe mjue mtawatisha wale wagombea lakini wapiga kura watasikiliza kauli za wajumbe.

Wajumbe wanapiga kura kutokana na maoni ya wananchi wanaowazunguka mana wao ndio wanaowajua. Ndio maana wote walioshindwa hakuna mwananchi anayelalamika zaidi ya wao wenyewe.

Kama ubunge una maslahi na ulinzi mzuri kuliko Ukuu wa mkoa basi tujue kabisa hata Huyo mtoto wa mkulima Dr .Andungulile naye anautaka na aliutafuta kwa nguvu zake mwenyewe bila kubwa wakati mwenzake anataka kubebwa na alibebwa pia na uRC wake.

Mungu atuepushie mbali na vijana wadogo wenye tamaa Kali kama huyo Paulo. Watu wanatamani hata ukatibu tarafa hawapati tena wana mpaka Digrii za masters.

Nitashangaa sana kama watamuacha mtu makini aliyepigania hilo jimbo la Kigamboni mwaka 2015 wakati ule wa mafuriko eti kwa sababu ya utabiri wa umakamu wa Rais. Hivi waafrika tumelogwa na nani?
Kusema tu kuwa Fulani unafaa kuwa Dereva au mvuvi basi inatosha kupuuza maoni ya Wajumbe zaidi ya 400?
Hapana Demokrasia iheshimiwe kwa kweli .
Kwanza hatukupewa nafasi ya kuwasikiliza kuwa ni kwa nini wameamua kugombea Ubunge na wana mikakati gani ya zaidi.!!
Bwashee umeongea kwa uchungu sanaa. Polee siyo yote yanayofanyika duniani yatakufurahisha mengine yapo juu ya uwezo wako. Ndio hivyo Makonda ni next MP wa kigamboni.
 


posti hiyo ya ukurasa wa BUNGENI LEO INAONESHA JINSI ALIVYOTABIRI, JAPO ALITABIRI PIA MIZENGO NDIYE ATAKAYEKHA RAIS
Haha ha, kumbe pamoja na Jiwe kumpenda sana Bashite lakini hakuwa chaguo la Moyo wa Bashite?
Kwa maana halisi ni kwamba Jiwe anajigonga tuu kwa Bashite, mapenzi ya Bashite yako kwa Pinda.
cc; Ikulu Chamwino
 


posti hiyo ya ukurasa wa BUNGENI LEO INAONESHA JINSI ALIVYOTABIRI, JAPO ALITABIRI PIA MIZENGO NDIYE ATAKAYEKHA RAIS
Ukimsikiliza vizuri makonda utakuja kugundua sio mtu wa kawaida kwenye hii nchi japo wengi tunamchukulia poa ila muda utaongea yetu macho
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
Ndiyo maana alipewa zawadi ya ukuu wa Mkoa
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
Kwa hiyo tumchukulie exRC ni MTABIRI? MPIGA RAMLI? NABII? MGANGA WA KIENYEJI? Je haya yanahusiana vipi na UROHO WA MADARAKA? Je aliwaambia nini kina Rizwan au Ben6?
 
Agenda ninayo iona hapa ni kutaka kumpenyeza makonda kinamna baada ya wajumbe kumvimbia.
Dalili iko wazi kabisa....hapa wanajaribu kupima reaction ya wananchi/wapigakura ukiacha 'wajumbe'.
 
At his age,bado Makonda ana nafasi kubwa tu kwenye siasa za nchi hii kuliko watu wanavyofikiria.
Umri alionao unaweza pia kuwa ni kigezo cha kuwa na muda wa kutosha kujizika kikamilifu kwenye siasa za Tanzania.

Kuna wengi ambao waliwahi kuwa viongozi wajati wa ujana, na ikawa ndiyo mwisho wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugulile awe makini sana na usalama wake, asijwe akapigwa ' juju' hapa majuju ni mengi sio lazima iwe uchawi
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu unakumbuka ulivyotokwa povu huu uzi.

😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom