Mama wa watoto 8 atorokwa na mumewe, aomba msaada

Watu wa vijijini wanaamini Uzazi wa Mpango ni kumzuia asizagamue/ asizagamuliwe.

Hivyo wanapinga sana kwa nguvu zote huku wakijificha kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu ya Zaeni Mkaijaze Nchi lakini pointi yao kubwa ni Mizagamuo tu.
Hatari sana..!
 
Uanzishwe mchango humu tumchangie. Sio kuchangia mpira na siasa pekee. Na akipendeza huyo mama, mjinga aliyekimbia majukumu anajirudisha. Na akina mama wasivyo na hiana, anapachikwa mimba ya 9.
 
Hata kama ni mimi nakukimbia,yaan yeye ikiingia tu imo na hajali kabisa uzazi wa mpango,clinic kumejaa mabango ya uzaz wa mpango alikuwa hayaoni

Ndo maana manesi huwa wanakuwa wakali yaan kila mwaka wanakuona una mimba tu,umekuwa ng'ombe
 
We umejuaje hajatekwa na kuuwawa? Kuna ushahidi gani katoroka?
Mke wake angesema kwamba mme wake haonekani nyumbani muda mrefu pengine kapotea au katekwa.

Lakini mke wake kasema kwamba, mme wake katoroka nyumbani kukwepa majukumu na ugumu wa Maisha.

Usicho elewa ni nini?

Au unataka kutetea upumbavu wa huyo baba mpumbavu?
 
Mtu aliyetekwa na kuuwawa na mtu aliyetoroka, yeye ametofautisha vipi?
 
Contact za mama zipo wapi??? Au tunampataje? Iwe watsup ya huyo police ikiwezekana.
Mh. Doroth gwajima,huyo afande mpambanie.
Kafanya jambo jema sana
Mngeomba muandaliwe utaratibu ili mtafutiwe wengi zaidi. Nchi nzima hali ni kama hiyo.
 
Mtu aliyetekwa na kuuwawa na mtu aliyetoroka, yeye ametofautisha vipi?
Wewe unathibitisha vipi huyo mme ameuwawa?

Mke kashatoa maelezo kwamba mume wake kamkimbia kutokana na ugumu wa maisha wewe unathibitisha vipi kwamba huyo mme ameuwawa?
 
Mambo mengine yanachekesha frankly.Ndio mwanamme kamkimbia,na ndiyo anahitaji kupata msaada,lakini wote wawili wamefikaje hapo,yeye na mume wake?Ni wazi kabisa kwamba ujinga ndio uliowafikisha hapo,kwa hiyo kama wasipopata msaada(I hope they will),wasimlalamikie mtu,ila wao wenyewe.Na huyo mwanamme popote alipo asakwe awajibishwe kufuatana na sheria zetu za nchi, na alazimishwe kubeba msalaba wake.Huwezi kusababisha tatizo halafu ukimbie.

All in all,jamani Mungu ametupa maarifa, akili,hekima,busara na utashi,ni lazima tuvitumie vitu hivyo ipasavyo kwa sisi wenyewe na jamii yetu .
 
Matusi hayasaidii, mama anataka msaada/mumewe.
Wewe na mumewe aliyekimbia mko sawa maana wote hamna Masada!
Weka Na.tutoe michango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…