Mama yako na Mke wako nani anastahili kukaa siti ya mbele ya Gari yako mnapotoka wote kwa pamoja?

Mama yako na Mke wako nani anastahili kukaa siti ya mbele ya Gari yako mnapotoka wote kwa pamoja?

Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Nitamuuliza ibenge
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Kwani kukaa siti ya mbele kuna kipi kizuri au kibaya anachokipata mkaaji?
Je kuna jukumu lolote atakuwa nalo mkaa siti ya mbele?
 
Ila Tanzania dah!!!!!! CCM itatawala milele,hivi kukaa mbele kunaongeza/kupunguza nini katika utu wako? Bosi wangu kipindi nipo MSI au MST alikua anapenda sana toka na kusafiri namie ila aligundua kua nafanya unafiki wa kujizungusha ili yeye ake mbele,ila kuna alinitolea uvivu na akanichana.......... Mr Ndibuka wewea kukaa mbele hakuondoi nafasi yangu ofisini,hata nikikaa nyuma mie ni bosi wako tu so kuanzia leo utakaa siti ya mbele uwapo namie........ Stop infantism,kukaa mbele au nyuma hakuondoi thamani ya utu wako....... Kwanini Maraisi hawakai siti za mbele,achilia mbali sababu za kiusalama?
 
Always anakaa siti ya nyuma gari lolote hata kama mbele hakuna mtu....

Hata nikiwa na Hilo gari.... Mama yangu hana muda wakung'ang'ania siti....... Ya mbele

Anapenda siti ya nyuma anakuwa more comfortable......
 
Mke anakaa mbele na mimi mume wake mama anakaa siti ya kati kati imeisha hiyo.............
 
Very simple. Katika gari yenye seat za mbele na nyuma kaa na mkeo mbele mama akae seat ya nyuma. Kama gari ina seat mbili za mbele tu, (pick up) itategemea kama mkeo anajua kuendesha basi mkeo aendeshe na mama akae naye mbele wewe ukae nyuma. Kama mkeo hajui kuendesha ni vema ampishe mama mbele. Hata hivyo syala la nani akae mbele na nani akae nyuma halipaswi kuumiza watu vichwa kwani popote utakapokaa utafika tu hatupaswi kusawajika eti kwa sababu mtu umekaa nyuma!
 
Back
Top Bottom