MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kama Mama Rayvanny ana furaha na maisha yake inatosha. Ni kosa kubwa sana la kiufundi kumzuia mama kujishughulisha kisa umekua tajiri. Kukaa tu inaweza kumletea shida za kiafya. Bora awe ACTIVE. Bibi yangu enzi za uhai wake alikuwa akitumiwa pesa kila mwezi na wanae kama mshahara ila kamwe hakuwahi kuacha kufanya shughuli zake ndogondogo. Ukimtembelea unamkuta yuko bize. Hadi anafika miaka zaidi ya 80 alikuwa na uwezo wa kutembea hadi 1km bila kuchoka.