Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Labda wanaidharau jinsi ilivyo kazi enyewe, ila wangejua maokoto yako hapo wasingesema.

Wawaache wamama wa watu wajitafutie pesa zao wenyewe.
Kwa kweli hao kina mama wapige kazi kelele Wawa achie vyura
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.

This industry is all about shit.
Sijui lakini. Ila kaa ukijua kuna wazazi wabishi sana. Anaweza kuwa na mtoto profesa ila bado akawa anauza pombe za kienyeji.
 
nafikiri tatizo sio biashara ya mbogamboga shida hawa wasanii wanatabia ya kuigiza maisha na kutengeneza picha flani kwa watu kwamba maisha wameyapatia kumbe sio ualisia jambo ambalo ndio usani wenyewe na watu hawaelewi
Shida sio wasanii shida ni watanzania... Wamekariri baadhi ya biashara na kazi sasa wakiona mtu anauza mboga na mtoto no msanii wanashangaa wakati huo huo asilimia 95 nyumba nyingi Tanzania mboga mboga ndio mboga kuu kwa milo yote.
 
Vipi kuhusu baba yake?
Sababu ya historical background na sintofahamu nyingi, siwezi kusema sana kuhusu baba.

Kwangu mimi, baba anayesubiri mtoto atoboe ndio aje, sio baba.

Baba asiyeshare bond wala emotions na watoto anajiitaje ndio baba?

Ingawa kama mtoto umsaidie kadri unavyowezs
 
Wao si ndio wanawake maisha yao tuyajue mitandaoni? Sada endelea na Show Off harafu ukibroke uone kama tutaacha kukusema.

Kama unayaonesha hadharani inakuwaje usitake.kusemwa hadharani?
"Hadharani" Una maana gani, huo muda wa kuwafuatilia unapata wapi?
Usikubali kuwa dampo la kila habari, jifunze kuchagua vitu vya kufuatilia! Zingine ni takataka Tu!
1734672580190.jpg
 
Afu watu hawajui, Bustani za mboga zina hela balaa, nilishawahi fanya,
Ila mie walikua wanakuja bustanini wenyewe walanguzi, pesa nayopata hadi mwenyewe siamini.

Ni biashara nzuri yenye hela hatarii, mchicha, tembele, pitiku, sukuma wiki, mnafu, Chinese, spinach, etc
Pitiku ni mboga ya maboga.
Umechanganya na Kingoni Mlongo 😂😂😂
 
Kipato cha mtoto kinaamua mama au mzazi afanye kazi gani.
Sio asifanye kazi bali afanye kazi gani kulingana na kipato cha mtoto wake.

Mama kakusomesha kwa kuokota makopo. Umefanikiwa na unapesa unamuacha aendelee kufanya kazi yake ya kuokota makopo, kisa ana uzoefu nayo?
Upumbavu mkubwa!
Ukiwa na pesa harafu hauna ubunifu hata wa kutafutia mama yako aina ya kazi/biashara, hiyo sio pesa halali.
Halafu unakuta àna mabody guards anawalipa kumlinda, kwanini asimpe màma yàke hela?
Huu ni upunguani ndo maana wanalaaniwa na kuanza kusaga wenzao kama huyo martha.
 
Shida sio wasanii shida ni watanzania... Wamekariri baadhi ya biashara na kazi sasa wakiona mtu anauza mboga na mtoto no msanii wanashangaa wakati huo huo asilimia 95 nyumba nyingi Tanzania mboga mboga ndio mboga kuu kwa milo yote.
Hata kama anauza Je anauza kwa mfumo upi? Huwezi kusema biashara Fulani inalipa wakati faida hapo haizidi 5000 kazi hiyo pia ni ngumu kwa mtu mzima kusimama juani unauza mboga
 
Halafu unakuta àna mabody guards anawalipa kumlinda, kwanini asimpe màma yàke hela?
Huu ni upunguani ndo maana wanalaaniwa na kuanza kusaga wenzao kama huyo martha.
Msanii ni lazima alindwe vijana wanaingiza pesa nyingi asikwambie mtu
 
Kufanya kazi ni baraka, kufanya kazi ni lazima

Tangu kuumbwa kwa dunia Mungu alimwamrisha binadamu afanye kazi!

Na ndio maana alimpa Bustani ailime na kuitunza!

Kazi ni lazima haijalishi una pesa ngapi unless una afya isiyo njema au umri mkubwa
 
Afu watu hawajui, Bustani za mboga zina hela balaa, nilishawahi fanya,
Ila mie walikua wanakuja bustanini wenyewe walanguzi, pesa nayopata hadi mwenyewe siamini.

Ni biashara nzuri yenye hela hatarii, mchicha, tembele, pitiku, sukuma wiki, mnafu, Chinese, spinach, etc
Pitiku ni nini cocastic
 
Hamjui kuna familia wanakufanyia mambo ya ajabu unabali na watu baki kwenye maisha yako
 
Bimkubwa ana watoto wanne wakiume wote tunajiweza. Ila kila siku jioni anapika mikate anauza ambapo faida yake kwa siku ni kama 6000. 6000Tsh ndio faida yake kwa siku pesa ambayo anaiweza kuipata bila kufanya kazi,ila anaskia raha kuifanya ile kazi yake na kuzalisha kipato chake hata kama kidogo.
Na inampa afya ya akili kukaa bila kazi sio vizuri
 
Afu watu hawajui, Bustani za mboga zina hela balaa, nilishawahi fanya,
Ila mie walikua wanakuja bustanini wenyewe walanguzi, pesa nayopata hadi mwenyewe siamini.

Ni biashara nzuri yenye hela hatarii, mchicha, tembele, pitiku, sukuma wiki, mnafu, Chinese, spinach, etc
Hongera sana bibie.
 
Back
Top Bottom