Mama Samia : Utafiti unaonesha Zaidi ya nusu ya Tanzania wenye umri wa kuoa au kuolewa hawajaingia kwenye ndoa . Je sababu yako ni nini ?

Sababu kuu ziko tatu.

1. Mke anadai vitu vya gharama kubwa ambavyo havina umuhimu (k.m. wigi la laki tatu, i-phone latest n.k.). Kijana akishajua akimwoa binti atadaiwa vitu hivyo, hawezi kumwoa.

2. Umasikini wa mwanaume kukosa kipato kunamfanya mwanaume awe na msongo wa mawazo saa zote. Kwenye msongo kama huo, hata "wajibu wa chumbani" unamshinda mwanaume.

3. Kijana anataka msichana mwenye uzuri wo-o-te huku hajui kila mwanaume atamtaka. Akiwa bado anachumbia, anagundua binti ana wanaume kibao wenye pesa wanamfuatilia. Hata kama binti hajawakubali, kijana wa kiume hawezi kumwoa kama huyo. Ndio maana unakuta mabinti weeeengi wazuri sana hawajaolewa
 
Zile ajira ambazo vijana wanategemea kupata pesa ili kutunza familia nazo zinachukuliwa na wanawake...Acha vijana wajitafute
 
Waoe then wawalishe nini? Vijana wengi hawana means za kuwaingizia kipato au kipato ni kidogo sana hakikidhi standards za maisha.
 
Mwaka huu serikali inatarajia kutoa ajira zipatazo 25,000/= katika ajira hizi vijana wa kiume wapatao 12000 wataajiriwa katika kada ya Afya na ualimu . Inatarajiwa ndoa 10, 000 zitatokea ndani ya mwaka huu .

Hivyo tatizo hapa ni kuwa vijana wengi hawana maisha wengi wapo mtaani wanabangaiza tu. Vipato bado vinawapiga chenga jambo linalopelekea wengi waogope kujitwisha majukumu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…