Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Kama Mama Rayvanny ana furaha na maisha yake inatosha. Ni kosa kubwa sana la kiufundi kumzuia mama kujishughulisha kisa umekua tajiri. Kukaa tu inaweza kumletea shida za kiafya. Bora awe ACTIVE. Bibi yangu enzi za uhai wake alikuwa akitumiwa pesa kila mwezi na wanae kama mshahara ila kamwe hakuwahi kuacha kufanya shughuli zake ndogondogo. Ukimtembelea unamkuta yuko bize. Hadi anafika miaka zaidi ya 80 alikuwa na uwezo wa kutembea hadi 1km bila kuchoka.
 
Unawafahamu vizuri wanawake wa Mbeya? Huwa hawapendi kusubiri kuletewa mezani. Wanapenda kuchakarika.

Mbali ya hiyo, mkuu mama zetu wako tofauti kidogo, hawawezi kukaa Asubuhi mpaka jioni kisa ana mtoto wa kumletea mahitaji.
Hata kusafiri tu mbali na miji yao ndani ya wiki 1 , utamsikia kuku wangu kule nyumbani, nyumba yangu kule nyumbani.
Ndiyo maana bado wako na stamina.
 
Kuna vitu vipo kiroho zaidi kwa wanaoelewa wataelewa. Sijui niite umaskini au kukataa mabadirko kuna watu hata uwasaidie vipi watabaki jinsi walivyo. Kuna watu miaka na miaka analia hana mtaji ataenda bank atakopa, ndugu watasaidia ila wimbo wake haubadiriki kamwe. Hii ya kuuza mboga na juice haimanishi hawa watu hawasaidiwi. Biashara yoyote ina faida ni wewee muuzaji uamue uiweke daraja gani. Kuna ndugu yangu anauza maziwa kwa mwezi anakunja 3m achilia mbali wale wateja wa rejareja wa kila siku.
 
Acha kufuatilia maisha ya watu


Ww mother wako unampa mahitaji?
 

Attachments

  • 5904201-c718b1a3ef83d67f79ef3cec17c4152.mp4
    153.1 KB
Nenda kasome story ya Emanuel Adebayor, Emmanuel ebou,mwakinyo hao wote wametengana na familia zao ila ukitaka kufa masikini endekeza ndugu unawasaidia ila hawana shukran na wakishakuwa na ndugu maarufu hawataki kufanya kazi.

Nenda YouTube kaangalie interview ya samata na Salama utanielewa vizuri.
 
Mimi huwa siwaelewi watu wanaodharau kazi za watu wengine. Nani alisema hii ni bora na hii ni ya hovyo? Kwanini umpangie mtu na familia yake kitu cha kufanya? Wewe familia yako na ukoo wako, je wote mna hizo kazi nzuri unazosema?

Acheni watu waishi maisha yao halisi, wanayofurahia na kuzoea. Tukianza chunguza kila mzazi nini anafanya, utarudi kuomba hii thread ifutwe. Bora atafutaye vya halali, kuliko vya kudhulumu, kutapeli, kuiba. Kila mtu akiwa na hiyo so called kazi nzuri nani atamtuma mwenzake au kupata mahitaji mengine?
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.


This industry is all about shit.
Si kwa ubaya ila wapo wazazi ambao wanaamini katika jitihada juu ya kile kilichowatoa katika maisha kuliko kutaka kujikweza ,kwa maana si kila unapofanikiwa watu wanapenda maendeleo yako maana kuishi na binadamu ni kazi sana
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.


This industry is all about shit.
Sasa kama wanapata faida wasiuze?
 
Hizo si ndio kazi za majority ya Watanzania ? Tena bora hizo legal wengi wametoboa kwa kusomeshwa na wazazi wao wakiuza mpaka gongo...., That said mdau unadhani hao wasanii wanapata wapi pesa (Ukiwaona Insta au kwenye Luninga hapo wanauza Lifestlye..., they need to portraly stardom, hata kama wanaishi kwa kupiga mizinga unataka na kwenye video zao waonyeshe wanapiga mizinga ?

That said wewe ni lini mara ya mwisho umenunua kazi ya msanii (kununua na sio kudownload bure) au umekwenda show lini (Zingatia hio ndio moja ya money stream ila kumbuka hata hizo show na video msanii anapata percent kidogo tu nyumba yake kuna wadau kibao wanakinga mikono)...

Nadhani wengi tunapeleka lawana zetu ndipo sipo (kwa hawa tusiowalipa na wanajitahidi) kuliko kuzipeleka kwa wanaohusika tunaowalipa (watunga sera / overpaid, underperforming prima donnas AKA Politicians).., hao wangefanya kazi zao hawa kina mama wangekuwa kwenye ajira za kupata ujira.., na sio kutegemea watoto wao wakiitwa kwenye show ili wagawiwe makombo
 
Ulitaka wakae bila kufanya kazi halafu wale nini? Watoto wao warithi nini?
Hata kama mtoto wako ni tajiri kiasi gani kufanya kazi ni lazima.
Labda wanangu waje kunifanyia hivyo mimi lakini mimi siwezi kuruhusu mama yangu mzazi akaokote makopo apimie juisi akauze.

Kama case ni lazima afanye kazi ndiyo ale basi nitamboreshea mazingira kwa kumnunulia vifaa wezeshi kuifanya hiyo kazi,kwani hizo juisi hakuna vifungashio special vinauzwa madukani mpaka aachwe akaokote makopo?
 
Na ukitaka kujua ilo kua Lina ukweli,subiri waumwe.
utashangaa utawaona wanatia huluma crouds Medea wakitaka sisi tuwachangie buku buku ili ifike laki Tano kwa ajili ya matibabu😂. kiufup wasanii wa bongo 90%wanaishi maisha ya propaganda.
 
Mimi nadhani tatizo sio wazazi kujitafutia bali ni mazingira ya kazi......

Ni fedheha kubwa sana kwa mtu unayejiweza kiuchumi huku mama yako anapita kuokota makopo akapime apate ridhiki.......

Ni fedheha kubwa kwa mtu anayejiweza mama yake kutembeza mboga mboga na beseni kichwani.....

Tumeagizwa tuwatendee wema wazee wetu.....

Moja ya Raha ya kujiweza kwa kijana ni kuwaboreshea mazingira ya kuishi wazee wake.....

Hata kama wanapenda kufanya kazi basi waboreshee kazi zao huku wakifurahia maisha.......
 
Back
Top Bottom