The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Spika Wa Bunge La Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dk Tulia Ackson amesema licha ya kuwepo kwa Juhudi mbalimbali za kuwainua Wanawake Katika Nyanja Mbalimbali Ikiwemo Uchumi na uongozi lakini bado kundi la Wanaume wana wajibu wa kuendelea kuwasaidia Wanawake ili kufikia viwango vya juu sawa na wanaume.
Akizungumzia katika Kongamano kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani lililowakutanisha wanawake wa mikoa ya nyanda za juu kusini na kufanyika jijini Mbeya kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wanawake ikiwa ni pamoja na namna ya kujikwamua kiuchumi na kibiashara pamoja na mchango wa wanawaume katika miaka 30 ya Beijing.
Aidha Dk Tulia amesema bado wanawake wanaitaji kushikwa mkono ili kufikia viwango walivyo fikia wanaume, "Hatumaanishi tunaitaka Nafasi ya Wanaume hapana Bali tunataka na sisi tupewe Nafasi ya kufanya Mambo sawa sawa na wanaume na Mahala tunapokwama basi tushikwe Mkono tusiachwe"
Naibu Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya habari na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka Wanawake Kuendelea Kumuungo Mkono Rais Wa Jumuuri ya Muungano wa Tanzania Dkt: Samila Suluhu Hassani zaidi akiwakumbusha wanawake kuendelea kupambana kichumi kwakuwa mwanamke yoyote akifanikiwa hata familia yake inakuwa na misha mazuri.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara wa Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalumu Felista Mdemu ameeleza lengo la kongamano hilo kuwa ni kuendelea kuwakumbusha wanawake kujiimarisha kiuchumi na kuepuka utegemezi uliokithiri.