Mama Samia una wabunge 90+% futa vyama vya upinzani

Si mlikuja na mkwara kuwa mtatumia wembe ule ule mletegemea rais akae kimya? Piga spana tu.
 
Mkuu, kwa nini unampa ushauri mbaya kiasi hiki; ina maana kwamba umekata tamaa kabisa juu yake kuhusu yale mapenzi ya mwanzo?

Mpe ushauri mzuri, pengine atakusikiliza.
Huu ushauri uliompa ni kama unatoka kwa mtu adui yake mkubwa sana kwake anayetaka kumharibia kila kitu.
 
Makundi mangapi amekutana nayo,Pemba huko mikusanyiko ilikuwepo kwenye kampeni,CCM kila uchwao wanakusanyika.korona haikuwepo ila vyama vingine vinasababisha korona.Tuache unafiki wakumpamba,pakichafuka wataumia ndugu zetu hata yeye ataishi kiuadui kisa vyama.
FUTA VYAMA KIBAKI KIMOJA,BUNGE LINATOSHA KUPITISHA AGENDA KWA DHARULA.Kongamano lilikuwa sawa na walevi wanakunywa wakilewa wanaondoka.
Hakuna MTU alikuwa busy kusikia Mwanza kuna nini.USHAMBA WA MADARAKA
 
Mkuu Kabugula, nina hakika hukunielewa nilivyomjibu mkuu 'AssadySyria' kuhusu ushauri wake kwa rais.

Kutokana na jibu lako hapa, ni wazi tupo sehemu moja.

Ushauri wa kufuta vyama kwa sasa ni ushauri mbaya kabisa, tena usio na tija kwa nchi.

Kufuta vyama ndiko pengine kutachochea zaidi kuondoka kwa CCM mapema sana, licha ya kwamba Samia hana huba ya kufanya kitu kama hicho.
 
Nilikuelewa,kufuta nikukazia aone uzito wa jambo
 
Nilikuelewa,kufuta nikukazia aone uzito wa jambo
Si ndipo atakapokuwa ameharibu kabisa, maana AssadSyria alieleza kwamba alikuwa na mapenzi naye mama.

Huwezi kumshauri mpenzi wako jambo ambalo litamharibia zaidi, au sio?
 
Si ndipo atakapokuwa ameharibu kabisa, maana AssadSyria alieleza kwamba alikuwa na mapenzi naye mama.

Huwezi kumshauri mpenzi wako jambo ambalo litamharibia zaidi, au sio?
Katumia fumbo tu na fasihi ili mama ajichanganye zaidi.
 
Uhalali wa hao wabunge je ulipatikanaje.
Ni wabunge wa serikali au ni wa wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…